Kinachoendelea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

kyalankota

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
2,585
1,442
Ndugu wanajukwaa, natumaini mnaendelea vizuri katika harakati za hapa na pale za kujikwamua kiuchumi.
Bila kuwachosha niende moja kwa moja kwenye hoja husika:

Siku za nyuma hivi karibuni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza nafasi ya kazi ya muda mfupi kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa waandishi wasaidizi na waendeshaji wa BVR ambapo tarehe ya mwisho ya kutumia maombi ilikuwa tarehe 27/04/2024.

Baada ya hapo kumekuwa na maswali mengi watu wakiulizana kwenye mitandao ya kijamii na maswali hayo ambayo watu wamekuwa wakijiuliza yamelenga zaidi juu ya:

1. Lini majibu ama orodha ya waliochaguliwa itatoka?
2. Lini usaili / interview itafanyika?
3. Lini semina itaanza na itafanyika kwa muda gani?
4. Lini kazi yenyewe itaanza na itachukua muda gani?
5. Taarifa juu ya yote hayo yanayojiri yatapatikana kwa njia gani?

Kwa mimi binafsi nadhani kwa mlioomba hizo nafasi muwe watulivu na kwa namna mlivyopokea hayo matangazo ya kazi ndivyo mtakavyojuzwa msije mkapotoshana. Vyanzo vya kuaminika kuna Tovuti ya tume husika, ofisi za kata, vijiji/ mitaa, mkurugenzi e.t.c.

N.B kwa yule atakayekuwa wa kwanza kupata taarifa yoyote sahihi na chanzo sahihi ajulishe wenzake kupitia Uzi huu ama kama una namba zake za simu mjulishe ili asije akapitwa na fursa.

Asanteni na karibuni.
 
Zoezi mwezi wa sita Kaa mko wa kula
Hilo wengi wanalifahamu maana kikawaida mara nyingi zoezi linafanyika kwenye madarasa na linahusisha walimu kwa asilimia kubwa, hivyo inabidi shule ziwe zimefungwa yaani likizo. So obviously ni June ila tarehe ndo bado, itajulikana hapo baadaye ndo maana nimehitimisha kuwa wawe watulivu wasubiri taarifa sahihi.
 
Watendaji kata na wenyeviti wa Vijiji wameketi Leo kujadili majina ya waombaji, kigezo kikubwa ni kuwa wanachama wa CCM ndio wanaopewa kipaumbele zaidi, kama siyo mwanachama basi omba Sana Mungu kuweza kuvuka hicho kinyang'anyiro
Una uhakika?
 
Back
Top Bottom