Kuna tofauti gani kati ya msukuma na mnyamwezi?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Nimejaribu kuangalia jamiii hizi mbili za wanyanwezi wa Tabora na wasukuma toka Shinyanga na Kanda ya ziwa.

Kiukweli hadi sasa nimeshidwa kuwatofautisha kati ya wasukuma na wanyamwezi japo mila na desturi inasemekana zinafanana lakini mi naona tofauti kwa sababu kila nikimuangalia mnyamwezi naona anafanana sana na mikoa ya Tanga au Pwani yaani naona watu wenye asili fulani ya umwinyi umwinyi na pia watu wasiopenda kuongea lugha ya kwao.

Na wasukuma wengi naona ni watu wanaopenda lugha yao, kabila lao wachapa kazi, wafugaji,n.k .

Lakini hapo hapo tunaambiwa mnyamwezi na msukuma ndugu, kwa mnaofahamu hebu tupe tofauti ya mnyamwezi na msukuma.
 
Mnyamwezi mzembe sana, kazi kulea vitambi lkn pia wanapenda umwinyi kupita kiasi lkn ni wababbe sana sana. Usijiloge kwa demu wa Kinyamwez utaambulia nakoz kama unabisha Muulize Nuh Mziwanda, Dogo Janja na K.Chokoraa
Wababe tena kiongozi ahaaa hahaha
 
Wanyamwez ni wasukuma kama walivyo wasukuma wengine

Shida inakuja kuwa wanyamwez walitawaliwa na waarabu ndo maana unawaona hawana maendeleo na hawapend kaz na hawapend kuongea kilugha chao
 
Mkuu mimi ni Mnyamwezi, wasukuma ni wajomba zetu kiasili. Wasukuma wana sub-tribes kama walivyo wanyamwezi , watu wengi wanawafananisha wanyamwezi na wasukuma kwa uhusiano huo wa zamani, pia ukaribu wao na sub-tribe moja ya Kinyamwezi inayoitwa Wayubi ( wayubhi) wanaopatikana kule Nzega na Igunga. Hawa wa Nzega na Igunga wanashabihiana sana na wasukuma maana wao pia wafugaji na lafudhi zao zinakaribiana sana. Wasukuma na wanyiramba wamejinasibisha sana na wanyamwezi kwa sababu ya historia ya wanyamwezi kama warriors enzi za Mtemi Mirambo , Isike , Nyungu ya mawe, Msabila na wengine. wasukuma hawana asili ya ujasiri , wao wana asili ya uchawi uliotukuka kama akina mwanamalundi nk.

Unyamwezi taifa ( Bara Unyamwezi)
Unyamwezi ya zamani ilikusanya mikoa ya Tabora, Shinyanga ( baadhi ya wilaya) , Singida, Baadhi ya maeneo ya Iringa ( njombe) Mbeya , na Mpanda. (baadhi ya maeneo , hasa huko Ikonongo)

Nyamwezi Sub-tribes

Wagalanganza, Wasenye, Wayumbu, Wanyanyembe, Wayowa, Wayubi, Walambo, Wawele, Wakimbu, na mengine mengi

Sukuma Sub-tribes

Wanyantuzu, ongezeeni hapa

NB: Kuna Hostoria inasema wanyantuzu wametokea South Africa , wanauhusianoo wa karibu na wazulu , refers Movement Zulu movement from South Africa to East ....
 
Wewe mwenyewe, umewachambua na kubainisha tofauti zao, jibu ndilo hilo.
 
Wewe mwenyewe, umewachambua na kubainisha tofauti zao, jibu ndiyo hilo ulilo nalo, ndicho kinachowatofautisha.
 
Wasukuma na Wanyamwezi!
Wanaonekana wanashabihiana hasa kwa lugha zao!
Tofauti yao sio kubwa sana! Lakini ukitazama katika lugha zao,Utaona utofauti mkubwa - Hapa Kinyamwezi kinapoongewa hata kama sio Mbantu ila unajua kiswahili utajua wanaongelea nini? Kwa sababu Kuna maneno mengi ya kiswahili yanatakwa kinyamwezi:
Kisukuma: Ng'washika?
Kinyamwezi: Mwafika?
Kisukuma: Ginehe?
Kinyamwezi:Vihe?
Na maneno mengi tu ambayo kiisimu yanawafanya wanyamwezi kuwa kabila lililoathirika sana na Upwani.
Ila Kiasili hawa watu wana blood line moja iliyokuja kugawanyika kutokana na intermarriage na kati ya makabila mengine.

