Kauli ya 'Kata simu kwanza kuna mtu ananipigia' huwa unaichukuliaje?

Ivi hii kauli na agizo uwa unalichukuliaje na uwa unajisikiaje!? unapoongea na mtu kwenye simu Kisha anakupa ilo agizo

Hiyo humtokea MTU yeyote kutokana na level yake.

Mwanzo nilikuwa naiona Kama dharau Ila kuna siku nilikata simu ya mh Mbunge ili niongee na boss mmoja hivi.

So katika MAISHA yangu huwa sichukulii mambo personal

Hata rais wa nchi anaweza kukatiwa simu
 
Ukiona hivyo wewe hauko kwenye list yake ya watu muhimu

Usijisikie vibaya tafuta hela

Zamani nilikuwa nasema watu wakipata pesa huwa wanabadilisha marafiki

Nikaja kugundua kumbe ukipata pesa na marafiki wanabadilika automatically pasipo wewe kutaka ..

Unakuwa una marafiki wapya..
 
Usichukulie mambo personal sisi waswahili bado mambo mengi hatuyajui unabidi kuchukulia kawaida
Kuna kitu kinaitwa polite speaking, sijui kwa kiswahili nisemeje. Watanzania wengi sana hatuna huu utamaduni. Hili la simu ni moja kati ya mengi.

Ukiwa ofisini majuu utafurahi mwenyewe jinsi watu wanavyoweza kuelekezana mambo ambayo yangeweza kufanya mtu anayeelekezwa ajisikie vibaya lakini lugha inayotumika inaondoa ukakasi wote.
 
Kwa mwenye inferiority complex anaona kadharaulika, ila kwangu hapana. Ukiniambia hivyo nakuelewa sana tu kutegemea na jambo. Mf, napiga na wewe soga tu pengine muda wa kazi bosi amepiga inakuwaje hapo? Au imagine nipo mahali namsubiri mtu anifikie, kapiga wakati napiga soga na wewe, asubiri mpaka tumalize soga au nimpokelee? Wabongo ni watu wa kujishtukia sana
 
Ukiona hivyo ujue mlikuwa mnaongea ujinga kwahiyo Kuna mtu anataka kuongea naye issue serious Kisha akimaliza atakupigia muendelee mlipoishia na ujinga wenu
Upo sahihi kabisa, huyu ni mimi na shost zangu tukishamaliza ya maana tunaingia kwenye umbea simu ya kazi au familia inaingia lazima nimwambie kata/subiri kwanza nimpokelee fulani, kisha tunaendeleza umbea wetu.
 
Back
Top Bottom