KERO Kero kubwa ya Umeme mkoa wa Mtwara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Shida ya umeme ilipofikia sasa mkoa wa mtwara si pazuri, leo ni siku ya nne umeme hauwaki mchana unawaka usiku tu, tena hiyo usiku unaweza kusema labda kaachiwa mtoto achezee kidogo umewaka kidogo umekata ili mradi kero tu.

Tulitangaziwa kuwa umeletwa mtambo wa megawati 20 kumaliza tatizo mpaka March 30 tatizo lingeisha, kumbe wameenda kuchukua mtambo mbovu wa Ubungo wakatuletea sisi tusumbuane nao yaani wanatuchukuliaje?

Tunamuomba Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Doto Biteko kama serikali imeshindwa kutuletea mtambo mpya (maana nasikia kuna mitano imezimwa huko) basi watutafutie mwekezaji wa kuja wekeza huku, ili awauzie umeme TANESCO na wala sio jambo la aibu kutafuta mwekezaji ukishindwa kuendesha jambo mwenyewe bali ndiyo busara, kwasababu wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini wauza mabucha ya samaki, wauza juisi, waranda mbao, wachomea vyuma, wenye saloon waoka mikate n.k sasa hao na mfano wao unawakatia umeme siku nne ili waishi vipi?

Gesi tunayo imejaa kuliko maji, kwanini tuteseke na umeme watu wa Mtwara?

Kama tulivyompa mwekezaji bandari na mwendokasi basi tumpe na huu mradi wa umeme wa gesi mtwara wananchi wafanye mambo ya maendeleo tujenge nchi yetu.
 
Back
Top Bottom