Kitendo cha kutaka kuhamisha familia 400 zinazozunguka eneo la kimondo cha Ndolezi Mbozi bila fidia ni cha kishenzi

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
2,238
3,917
Wananchi wa kijiji cha Ndolezi kilipo kimondo maarufu cha Mbozi wamekuwa wakiishi hapo kabla ya wanasayansi kuthibitisha kuwa jiwe lile ni kimondo, hivyo kulipa jiwe hilo hadhi ya pekee kulinganisha na mawe mengine yaliyopo kijijini hapo.

Baada ya uthibitisho huo wanasayansi, watalii, na watu wengine wadadisi kwa mamia wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Hapo awali ilikuwa kutembelea eneo hilo ilikuwa bure kabisa lakini baadaye serikali ikaweka ada ya kuliangalia jiwe hilo. Jambo hilo halikuwa baya kwani kijiji na serikali vilipata fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Tofauti na awali ambapo wanakijiji walifurahia kupokea wageni na kunufaika kiuchumi sasa jiwe lile (kimondo) limezua balaa. Wananchi wanatakiwa kuondoka eneo hilo ili serikali ijenge wigo kwa ajili ya wanyama wa porini (Zoo) ili kuongeza vivutio kwa watu wengi zaidi kutembelea eneo hilo.

Kitendo hicho hakikubalika kabisa na hasa kuwaondoa wananchi bila stahiki na fidia za mali zao. Kwa nini serikali hii inayojinasibu kuheshimu haki za binadamu inataka kuwafanyia dhuluma wananchi wake kwa sababu ya wanyama wa porini? Kwani hakuna vivutio vingine nchi hii zaidi ya wanyama? Kwa nini serikali hii inapenda kuanzisha migogoro isiyo ya msingi na wananchi wake?

Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa serikali hii haina watu wabunifu, wamekaririshwa kuwa wanyama pekee ndiyo kivutio cha utalii. Hivi haiwezekani serikali kujenga nyumba ya makumbusho (Museum) ambayo kwanza itachukua eneo dogo lakini pia itahifadhi vitu vya kale na vya utamaduni wa jamii ya watu wa mkoa wa Songwe. Pili itawawezesha wananchi wanaoishi eneo hilo kuendelea kukaa kwa amani na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Wakati umefika kwa serikali kujisafisha kwa kuondoa watumishi wanaokosa ubunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuajiri wanaoweza kubuni miradi ambayo itawanufaisha wananchi na serikali kupata kipato bila kuathiri maisha ya watu na mazingira yaliyopo!
 
Labda ajitokeze muarabu hapo ndiyo mtahamishwa kwa fidia lukuki kama wale wamasai wa Ngorongoro.
 
Hii inanikumbusha stori ya ng'ombe, panya na mtego wa panya. Panya alipolalamika kwa ng'ombe kuwa mwenye nyumba kaleta mtego wa panya tuutoe ng'ombe akajifanya havimuhusu ila mtoto wa mwenye nyumba alipoumwa na nyoka aliyenasa kwenye huo mtego ng'ombe akatakiwa kuchinjwa siku ya msiba.

Wakati wananchi wa loliondo wanalalamika kuhamishwa kimabavu watu wa maeneo mengi tuliona hayatuhusu tuwaachie wenyewe, sasa yanapotufika na sisi kwetu tunatafuta sympathy ya nchi nzima.

Hizi makitu hazitaisha hadi wananchi wote bila kujali tuko wapi tusimame tuseme NO!
 
Wananchi wa kijiji cha Ndolezi kilipo kimondo maarufu cha Mbozi wamekuwa wakiishi hapo kabla ya wanasayansi kuthibitisha kuwa jiwe lile ni kimondo, hivyo kulipa jiwe hilo hadhi ya pekee kulinganisha na mawe mengine yaliyopo kijijini hapo.

Baada ya uthibitisho huo wanasayansi, watalii, na watu wengine wadadisi kwa mamia wamekuwa wakitembelea eneo hilo. Hapo awali ilikuwa kutembelea eneo hilo ilikuwa bure kabisa lakini baadaye serikali ikaweka ada ya kuliangalia jiwe hilo. Jambo hilo halikuwa baya kwani kijiji na serikali vilipata fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Tofauti na awali ambapo wanakijiji walifurahia kupokea wageni na kunufaika kiuchumi sasa jiwe lile (kimondo) limezua balaa. Wananchi wanatakiwa kuondoka eneo hilo ili serikali ijenge wigo kwa ajili ya wanyama wa porini (Zoo) ili kuongeza vivutio kwa watu wengi zaidi kutembelea eneo hilo.

Kitendo hicho hakikubalika kabisa na hasa kuwaondoa wananchi bila stahiki na fidia za mali zao. Kwa nini serikali hii inayojinasibu kuheshimu haki za binadamu inataka kuwafanyia dhuluma wananchi wake kwa sababu ya wanyama wa porini? Kwani hakuna vivutio vingine nchi hii zaidi ya wanyama? Kwa nini serikali hii inapenda kuanzisha migogoro isiyo ya msingi na wananchi wake?

Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa serikali hii haina watu wabunifu, wamekaririshwa kuwa wanyama pekee ndiyo kivutio cha utalii. Hivi haiwezekani serikali kujenga nyumba ya makumbusho (Museum) ambayo kwanza itachukua eneo dogo lakini pia itahifadhi vitu vya kale na vya utamaduni wa jamii ya watu wa mkoa wa Songwe. Pili itawawezesha wananchi wanaoishi eneo hilo kuendelea kukaa kwa amani na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Wakati umefika kwa serikali kujisafisha kwa kuondoa watumishi wanaokosa ubunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuajiri wanaoweza kubuni miradi ambayo itawanufaisha wananchi na serikali kupata kipato bila kuathiri maisha ya watu na mazingira yaliyopo!
Labda wameambiwa kuna kingine kinakuja
 
Back
Top Bottom