Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WaTZ wengi hatulipi kodi kwa sababu ya upuuzi wa watumishi wa TRA. Nimeamua kwenda TRA kujisalimisha nilipe kodi, ukifika mtu anataka kumalizia shida zake zote kwako. usipompa kitu kidogo, utajuta kwa nini umekuwa muungwana wa kujipendekeza kulipa kodi

hahaha, nilikwenda pale kusajili tin, nikaambiwa nije na risiti ya malipo ya kodi ya miezi 4 nyuma ambayo sikufanya biashara. You knw what i did, niliamua kuachana nao, nikawasusia na litin lenyewe! Ndo maana wtz tunapat shida kulipa kodi! Ooh!
 
Wadau. Naomba kwa mwenye uzoefu aniambia ni nini na ni kinahitajika ili kusajil jina la kampuni binafsi brela? Na je brela wanachukua muda gani ili kupitisha jina la kampuni? Natanguliza shukurani.
 
huvi angakuuliza anataka kusajiri kampuni je aende wapi? ungejibu nn? au yote yanajibu moja? so bwana mdogo acha pumba jibu swali......ukishindwa kaa kimya. au nenda majukwaa unayoyaweza.
 
Kachukue form brela bei 5000 kisha jaza jina, objectives,na address. Ukirudisha unapewa jina lako uliloomba, nashangaa hawa jamaa hawatoi cheti ambacho kingekuwa uthibitisho wa kusajili
 
andika barua yakuomba jina la kampuni,
ndani yake orodhesha majina yako 3 unayopenda ili 1 lipatikane.
kisha baada ya siku 3 nenda utakutana na mafaili ambapo jina lako litakuwa limeshapitisha tayari kwa kusajiliwa.
maelezo zaidi ni Pm.
 
Wadau. Naomba kwa mwenye uzoefu aniambia ni nini na ni kinahitajika ili kusajil jina la kampuni binafsi brela? Na je brela wanachukua muda gani ili kupitisha jina la kampuni? Natanguliza shukurani.
Kamanda ingia kwenye website ya BRELA, kisha down form kwani BRELA hawatoi form kwa sasa. (ni form namba 3 kama ni sole propriatorship) na (form namba 2 kama ni partnership). Ukishaijaza vizuri irudishe BRELA, Ushirika building Ghorofa ya sita. Wakishaipitia hiyo form na kuapprove utaelekezwa chumba cha kwenda kulipia (accounts) na utapewa risiti (ni ghorofa ya pili). Gharama ni Tsh. 6000 (yaan Tsh. 5000 kama registration fee na Tsh. 1000 kama maintanance fee).

Kama file lako halitakuwa na matatizo (kama kuingiliana kwa jina) basi after three working days unatakiwa upate certificate of registration (kwa mujibu wa customer charter). Hata hivyo experience inaonyesha kuwa hao watu wahaoperate ndani ya huo muda, kwa hiyo jiandae kucheleweshwa zaidi

Kwa urahisi zaidi chukua hii ya kwenye attachment
 

Attachments

  • BRELA forms-Individual.DOC
    33.5 KB · Views: 619
andika barua yakuomba jina la kampuni,
ndani yake orodhesha majina yako 3 unayopenda ili 1 lipatikane.
kisha baada ya siku 3 nenda utakutana na mafaili ambapo jina lako litakuwa limeshapitisha tayari kwa kusajiliwa.
maelezo zaidi ni Pm.
Mchakato wa kuandika barua ya Name search unakuwepo kama mtu anataka kusajili limited company (hii ni kwa Tanzania). Kwa kuwa huyu anasema anataka kusajili jina la biashara (business name), hutakuwa sahihi ukimwambia aandike barua ya name search.

Hivyo suala la msingi ni kujaza form na kuilipia kama nilivyomuelekeza hapo juu. Hiyo search huwa inafanyika on the process (baada ya kusubmit form), na kama ikitokea lile jina alilolijaza limeshatumika basi ataambiwa abadilishe
 
Sole propietaship ni nini?

Partnership ni nini?

Ltd ni nini

Je baada ya kukubaliwa Jina na BRELA, hatua gani inafuata?

MOU and Association of artcles inatakiwa katika hatua gani?

Kuandikisha kampuni ya Utalii (tour Operator) au Travel Agent ni hatua zipi?

Je kuandikisha NGO ni same process ama tofauti?

Great Thinkers karibuni mdadavue majibu, najua wengi mmesoma Economy na Business administration.

--- You can also pm me if you are based in Arusha or Moshi and I can meet you----
 
Wana Jf naomba msaada ni vitu gani (Requirement ktk establishing a companya) itakayodili na kusupply vitu mbalimbali kwa mfano, stationerie, computer accessories. Nisaidiwe hatua ya mwanzo mpaka ya mwisho. Nawasilisha
 
Mkuu, ina kubidi kwanza uamue ni kampuni aina gani unayo taka kuanzisha.
Una weza kufanya biashara hiyo kwa kutumia jina lako binafsi, yaani bila ku-register jina la biashara. Hii utahitajika upate barua kutoka kwa mjumbe wa pale ofisi yako ilipo uipeleke pamoja na kitambulisho chako kwa mtendaji atakaye andika barua ya utambulisho kwa watoa leseni wilayani kwako. Baada ya kupata leseni utaenda ofisi za TRA husika kati ka eneo lako ili kupata TIN certificate. Hapo tayari unaweza kuanza kufanya biashara yako.

