Kanisa Katoliki latoa waraka mpya unaiotwa 'Dignitas Infinita' likipinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,669
4,921
Siku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba.

Katika waraka huo wenye Point 66, umevavaduliwa kama ifuatavyo

USHOGA NA KUBADILI JINSIA
Point ya 60 katika Waraka huu inapinga hali ya ushoga au kubadili jinsi. Kanisa likisisitiza mtu kuheshimu jinsi alivyoumbwa tangu anazaliwa, hivyo kuheshimu mpangilio wa asili wa mwili wa binadamu tangu anazaliwa. Kanisa linapinga kitendo chochote cha ubadilishaji jinsia kinyume na asili ya mwanadamu ukiachilia mbali wale waliozaliwa wakiwa na shida ya maumbile ambapo Daktari atathibitisha hilo.

KUTOA MIMBA
Point ya 47 inasisitiza kanisa linakataa utoaji mimba, na kwamba ni kinyume cha mapenzi ya MUNGU, na kwa sababu mtoto yeye hana makosa na hawezi kujitetea. Utoaji mimba ni kosa katika miiko ya kanisa

KUPANDIKIZA MIMBA (SURROGACY)
Point ya 48, 49, na 50 Kanisa linakemea kitendo cha kubeba mwanamke kubeba mimba kwa niaba ya mwanamke mwingine au kupandikiza mimba, likisisitiza Mtoto anatakiwa kubebwa katika mfuko wa uzazi wa mama yake na si mtu mwingine.

VITA
Point ya 38 na 39 kanisa linahimiza kuepuka vita, na kupinga vikali vitendo vyote vinavyochochea vita au ubaguzi kwa namna yeyote.

WAHAMIAJI HARAMU (IMMIGRANTS)
Point ya 40 kanisa linasisitiza wahamiaji haramu wasitengwe au kufanyiwa uvunjifu wa utu wao, Kanisa linataka wahamiaji haramu watendewe mema kama watu wengine kwa sababu hawakutaka kuwa katika hali hiyo, hivyo jamii ziwapokee, ziwasaidie na si kuwabagua.

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU (HUMAN TRAFFICKING)
Point ya 41 na 42 kanisa linasema litaendelea kupambana na vitendo vya kusafirisha binadamu kwa ajili ya kuuza viungo vyao vya mwili, kwa ajili ya kazi za kitumwa, kwa ajili ta kazi za umalaya, kwa ajili ya kuwatumikisha kingono mabinti na vijana wadogo, kwa ajili ya vitendo vya kigaidi na kazi zote za namna hiyo.

UKATILI WA KIJINSIA
Point ya 43 kanisa linapinga ukatili wa aina yoyote wa kijinsia

UKATILI WA WANAWAKE
Point ya 44, 45 na 46 Kanisa linapinga ukatili wa wanawake ikiwemo rushwa ya ngono, kitendo cha kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe kuwafurahisha wanaume, vipigo, kuwashurutisha kutoa mimba, bila kusahau kuwafanyia ndoa za mitaala (wake wengi), vitendo hivyo vyote vinapingwa na kanisa

KUSITISHA MAISHA YA MGONJWA, AU KUSAIDIA MTU KUJITOA UHAI
Point ya 51 na 52 kanisa linakataza kitendo cha kukatisha maisha ya mgonjwa kwa namna yoyote au kumsaidia mtu kujitoa uhai. Kanisa linaimiza hata kama mtu ni mahututi kiasi gani au hawezi kupona basi ni vyema tumfariji mpaka pale umauti wake utakapomfika na si kutoa uhai wake kwa namna yoyote hata kama ni kwa ridhaa yake.

UBAGUZI WA WALEMAVU
Point ya 53 na 54 Kanisa linapinga vitendo vya ubaguzi na kuwatenga walemavu.

VURUGU MITANDAONI YA KIDIGITALI
Point ya 61 na 62 kanisa linakumbusha kutumia mitandao katika njia nzuri, na sio kutumia kuumiza wengine. Kanisa linasema kazi ya Teknolojia ya kidigitali ni kumsaidia binadamu na si kumdhuru.

SOMA WARAKA WOTE HAPA CHINI: Declaration of the Dicastery for the Doctrine of the Faith “Dignitas Infinita” on Human Dignity
 
Siku ya leo Kanisa Katoliki kupitia idara ya habari ya Vatican limetoa waraka mpya unaoitwa "Dignitas Infinita" Miongoni mwa mambo yanayozungumziwa kwenye waraka huo Uliosainiwa na Papa ni pamoja na Msimamo wa Kanisa katoliki katika Kupinga Utoaji Mimba, Kubadilisha Jinsia na Upandikizaji wa Mimba...
1 .Chanzo cha taarifa yako ni media ipi? 2.Muda utakwambia uchafu wote wa vatican..........narudia tena it's just a matter of time. Hivi kwanini maraisi kibao lazma waende vatican? including Watanzania?

Tena wanaenda officially? kuna nini huko vatikani ......vijundi vyote vya kishetani vimeasisiwa vatican i.e JESUITS ILUMINANT FREEMASONS etc.

NB hayo yote uliyoyataja yanapigiwa chapuo na vatikan n swala la muda tuu ...sema wakatoliki wengi sanamu zimewalumbaza ata hamuwezi kung'amua lipi ni lip.

Allah akbar

Screenshot_20240408-220846_Biblia.jpg
 
Asante mleta mada kwa ufafanuzi wa waraka wa kanisa kwa wakati huu ambao kumekuwepo na mkanganyiko mingi kuhusu msimamo w kanisa kwenye baadhi ya mambo yenye influence kubwa kwa jamii yetu kwa sasa.

Bado kanisa linasimama na utu na ubinadamu na asili ya ulimwengu na Umungu.
Hata kama yapo ya hapa na pale ila kanisa lina tuweka kwenye mstari myoofu wa uadilifu.

Ibaki tu makasisi na watawa kuwa na ndoa ama wenzi. Hio ni changamoto ambayo kanisa inabidi iombe msaada wa Mungu kwa hili.
 
Asante mleta mada kwa ufafanuzi wa waraka wa kanisa kwa wakati huu ambao kumekuwepo na mkanganyiko mingi kuhusu msimamo w kanisa kwenye baadhi ya mambo yenye influence kubwa kwa jamii yetu kwa sasa...
Kama wanatakiwa kuomba msaada wa Mungu kwa swala la makasisi na watawa kuwa na ndoa. Je kauli ya kubariki wapenzi wa jinsia moja walishindwa kumuomba Mungu awaongoze kabla ya kutamka hadharani?
 
Kama wanatakiwa kuomba msaada wa Mungu kwa swala la makasisi na watawa kuwa na ndoa. Je kauli ya kubariki wapenzi wa jinsia moja walishindwa kumuomba Mungu awaongoze kabla ya kutamka hadharani?
Ile statement ipo biblical kaka, hakuna mwenye dhambi hata mmoja anaye paswa kufungiwa mlango na kanisa, kilichomleta Yesu duniani sio kwa yoyote aliye mwema ila kwa wote walio na dhambi ambao dhamiri zao zinawadai kufanya toba na marejeo kw Mungu muumba wao.

Alilaumiwa sana Yesu na ikawa sababu moja wapo ya kushtakiwa nayo kuwa karibu na wenye dhambi, ambao ndio ulikuwa uyumishi wake ambao pia aliwaagiza wafuasi wake wauneze mpaka zama zetu kwamba Kristo si kwa wema ila wenye kuhitaji toba.

Papa alipotoa kauli ile dunia na wenye mitazamo hasi wameitafsiri vinginevyo na kuja na mahitimisho tuliyo nayo sasa!

Hakuna shaka papa na uongozi wa vatikani ulipata msaada na mwongozo wa ki Mungu kabla ya kutoa kauli ile.
 
Asante mleta mada kwa ufafanuzi wa waraka wa kanisa kwa wakati huu ambao kumekuwepo na mkanganyiko mingi kuhusu msimamo w kanisa kwenye baadhi ya mambo yenye influence kubwa kwa jamii yetu kwa sasa.

Bado kanisa linasimama na utu na ubinadamu na asili ya ulimwengu na Umungu.
Hata kama yapo ya hapa na pale ila kanisa lina tuweka kwenye mstari myoofu wa uadilifu.

Ibaki tu makasisi na watawa kuwa na ndoa ama wenzi. Hio ni changamoto ambayo kanisa inabidi iombe msaada wa Mungu kwa hili.
Kwani mapadre na watawa wa kike wanapungukiwa kipi hasa wasipokuwa na wenza wao ?

Mafundisho ya mtume Paulo umesoma ?
 
Back
Top Bottom