Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,965
- 2,857
Habari za wakati huu
Kwa mujibu wa mwenendo wa maisha ya leo, ambapo athari nyingi hasa za kimfumo wa uzazi zinamwangukia mwanamke, ni vyema kuona anapata watoto mapema.
Ni nadra kwa mwanamke wa miaka 35 ambaye hajawahi kuzaa, apate ujauzito kirahisi. "Kuzaa ni afya" kwa mujibu wa daktari fulani. Katika hili kuna masuala ya kujiuliza;
Mosi; kama mwanamke hajazaa na umri umeenda na ana mpango wa kuzaa afanyeje?
Iweje mwanamke ambaye aliweza kujizuia kuzaa nje ya utaratibu (japo alikuwa akishiriki), pia hakutumia njia hatarishi kuzuia ujauzito, leo hii asipate mimba?
Iweje mwanamke ambaye ujana wake allishiriki ngono na ndani yake akapata mimba na kutoa, huyu hata akifika miaka 37 anazaa? Ni kwa kuwa mfumo wake ulishajaribiwa, na unaendelea kusubiria uzazi
Kiimani kwa nini huyu aliyejisitiri aje kukosa uzazi? Na akiupata basi iwe kwa mbinde?
Itafika wakati mabinti wengi sana watabeba mimba ili tu kutunza kizazi, ili ikifika wakati sahihi waje kupata watoto bila shida.
Itafika wakati mwanamke ambaye hajaolewa na ana mtoto, na umri umesogea, huyu atapata wa kuwa nae.
Itafika wakati mabinti watabeba mimba kwa lengo la kufanya abortion ili kulinda afya ya kizazi.
Mwisho ningependa kupitia uzi huu tupate wataalam ambao wana ushauri chanya kwa mazingira yaliyoainishwa hapo juu. Nini kifanyike ambacho kitalinda afya ya kizazi (cha mwanamke) ambaye umri umeenda na hajabahatika kumpata mwenza, na ambaye hapendi kuzaa nje ya utaratibu?