Jinsi Mgambo alivyonidhalilisha mbele ya Askari Polisi

Witch hunter

JF-Expert Member
Nov 21, 2018
1,437
3,320
Ndugu zangu niliona uzi humu ukikataza kuwa na urafiki na askari polisi, ila mimi nakazia zaidi hata hawa mgambo ni wa hovyoo tu.

Kuna mgambo alikuja kwangu kunipa taarifa kwamba nahitajika kituo cha polisi akanipa na sababu ya wito, basi sikuwa na hiyana nikamwambia twende. Kwa kuwa nafahamika hapa mtaani hakuona haja ya kunifunga pingu kama wahalifu wengine hivyo tulitembea mdogo mdogo kuelekea kituoni huku tukipiga story mbili tatu maana ni mtu tunayejuana.

Cha ajabu tulipokaribia kufika kituoni, na baada ya kuona askari pale kituoni, mgambo yule alinigeukia na kuniuliza kwa ukali “unataka kugoma? Unataka kugoma? Hata wale askari walimsikia. Kabla sijamjibu akashika suruali yangu kwa nyuma akaniinua nikaanza kutembelea vidole, kisha akaanza kunipiga huku tukielekea kuingia kabisa kituoni tena mbele ya askari.

Sikutaka kufanya fujo maana askari wa Bongo nawajua, ila nimemtunza tu huyu mgambo. Ipo siku mtamsikia kwenye vyombo vya khabari. I SWEAR ON MY LIFE.
 
Mchapie mkewe tu hakuna namna bora ya kurevenge zaidi ya hiyo.
Pili tafuta hela ndugu yangu,masikini nchi hii wanaonewa sana ukiwa na hela unakuja kukamatwa na OCS au OCD sio mgambo,kwanza mi mgambo akiniambia twende kituoni siendi,who are you?
Mgambo ana rank sawa na constable wa polisi. Kifupi mgambo ni sawa na askari polisi asiye na cheo chochote, wale nguo plain. Na hapo ni mgambo plain sio yule mwenye mbavu za chini.
 
Mchapie mkewe tu hakuna namna bora ya kurevenge zaidi ya hiyo.
Pili tafuta hela ndugu yangu,masikini nchi hii wanaonewa sana ukiwa na hela unakuja kukamatwa na OCS au OCD sio mgambo,kwanza mi mgambo akiniambia twende kituoni siendi,who are you?
Inategemeana na mazingira mkuu, huku kwetu ukigoma watakuja hata mgambo wa 5 watakunyoosha hatariii. Pia askari ni kama wamewakabidhi mgambo ofisi.
 
Wakati mwingine reasonable force inatumika endapo kuna umuhimu ili kufanya mtuhumiwa au mshukiwa apunguze kibri na majivuno.

Katika mafunzo ya mgambo wanafundishwa jinsi ya kufanya mtu ajisikie vibaya.

Sikupi pole manake mwanaume kupata misukosuko ya polisi ni kawaida sana.
 
Sawa mheshimiwa Mgambo. Reasonable force inaanza kutumika kituoni? Tena mbele ya askari? Reasonable force eehh? NTAMNYOOSHA
 
Nimecheka ingawa upo serious, kwani ulikosea nini meku mpaka ukwe mtu kati, mkasa ni kama haujaisha
 
Back
Top Bottom