Jinsi ya kujisajili kuwa mwanachama wa JamiiForums.com

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,265
Habari,

Kama bado sio Mwanachama wa Jamiiforums unaweza kujisajili kwa kufuata hatua hizi chache na rahisi zifuatazo:

1. Pakua App ya Jamiiforums kwenye kifaa chako (Simu au Kompyuta)

Katika hatua hii unatakiwa kupakua App ya Jamiiforums na ku-Install ndani ya kifaa chako. App hii utaipata ndani ya kivinjaro chako (Browser) kwa kufuata utaratibu uliobainishwa katika andiko hili chini: Jinsi ya Kuistall App ya ya Jamiiforums. Unashauriwa kutumia Browser ya Chrome na Firefox ili kuipata App hii kirahisi zaidi.

NOTE: App hii unaweza kuitumia kwenye PC, Tablet (iPad zikiwemo) na Simu za Mkononi (Android na iPhones). Kujua namna ya kuinstall


2. Fungua App yako
Baada ya kuistall App yako Utaona sehemu imeandikwa log in, iguse kisha itakupeleka sehemu imeandikwa log in na sehem nyingine imeandikwa Register.

1684409934475.png

Picha: Mshale mwekundu unaonesha sehemu ya kugusa baada ya kufungua hapa


2. Chagua/ Gusa sehemu iliyoandikwa Register now
Baada ya kugusa neno log in inakuleta sehemu ya pili ambayo inakupa machaguo mawili, kuigia kwenye akaunti yako kulog in (kama una akaunti) au kujisajili (Kuregister) ikiwa hauna akaunti. Hivyo, ili kuanza mchakato wa kufungua akauti mpya chagua sehemu iliyoandikwa Register now. Tazama kwenye picha hii hapa chini:

1684410961779.png

Picha: Sehemu ya Register now unayopaswa kuigusa ili kuanza kujisajili kuwa Mwanachama wa Jamiiforums

3. Chagua jina unalotaka kutumia unapokuwa Mwanachama wa JF
Baada ya kugusa Register now itakuleta sehemu ambayo utapaswa kuchagua jina unalotaka kutumia ukiwa Mwanachama wa JamiiForums. Sehemu hii imeandikwa Username: Required. Tazama kwenye picha hii hapa chini.

1684411124565.png

Picha: Utaweka jina lako ulilochagua ndani ya sehemu iliyozungushiwa rangi nyekundu

Katika hatua hii unaruhusiwa kuchagua jina lolote utakalotaka likumbulishe ukiwa Mwanachama wa JF. Hapa unaruhusiwa kutumia jina lako halisi au la kubuni. Unashauriwa kuchagua jina lolote ambalo haliashirii matusi, udhalilishaji au kukiuka maadili.

4. Weka Email (barua pepe yako)
Katika hatua hii mtu anayehitaji kujisajili JF analazimika kuweka email yake ili kurahisisha mawasiliano pale atakapohitaji huduma pale anaposahau taarifa zake za awali. Sehemu hii imeandikwa Email: Required. Unashauriwa kuweka email kwa usahihi.

1684411312666.png

Picha: Weka barua pepe yako (Email) ndani ya chumba kilizungushiwa rangi nyekundu

5. Chagua Nywila (Password) imara
Hii ni hatua ya pili kwa umwisho katika mchakato wa kuwa mwanachama wa JF. Hapa unashauriwa kuweka neno au namba lolote la siri ili kulinda akaunti yako unayoiunda isiingiliwe na mtu mwingine katika chumba kilichoandikwa Password: Required.

Kujua namna ya kutengeneza Password imara soma: Namna ya kuunda Password (nywila) imara

1684411590902.png

Picha: Weka nywila yako katika chumba kilichozungushiwa rangi nyekundu

6. Bofya neno Register
Hii ni hatua ya mwisho kabisa ya kukamilisha mchakato wa kuwa mwanachama wa JamiiForums. Baada ya kuweka user namna, email na Password utagusa sehemu ya mwisho iliyoandikwa register ili kutuma taarifa zichakatwe kwa muda mfupi na kisha kuruhusiwa kuwa Mwanachama mpya wa JamiiForums.

1684412113048.png

Picha: Sehemu iliyozungushiwa mstari mwekundu inaonesha unapotakiwa kugusa ili kuwa Mwanachama.

Pia Soma:
- SoC03 - Namna ya kuweka andiko lako ndani ya jukwaa la Stories of Change 2023

Ikiwa utakwama au kuhitaji msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia Support@jamiiforums.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom