Kuku wa kienyeji akikudonoa hutoa sumu

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,199
1,226
Wakuu hebu tuchangie hii dhana ya baadhi ya watu ambao husema na kuamini ya kuwa ati kuku wa kienyeji ana sumu hasa akikudonoa na kuweka jeraha basi lazima utakufa kama hujatibiwa kwa maana ya kudhibiti sumu......je wadau kuna ukweli juu ya jambo hili? naomba tuchangie wadau.....
 
usemalo ni kweli kabisa lakini mpaka huyo kuku awe ktk hali ya kutofahamu, namaanisha kuwa ikimjia akilini kuwa huyu ni binadamu basi ile sumu inaisha makali na hiki kitendo kinafanyika ndani ya sehemu ya sekunde.
 
Mkuu Isuto naomba unijuze ni mambo ya kufikirika tu? au ni kweli na kama ni kweli hiyo sumu hukaa sehemu gani ya mwili wa kuku? mbona haiingii akilini..
 
usemalo ni kweli kabisa lakini mpaka huyo kuku awe ktk hali ya kutofahamu, namaanisha kuwa ikimjia akilini kuwa huyu ni binadamu basi ile sumu inaisha makali na hiki kitendo kinafanyika ndani ya sehemu ya sekunde.
Tena wanadai ukimnyemelea usiku ukaupeleka mkono wako ndio hatari zaidi (hasa akikufananisha na nyoka)
 
duu, basi km ni hivyo hyo sio sumu. sumu inayoua akihisi ww ni nyoka na haikuui akihisi ww ni binadamu sio sumu.

Hata mimi nimejikuta nacheka sumu gani hiyo inayofanya kazi kwa kutofautisha hahaha hizi ni propaganda tu hakuna lolote
 
Nikifikiria jambo hili huwa nacheka sana...watu wanaacha kutumia akili zao wao wanatunia na kuamini kila wanaloambiwa......kuku tangu lini akawa na Sumu.....
 
Kuku wa Kienyeji siku hizi linatumika kivingine.......lakini nao wana sumu kali sana
 
Hii ishu ni kweli. Ni kwamba Mungu amewaumba viumbe kila kimoja na namna yake ya kujilinda. Kuku hususan usiku anapokuwa amelala. hu kusanya aina flan ya sumu kwenye domo lake (donoleo) kinapotokea kitu cha kutishia usalama wake kama nyoka akimng'ata sumu ile hutoka na kumdhuru mnyama yule. Na hata mwanadamu iwapo kuku atakung'ata kwa lengo la kukudhuru akiwa amehisi wewe ni hatari basi sumu itakupata na kukudhuru, lakini akikung'ata kikawaida kwa lengo la lukufukuza sumu haitoki.
 
Kuku ana sumu mbaya, na adui yake mkubwa ni nyoka. Hata nyoka akiingia bandani huwa havamii kuku haraka bali ni timing maana wao wajuana vema. Kuku hujihami kwa kumng'ata na kuachia sumu yake ambayo huua nyoka au yeye afanyiwe timing na kuuawa. msipuuze, hii ni kweli.
 
inamaana ukimla kuku mzima utakuwa umekula na hiyo sumu yake, au sumu ya kuku inakaa wapiu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom