Kasi ya kobe kwenye intaneti ya Tigo

Stavros Myles

JF-Expert Member
Jun 7, 2020
350
390
Nisikuchoshe kukupa salamu nyingi mno, ninataka kuzungumzia suala la Mtandao wa Tigo nchini Tanzania kushindwa kuhimili mahitaji ya Internet kwa wateja wao.

Si kwamba wanashindwa kutoa vifurushi vya Internet, shida kubwa ni kwamba mtandao wao hausomi kabisa na hata ukifanya kazi speed ya Internet haipandi juu ya Kb 10. Shida ni nini?

Au labda kwa Upande wa Mbeya tumetupwa na kuonwa tuko wachache? Je, kampuni ya Tigo inajua ni kwa kiasi gani hii service mbovu inafukuza wateja wake?

My take: Tigo kwa jiji la Mbeya wajitafakari katika suala la Internet, huu ujanjaujanja utawagharimu mno kwa kupoteza wateja.

PS: Nalalamika kwakuwa nimenunua bando. Nitahamia Mitandao mingine. Hii Ofa yao ya 1.5k inakutia wazimu alafu unakumbwa na sonona mbeleni.


UPDATES.

Baada ya muda saizi nimepokea meseji kutoka Tigo, meseji hiyo imekuja na ujumbe wakunitumia settings za Internet. Kuna mitandao mingine kila ukikaa unashangaa uliingiaje
 
Hata dar tigo wako hovyo sana, shida ya voda nao wanakula bando kama mchwa sijui tukimbilie wapi
 
hamia voda hata kifurushi cha 1500 gb 1 kipo.

halotel kipo kwenye ofa yangu
 
Nilijua HUAWEI MATE 40 pro yangu imeanza kuharibika nashauri tuelekee HALOTEL angalau kidogo 4G inatupunguzia hasira
 
Aisee! ndo nlikua najiuliza hapa leo imezidi jamani kha!
 
Mm nalipa 15000 napata 7gb na dakika900all net, kila tarehe moja huwa napewa bill nalipa ndani ya siku kumi so nishasahau kukwangua vocha
 
Numbisa ,kwa siku ya leo mvua haijanyesha .Hali ya hewa ilikuwa inaruhusu mwanga wa Jua kutufikia vizuri kabisa.

Labda wataalamu wa Masuala ya Telecommunication System wanaweza kuwa na sababu za kuelezea kama suala hili lina maelezo yakitaalamu.

Region F1 na F2 nadhani zilijigawanya vizuri wakati wa mchana.
 
Gamba la Mbu, basi Tigo kuna mahali wana "fail". Hili tatizo likiwa kubwa wanajiweka kwenye position mbaya kibiashara na kiushindani. Itafika wakati Sim Card ya Tigo itakiwa ni kwa ajili ya kupendezeshea kabati la Vitabu tena kwenye shelfu za chini kabisa
 
Back
Top Bottom