Jokate: Fomu ya urais ni moja tu

Na kwa nini iwe fomu moja tu! Kwa akili na mitazamo ya aina hii, haihitaji mtu kuwa na akili nyingi kugundua ya kuwa hata ndani ya hiyo ccm yenyewe hakuna kitu kinachoitwa demokrasia.

CCM ni chama dhulumati. Inaanza kwa kudhulumu haki ya wanachama wake ndani ya ya chama. Ikitoka ndani ya chama, kwa vyovyote itakwenda kudhulumu haki ya vyama vingine kwa kuiba kura zao, kisha inakwenda kudhulumu haki ya umma mzima kwa kuwatangaza viongozi ambao mara nyingi huwa hawajachaguliwa na wananchi, halafu inaenda kuunda Serikali ambayo kwa kiasi kikubwa huwa inadhulumu haki ya umma mzima kwa kuwatoza wananchi koda nyonya damu, na sehemu kubwa ya kodi hizo huishia kwenye ufisadi na anasa za viongozi wake.

Hakika kinachoanza kwa kudhulumu humalizia kwa kudhulumu.
 
Duh,kazi kwenu mnaotaka kugombania

Ova
Hakuna mwenye ubavu wa kupingana na Mwenyekiti ndani ya Ccm kwa sababu Mwenyekiti ndiye pia ni Mkuu wa Nchi na ndiye Mkuu wa Majeshi yote ya Nchi !

Kwa mintarafu hiyo tu mtu mwenye akili timamu atajiuliza huyo anayetaka kumpinga Mwenyekiti ana Akili timamu kweli ???!!
Hao wanaoongea kuhusu fomu moja wanaongea kwa kujipendekeza kwa Mwenyekiti tu ili wafikiriwe zaidi ya kile walichokwisha kupewa !

Ukweli ni kwamba hakuna mwenye ubavu ndani ya Ccm ya kumpinga Mwenyekiti hata wasipoongea akina Mwegelo ! 🙏🙏

Iko vile miaka yote na itabaki hivyo siku zote mpaka hapo itakapobadilishwa sijui na mtu wa kutoka kwenye sayari ya Mars atakapokuja. 😅😅😅🙏🙏🙏 !
 
Kwani tangu lini ilikuwepo ??!
Ikiwa hata mawazo mbadala tu hutakiwi kuyatoa hadharani ! Hiyo itaitwa ni demokrasia ??!

Huyo Jokate ukimuangalia hapo kwenye picha sura yake imeshakuwa ya kikatili ! Ndivyo wanavyotakiwa kuwa hivyo !
Hakuna Demokrasia ipo Domokasia !
Ukiongea tofauti na wanavyotaka kusikia utashughulikiwa !!
Kwani lazima rais atoke ccm?
 
CCM Imepasukia Ndani Humo Humo Ila Naamini Mwakani 2025 Watafukuzana Sana Sana
Wapo Wanaowa~Zoom Hao Form Moja, Wanasubiri Muda Wateme Nyongo U~Rais Unatakiwa Na Wote
Ngoja tuone hii movie 🎥 itaishaje !
Ile gang ya pwani inaonekana bado ina nguvu !
Lakini waswahili wanasemaga Nguvu ya mamba iko kwenye maji !

Eti akiwa nje ya maji anakuwa kama mjusi mkubwa tu 😅😅😂🙏

Ngoja tuone !
 
Hoja sio kuwaachia wengine hoja ni kwamba je huo ndio utaratibu wa chama....??
Utaratibu wa CCM kila awamu ni kwamba the sitting President hupita bila kupingwa Chamani !!

Ni kwanini utaratibu huo ubadilike hivi sasa ??
Au ni kwa sababu ya Jinsia au kwa kuwa ametokea upande wa pili wa Muungano. ???!!
Why NOW ??!!!!! 🙏🙏🙏
 
Aliyefunga matamanio ya membe Benard kwakweli ametuweza sana ,asingekubali ujinga huo kama kweli utakuwepo
 
Utaratibu wa CCM kila awamu ni kwamba the sitting President hupita bila kupingwa Chamani !!

Ni kwanini utaratibu huo ubadilike hivi sasa ??
Au ni kwa sababu ya Jinsia au kwa kuwa ametokea upande wa pili wa Muungano. ???!!
Why NOW ??!!!!! 🙏🙏🙏
Hupita bila kupingwa baada ya kupigiwa kura au kwa kupewa.....??
 
Back
Top Bottom