UZUSHI Kula pilipili wakati wa Ujauzito kunafanya mtoto kuzaliwa na macho mekundu

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Habari JamiiCheck,

Mimi ni mjamzito, nimekuwa nasikia kuwa ulaji wa pilipili wakati wa Ujauzito kunafanya mtoto kuzaliwa na macho mekundu.

Nisaidieni kuhakiki hii maana napenda sana kula pilipili lakini naogopa mwanangu kuzaliwa na macho mekundu.

types-of-hot-peppers-644144dbbd304.jpg
 
Tunachokijua
Bila shaka umewahi kusikia kuhusu uvumi huu unaofafanua kuwa mwanamke mjamzito akila pilipili atajifungua mtoto mwenye macho mekundu. Kama ulikuwa haujasikia, leo utapata fursa ya kuelewa dhana hii kiundani.

Kwa mujibu wa madai haya, mjamzito akila pilipili huingia moja kwa moja kwenye mzunguko wa damu kisha kupita kondo la uzazi hivyo kuleta athari hasi kwa mtoto ikiwemo kuzaliwa na macho mekundu.

Ukweli wake upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai haya hayana ukweli.

Ulaji wa pilipili huwa hauna athari kwa mtoto na hauwezi kusababisha azaliwe akiwa na macho mekundu hivyo mjamzito anaweza kuitumia kama kawaida.

Hata hivyo, kutokana na uwepo wa mabadiliko makubwa ya homoni za mwili, ulaji wa pilipili unaweza kusababisha kiungulia kikali, tatizo ambalo husumbua wajawazito wengi.

Kwa baadhi ya wanawake husababisha kichefuchefu pamoja na kujaa kwa gesi tumboni. Hizi zote siyo dalili za hatari kwa ujauzito.

Faida za Pilipili kwa Mjamzito
Tafiti za afya zinabainisha kuwa maji ya mfuko wa uzazi (Amniotic fluid) yanaweza kuwa na ladha ya baadhi ya vyakula anavyotumia mama na watoto wanaweza kuzoea ladha hizi tangu wakiwa tumboni hivyo kuwajengea mazingira mazuri ya kutokuwa na mzio (Allergy) wa vyakula.

Faida nyingine ni kuboresha mfumo wa kinga za mwili. Mathalani, capsaicin , kemikali inayoipa pilipili ladha yake ya ukali huwa na faida ya kupunguza uvimbe joto (Inflammation) mwilini.

Pia, pilipili huhusishwa na tafiti kuwa na uwezo wa kupunguza lehemu mbaya mwilini hivyo kupunguza pia nafasi ya kupatwa na kiharusi na magonjwa ya moyo.

Ushauri
Mjamzito anaweza kutumia pilipili kama livyo vyakula vingine. Hata hivyo, matumizi yake yataambatana na dalili mbaya anapaswa kusitisha na kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Kwa upande wangu sidhani kama hii kauli ina ukweli wowote labda wataalamu watusaidie and naomba kuongezea hapo na kama mjamzito anapenda kunywa pombe mtoto atatoka bila akili???
Naombeni msaada
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom