let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 3,346
- 7,977
Papa hakusema ushoga wao ubarikiwe, bali mashoga wabarikiwe.Andiko gani linasema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe kanisani?
Nakubali hakuna mwenye dhambi anapaswa kufungiwa mlango, na natambua Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi.
1.Lakini kuna tofauti hapo, Yesu alimfata Zakayo mtoza ushuru (alikuwa mwenye dhambi maana aliwadhurumu watu mali zao), akampa injili hatimae Zakayo akaacha dhambi (akaacha kudhurumu na akarudisha mali za aliowadhurumu mara 4 zaidi)
2.Yesu alipoletewa mwanamke aliefumaniwa akifanya uzinzi (dhambi), alimsamehe na kumwagiza asitende dhambi tena.
Swali langu kwako, Papa aliposema wapenzi wa jinsia moja wabarikiwe je kuwabariki kungewafanya waache dhambi zao (kufanya mapenzi ya jinsia moja) au wakibarikiwa maana yake aendelee kufanya dhambi (kuendeleza mapenzi ya jinsia moja)?
Kama walipata uongozi wa Mungu kubariki wapenzi wa jinsia moja
1. Kwanini watu wa sodoma na gomora walichomwa?
2. Kwa nini kauli imebadilika sasa, je Mungu amegundua alikosea kuruhusu jambo alilolikataza mwenyewe?
Kuna ushoga hapo na mashoga.
Ushoga wao kanisa haliukubali, ila linapinga kuwatenga mashoga.