Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,988
- 960
KITETO: Kata ya Engusero Yapokea Ambulance 🚑 Mpya ya Kubeba Wagonjwa, Wananchi Wamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan
Wananchi wa Kata ya Engusero Jimbo la Kiteto wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Gari jipya la wagonjwa ambalo litawaondolea adha ya Usafiri wa wagonjwa katika Kata hiyo na Tarafa nzima ya Matui.
Pia, Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Gari jipya la wagonjwa ambalo litawasaidia Wananchi wa Kata ya Engusero na maeneo ya jirani na kwa miradi mingine mingi ambayo Kiteto imepata kwa kipindi kifupi
Mhe. Edward Ole Lekaita ametumia hadhara hiyo kuhutubia Mamia ya Wananchi wa Kata ya Engusero waliojitokeza kumpokea na kupokea Ambulance 🚑 mpya ambapo amewataka kulitunza gari hilo ili liweze kusaidia Tarafa nzima ya Matui
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.41.33.jpeg129.5 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.41.33(1).jpeg141.6 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.41.34.jpeg138.7 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.41.34(1).jpeg129.5 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.45.35.jpeg134.3 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.45.36.jpeg145.9 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-05-04 at 23.45.38.jpeg116.3 KB · Views: 1