Unaweza pia kuanza kwa kusajili jina la biashara (Business name)
Business name una weza kusajili kama sole proprietor (una endesha biashara mwenyewe)
au partnership (ya watu wawili au zaidi). Unaweza pia kusajili Limited Company.
Usajili huu wa business name, partnership au Ltd Company utafanyika kwenye ofisi za BRELA zilizopo jengo la Ushirika, mnazi moja, Dsm. Utaandika barua ya kuomba usajili wa kampuni alafu watakujulisha kama hilo jina limesha sajiliwa tayari. Kama bado watakupa fomu za kujaza ili wakutengenezee vyeti vya usajili. Kwenye partnership na Ltd Company utahitaji usaidizi wa wakili ili kutengeneza Partnership deed au Memorandum and articles of Association ya Limited Company.

Kwenye bajeti ya juzi waziri alisema mtu binafsi ata ruhusiwa kusajili na kuanzisha Limited company hata akiwa mwenyewe. Sijui kama hili limesha pitishwa lakini limited company ilikuwa inahitaji watu wawili na zaidi.

BRELA watakupatia vyeti viwili, certificate of registration itakayo onyesha tarehe, jina na namba ya usajili ya kampuni yako na extract from register itakayo onyesha majina ya wenye kampuni. Watapiga mihuri yao pia kwenye partnership deed au Memorandum and articles of association kutegemea kama kampuni ni partnership au Ltd company.

Kama uliamua kutumia business name kwenye leseni hapo juu basi utaambatanisha certificate of registration na extract from register unapofuatilia kwa mtendaji, wilayani na TRA. Katika kila hatua kuna hela utalipia kwenye ofisi husika (Sina hakika sasa hivi ni kiasi gani- lakini sio hela nyingi), TRA ndio nadhani bado hawalipishi chochote kutoa TIN certificate.

Mkuu, usiogope kwenda ofisi yeyote kwa ajili ya kufuatilia usajili wa biashara yako. Kuna watu ambao wameajiriwa na serekali ili wakusikilize na wakuhudumie wewe. Maendeleo ya nchi hii pia inaanza na watu wenye uamuzi kama wako. Kuwa mjasiri na ujiamini kwa kila jambo na utafanikiwa. Nakutakia vyema.
 
Mkuu Chash, naomba unieleweshe vizuri hapo, kwahiyo unapotaka kufungua kampuni ya General suppliers huna haja ya kwenda BRELA issue yote ya usajili inaishia baada ya kupata Leseni ya biashara halmashauri ya wilaya na kwenda TRA basi?
 
Mkuu,unaweza kufanya biashara kwa jina lako binafsi bila kwenda BRELA kwa kutumia kitambulisho chako kupata leseni na TIN.

Unaweza pia kusajili jina hilo lako kuwa jina la biashara kupitia usajili wa BRELA. Kama unatumia jina lako binafsi sheria inakuruhusu kuto kwenda BRELA. Lakini kama utataka kutumia majina mfano. Mjamaica enterprises, Mjamaica general suppliers, mjamaica industries, Mjamaica ltd nk itabidi uanzie BRELA kusudi ijulikane kama kuna kampuni nyingine lenye jina hilo.

Kama unatumia jina lako binafsi na unaona labda kampuni inaweza kuwa kubwa au kuwa inaweka matangazo kwenye vyombo vya habari ni vizuri usajili jina lako BRELA hata kama ni la binafsi. Hii ni kwa sababu mtu mwingine akiwahi kusajili jina hilo (labda anaitwa hivyo pia) hautaweza kuweka matangazo yako kwa sababu anaweza kukushtaki. BRELA ina hakikisha kwamba hakuna kampuni mbili zitakuwa na jina linalo fanana na la kampuni nyingine.

Anaye wahi kusajili jina la biashara BRELA basi haitakubalika kamwe kampuni nyingine kuitwa jina hilo hilo. Inakuwa ni jina la kipekee na inasaidia sana kwa sababu mfano ukilipwa kwa cheki inamaanisha mtu yeyote mwenye jina kama lako anaweza kuchukuwa ile cheki na kuingiza kwenye akaunti yake na kulipwa hela yako.

Ndio sababu benki wanaitisha vyeti vya BRELA wakati wanafungua akaunti za biashara na wanaenda kufanya search huko huko BRELA kuakikisha ni vyeti vya kweli.
 
Wana jamii, naomba niulize jinsi ya kusajili kampuni hapa nchini. Ni taratibu gani za kufuata? Mie nipo Arusha. Asanteni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom