1979Magufuli
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 453
- 1,800
Huwa navutiwa sana ninaposikia Kibatala anamtetea mtu, nimeanza kukufuatilia kitambo sana uwezo wako kisheria na kweli umenifanya hata mimi nipende kusomea sheria, Wakili msomi Kibatala, mimi nimeshuhudia mawakili wengi wasomi kuliko wewe, mfano marehemu Dkt.Masumbuko Lamwai, Herbet Nyange, Mosses Maira, Mabere Nyaucho Marando, Professa Abdallah Safari nk.
Nilikuwa nashinda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwasikiliza mabingwa hao tu wakiwakilisha watu mahakamani, miongoni mwa mawakili waliobaki ni huyu msomi Majura Magafu.Huyu ni bingwa kuliko wewe Kibatala.
Kwanza kwenye roll of advocates nadhani Magafu ni senior kwako, lakini hata hivyo nimekuwa nikikuona sana Kibatala ukiongea kwa kebehi sana dhidi ya serikali.Kwa mfano leo katika kesi ya Boniface na Malisa unasoma hati ya mashtaka mbele ya waandishi wa habari kwa majivuno ukisema unawasubiri hao waliokuwa wakifanya press yaani Jeshi la Polisi na utaomba waitwe mahakamani ili uweze kuwahoji.
Ukaongea kwa kebehi eti nanukuu, " Tutaomba pia hao ambao mwanafamilia amesema ni jeshi waje pia kutoa ushahidi." mwisho wa kunukuu.
Maneno hayo ni ya dharau, kebehi na majivuno, huko serikalini kuna wanasheria wasomi kuliko wewe, kwanza unavyojifanya mjuaji naona kama unawatafutia balaa hao washtakiwa wawili, kesi ni ushahidi na ushahidi kuwa washtakiwa wametenda kosa ushahidi dhidi yao utathibitishwa mahakamani na hao unaowapa matumaini utawasababishia matatizo.
Wewe kujua sheria haina maana kuwa Jacob na Malisa hawawezi kuwa behind the bars, nakusihi sana Bro, navutiwa sana sana sana na uwezo na kipaji ulichonacho kisheria lakini sio sawa kuwa mjivuni, kudharau mamlaka kwa sababu tu una itikadi za Chadema.
Sasa Jamhuri itakupangia mawakili wa saizi yako na huyo Jacob atakonda mwenyewe baada ya mwezi.