Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,518
- 34,322
Asubuhi ya leo wakati navua raba nilipotoka mazoezini, ghafla lilinijia wazo la ni nani alikuwa anaivaa raba hiyo kabla haijaletwa Tanzania kama mtumba?
Nikaanza kuangalia jinsi mitumba ilivyotawala maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa Sana. Lakini huwa tunajiuliza hiyo mitumba ilikotoka ilikuwa inatumiwa na nani?
Kwa mfano magari ingawa hatupendi sana kuyaita mitumba, badala yake tunayaita "Used" lakini ukweli wa mambo na yenyewe pia ni mitumba.
Unaweza kuwa unachukia watu wenye tabia ya ushoga, lakini una hakika mitumba unayotumia hakuna ambao ulikuwa unatumiwa na shoga kabla ya wewe kuununua?
Ipo mitumba toka kwa wezi, majambazi, makahaba, watu wa dini tofauti na sisi, wabaguzi, wauwaji, wafungwa, wabakaji, matapeli na lundo jingine kubwa sana la watu tusiowapenda.
Unapotumia mtumba jua kuwa inawezekana kabisa kabla ya kuletwa Tanzania huko ulikotoka ulikuwa unatumiwa na mtu/watu usiowapenda kabisa.