miles45
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 3,478
- 8,325
Kipindi hicho nipo chuo mwaka wa pili nikiendelea kula kitabu na kufurahia maisha ya chuo bila stress na bata za chuo zikiendelea kama kawaida.
Basi nilipanga mtaani kwenye nyumba ambayo ilijengwa na mzee mmoja hivi alitambulika kwa jina la (katili) na huyu mzee alikua ni katili haswa amewanyanyasa sana wanafunzi na kodi yake ulikua hauvushi hata siku mbili ya tatu vyombo vyako vyote vipi nje. Na ukileta mdomo matusi na vibao unapigwa na hauna cha kumfanya alikua ni mjeuri haswa.
Na pia eneo lililo jengwa hii hostel ni eneo lenye thamani sana ila yeye alilipata kwa kumkopesha laki nane mama mjane alipe ada za mwanae hivyo huyu mama akashindwa kulipa riba zikazaana hadi akataifisha uwanja na kujenga hizi hostel.
Pia ni mzee ambaye ukikopa hela zake huwezi zirudisha na kazurumu wengi kwa hiyo staili nenda popote atakushinda.
Mimi na yeye tulikuja kukwaruzana hapa ...ilikua ni siku kaja kutembelea mjengo wake akanikuta najiandaa kuenda kupasha. Basi akaniuliza taarifa za mpangaji mwenzangu nikamjibu sifaham chochote ile kifupi akakaa kimya baada kama ya dk mbili tatu akaniuliza za mtu mwingine nikamjibu mzee wangu samahani sina taarifa za mtu yoyote.
Akaniuliza tena kwani wewe unaishije na wapangaji wenzio nikamjibu naishi nao vizuri tu. Akaniuliza kwa nn sina taarifa zao nikamjibu Mimi sio msemaji wao wala wao hawajanipa maagizo yotote juu yako. Nikawa nanyanyuka kuingia ndani niweke mambo sawa niende zangu zoezi.
Ile natoka akaniuliza we kijana mbona jeuri sana . Nikamuuliza kwa nn unanihukumu bila sababu...? Au kuna kodi unanidai....akaniambia hii jeuri unaitoa wapi mtoto mdogo kama wewe bado unanuka mikojo ya mama yako....? Hii kitu ilinistua na kuteka attention yangu haswa. Nikageuka na kumuambia mzee samahani nimekukosea nini......? Akanijibu ungekua na jeuri ungejenga nyumba yako.
Sikutaka kuwa mnyonge niliendelea kukaza maana huyu mzee alijua kila mtu atamuhusudu kama anavyo husudiwa na wengine.
Basi akawa anakuja usawa wangu huku akisema kama kwetu sijafundishwa adabu basi yeye atanifundisha (moyoni nikasema kwa msenge kama wewe ambae sina cha kupoteza naona leo anguko lako limekuja) hapo nikiwa nimevaa six zenye meno ya chuma chini nikawa kama najiweka sawa kwa ajiri ya mapambano nikaona kama amejaa maji hivi akaropoka sikutaki kwenye nyumba yangu nikirudi nisikukute.
Nikasema we mzee hujitambui kwanza hii nyumba tupo kukufariji tu hapa kifupi hapa hamna kitu haya mabanda yako kwetu tumefugia kuku. Watu wakawa kama wamejaa pale nae zoezi alilo jia likawa kama limesitishwa akaondoka na mm nikaendele na ratiba zangu .....
Sikujua kinacho endelea kumbe mzee kaenda kubeba police .....
Inaendelea...