Nimekuwa nikifuatilia wananchi wa Mkoa wa Arusha wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Makonda. Kwa asilimia kubwa lazima sheria zifuatwe na Mkuu wa Mkoa hayuko juu ya sheria. Inawezekana kero nyingi zilizotolewa tayari aidha ziko Mahakamani au uamuzi wa kisheria ulikwishapitiwa.
Mimi naona wananchi wengi wanapoteza muda wao na hawatasaidiwa chochote na Mkuu wa Mkoa ni vema wakafuata taratibu za kisheria. Hata yule Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha alioagiza ahamishwe, mimi naona siyo utawala bora kusema mbele ya watu kuwa ahamishwe.
Usitafute popularity ambayo haisaidii. Najua wananchi wana kero nyingi na wanaonewa lakini ni hakuna budi sheria zifuatwe kutatua kero hizo.