Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,790
66,975
Katibu mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5.

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana CCM hao?

---
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la ya Covid-19, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.

"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan "

"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali."

"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza"

"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja"

"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu"

Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
 
Back
Top Bottom