Kitu gani kilikushangaza mara baada ya kuingia kwenye ndoa?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,150
32,958
Habari za muda huu wanajamii,

Wahenga wanasema usilolijua ni usiku wa giza, kila mmoja wetu anapotarajia kupata jambo jipya au kuingia kwenye maisha mapya hujawa na shauku na mshawasha.

Ndoa ni taasisi ambayo kabla hujaingia unakuwa na matarajio makubwa yaliyojaa furaha kutokana na jinsi unavyompenda mwenza wako lakini wakati mwingine mambo huwa tofauti na vile ulivyofikiria yanaweza kuwa hasi au chanya.

Je ulipatwa na mshangao gani mkubwa baada ya kuingia kwenye ndoa?

Unaweza uka share na kuwa funzo kwa wengine ambao ni watarajiwa.
 
Back
Top Bottom