MNYAMWEZI - HISTORIA NZURI - MZIGI MZITO MPE MNYAMWEZI!
Kauli mbiu hii(msemo maarufu) inatokana na Historia ya biashara za masafa marefu kati ya Waarabu na Makabila ya Bara.
Wanyamwezi walijulikana kwa kusafiri na kubeba bidhaa za Waraabu toka Bara kwenda Pwani( Pembe za Ndovu,shaba n.k) Walikuwa Wapagazi maarufu sana! Kufikia Mwaka 1850 Wanyamwezi walishajaa Dar ya wakati huo (Mzizima).
Ni eneo pekee magharibi walipompinga mkoloni kwa Nguvu na Kumshinda kwa nyakati fulani.
Watemi wao ni pamoja na ISIKE huyu aliwapinga wajerumani mpaka dakika ya mwisho wa uhai wake alipoamua kujilipua na baruti kuliko kujisalimisha kwa Wazungu.
Mirambo - Kiongozi wa Jeshi la Warugaruga, Aliwanyoosha waraabu waliotaka kupita unyanyembe bila kutoa HONGO (Tax) Sasa wakati wanapambana naye kuna Mzungu Stanley H.M alikuwa naye yupo kwenye mishemishe zake kumtafuta misheneri aliyepotea Dr. David Livingstone akakuta Mwarabu kabananishwa na Mirambo Mzungu akaamua kumsaidia Mwaraabu ili wapite BURE.Ni kwa mara ya kwanza Machine Gun! kutumika pale Tabora,Stanley alikuja na Mashine Gun kutoka marekani lakini ikafua dafu! Ndio alipoona wamezidiwa wakakimbia na akatamka amemuona Napoleon wa Afrika.
Wanyamwezi nao walishangaa kuona Bunduki ya kutoa risasi mfululizo hivyo wakamuita Stanley "Mpura Matale" Mvunja Miamba.
Ni watu wa kwanza kupanda ndege na kwenda Uingereza.(kalulu) ni kijana wa kinyamwezi aliyechukuliwa na Stanley na kwenda nae Ulaya.
Ni mashujaa wa enzi.
Harakati za Uhuru zilizozaa Mambo ya msingi wa Uhuru wetu zilizaliwa Tabora.
Wazee wa Kavu waliompinga Nyerere waziwazi walitoka Mkoa huu - Joseph Kasela Bantu,Chris Kasangatumbo,Chief Fundikira.
Ni wasafi sana! Mwanamke wa kinyamwezi akiamka asubuhi ni kuoga kwanza hata kama haendi wapi?

SIFA MBAYA
Ni kabila Masikini Jeuri! (Kufahamu hili fika Tabora) ndani ya masaa 24 utajua hawa jamaa ni Masikini Jeuri!
Fiksi sana! Wanajua kupiga Tiralila achaa.
Ni watu wa kufatilia maisha ya watu sana! (Gossips,backbite)
Huezi jua kama kakasirika au la!
Hawapendi kazi ngumu ngumu kivile.
Mwarabu amechangia sana kuwavuruga hawa jamaa! Mnyamwezi anamheshimu Mwarabu kuliko Mnyamwezi mwenzie! Anaacha kukuuzia wewe Kuku kwa 9000/- anaenda kuuza kwa Mwarabu 7000/-
Ndio hivyo kila jamii na Udhaifu wake.

MSUKUMA - HISTORI NZURI - NDUHU TABU.(Hakuna Shida)

Ni kabila linalofahamika kwa uchapa Kazi! Ni jamii ambayo wakati wamisheneri wanatafuta sehemu ya Kuishi walikaribishwa vizuri sana halafu kesho yake walijikuta wako peke yao! msukuma kasha kata mbuga zamani - Alihofia kukosa wachungaji wa mifugo yake,kwa sababu alijua wazi kuwa ujio wa wazungu ungeharibu scheme zake zote.
Ni kabila ambalo hawakupambana na Wakoloni na kujipatia sifa kama wanyamwezi (Waoga).

Sifa kubwa ya hawa jamaa ni Mtu maarufu sana Katika Historia ya Wasukuma alikuwa MWANAMALUNDI.
Huyu alikuwa balaa! Balaa kweli,Alikuwa na uwezo wa ajabu sana! Kuvuka maji/bahari kwa miguu,Kupanda mbegu na kuota hapo hapo! Kukausha mti kwa kunyoosha mkono tu,Kuweka maziwa yasingande kama ishara ya yeye kuwa yupo hai.
Ni wachapa kazi balaa!Unaposikia popote Tabora kuna chakula kingi ni wao ndo wakulima stadi.
Wakarimu sana! Mgeni kwao ni mtu wa maana sana.
Waungwana sana! Wapole mno
Wakibahatika kwenda Shule ni Mshale darasani - Dr. Chagula,Bob Makani,Jaji Francis Nyalali,Paul Bomani na Jiwe Dr. John Pombe Magufuli.

SIFA MBAYA.
Wachafu - Hasa jamii za Wafugaji unaweza usinywe maji kwao.
Wakatili wanapoamua kulipa kisasi ( Upole wao unapofikia mwisho)
Ni washamba sana! msukuma hawezi kugongwa na gari kwa sababu anaweza kuyasubiri hata kwa masaa 4 yapite ili naye apite.
Hawapendi shule aisee! Mpaka kukurukakara ya serikali.
Hawakati sweta!
Wanaamini na kushiriki sana mambo ya uchawi uchawi
Ndio hivyo sasa! Kila kabila na mapungufu yake.
 
Iyo highlight ya kijani, hamna shule hapo
 
Back
Top Bottom