Jifunze silaha kuu tano (5) za ulimwengu wa kiroho ili upate ushindi kwenye kila jambo

Asante Mr 7seven kwa kazi nzuri, nikifanikiwa kupenya nitakuja na hilo somo.
Huku upande wa Nuru kiongozi wa mambo yote ni Roho Mtakatifu, ukishampata huyu ndiye anayekuongoza katika maombi.

Halafu unampata Yesu ambaye huyu tunaweza kumuita Operational Manager(maana tunavyosema damu yake, Neno lake na Jina lake linafanya kazi).

Sasa ili uvitumie vitu vyote vya ufalme wa Nuru ni lazima uwe navyo vyote, kuvipata ni bure hakuna gharama yoyote ile.

Huwa ni kwa mtu yeyote yule mwenye uhitaji naye maana Yeye ukishaonyesha nia anakuja ndani yako kukusaidia.

Ila kabla ya yote lazima upate mtu/mtumishi sahihi atakayekuongoza sala ya toba ili Roho Mtakatifu aweze kuingia ndani yako na kuanza kukufundisha jinsi ya kubomoa, kuvunja, kuharibu, kusambaratisha nguvu za giza, kurejesha kila kilichoibwa na shetani na kuishi maisha matakatifu yampemdazayo Mungu.

Ukishampata Roho Mtakatifu, maisha yako yanaanza kubadilika kimtazamo, kimaono, kimaongezi, kimatendo, kimaamuzi hata kifikra. Anakuwa anakushauri kufanya mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuona; ndio maana wale wasiomjua huwa wanasema ni uwendawazimu kuzungumzia mambo ya Mungu.

Siyo wao, ni fahamu zao zimetekwa, macho yao na mioyo yao iko mbali na Upendo wa Mungu hawawezi kuuona au kuhisi mguso wa Mungu.

Hivi umewahi kuona mtu anayeombewa analia? Hii ni kwasababu anakuwa ameguswa na Mungu, ametolewa mizigo,amefarijiwa, ameguswa na yule aliyemuumba. Wengine wanamuona Mungu katika ndoto ndio maana wanajikuta wanalia.

Watu wengi huota ndoto za namna hii za kulia machozi, kuna mawili.
1.Wameonana na Mungu kiroho, hii inasababisha kushindwa kujizuia. Furaha inazidi kipimo, ni sawa na mtoto ambaye hajawahi kumuona mzazi wake, sasa itokee siku amemuona, jinsi atakavyopata furaha ndivyo mtu anayekutana na Mungu huwa anafurahi namna hiyo.

2.Mtu analia kwenye ndoto ni kwasababu amekutana na Mungu na amejibiwa maombi yake;Hapa usichanganye, siyo lazima uamke asubuhi na kukuta umejibiwa la hasha! Ila matokeo yake huonekana baadaye. Ndio ile unasikia Mungu amenifuta machozi, amenishindia kesi, amenipa mtoto, ameniponya n.k

Sala ya toba inatolewa na mtu yeyote mwenye ujazo wa Roho Mtakatifu,hata mimi naweza kuiandika hapa na mtu yeyote mwenye uhitaji akaitamka kwa imani na akaanza kuitumia huku akiendelea kupata mafundisho mbali mbali ya Kristo .

Maana mtu asije akasema anataka kutumia silaha za Nuruni kama hamtaki mwenye silaha zake, hapa haziwezi kufanya kazi maana ni kama unaiba vitu vya mwenyewe.

Upande mwingine wao nao lazima utamke maneno vile vile na ukiri, utoe kafara au sadaka ya kitu, vitu, fedha n.k.ila huu upande gharama yake ni kubwa na masharti yake ni magumu.

Siku ikitokea umeacha masharti. Mfano umeumwa hujiwezi na huna mtu wa kimwambia haya mambo maana huwa ni ya siri, umekufa; familia yako itapata taabu sana maana yenyewe haitaweza kujua jinsi ya kufanya, sasa hapo ndipo inapoanza kudaiwa.

Kama ulipata mali zitaanza kupukutika, kama ni damu inahitajika, mifugo hata watu wataanza kufa, magonjwa yanajitokeza ya ajabu ajabu, umasikini wa kupindukia unaanza kuinyemelea, mikosi, nuksi zinapishana tu ndani.

Pia ukikosea tu masharti moto wake utauona. Huu upande aisee una gharama kubwa.Kubwa kuliko ukifa kabla hujatubu ni kwenda motoni moja kwa moja,hakuna msamaha. Hata wale wanaosemaga eti maiti inaombewa ili isamehewa dhambi ni kujilisha upepo tu maana Mungu hasikii maombi ya wafu,Yeye ni Mungu wa walio hai. (Hakuna tijara kati ya walio hai na wafu).

Upande wa nuru hauna majuto usipolipwa wewe kikubwa watalipwa watoto, wajukuu, vitukuu hata vilembwe mpaka kizazi cha 7,huu upande ni wa kutunza ahadi na kuzitimiza.

Kuna watu huwa wanasema hawajawahi kuona mauzauza hawaamini uchawi, ushirikina, uganga, kulogwa na wanasema mambo ya Mungu ni upumbavu kwani hayapo, ni ujinga na ni mambo ya kufikrika.

Hapa huwa kuna mambo kadhaa

1.Mosi ni watu wanaojua wanachokifanya kuwarubuni watu wasimjue Mungu ili wafanye uovu na kuangamia. Watu wanaofanya hivi mara nyingi ni zile roho ambazo zimekwisha hukumiwa hata ziombe toba ya namna gani haziwezi kusamehewa (hizi ni roho za kuzimu zenye miili ya wanadamu zinatafuta wafuasi wa kwenda nao jehanamu ya moto).

2.Hawa ni watu ambao roho ya mpinga Kristo iko ndani yao na inafanya kazi ili kutimiza maandiko na kwasababu ya imani haba ya watu na kutokuyasoma na kuyatafakari maandiko wanashindwa kujua nyakati za kurudi kwa Kristo.

3.Hawa ni wale ambao unakuta kwenye kizazi chao alikuwepo mtu aliyesawazisha haya mambo kwahiyo hawana shida maana hakuna vizuizi vya kuwakwamisha hawana shida ya kumtafuta wala kumjua Mungu, maana hawasumbuliwi na shetani na Mungu hana kipingamizi kwenye maisha yao anakumbuka agano alilolifanya na mtu wake.

4.Hawa ni wale mawakala wa shetani ,watumishi wake watiifu, ambao ukiongelea mambo ya Mungu wanaona ufalme wao wa giza unaharibika na watakosa washirika, pesa.Wanafanya kitu wanachokijua ( waganga wa kienyeji wa kweli,wachawi, washirikina, wapunga mapepo, wasoma nyota n.k)

5.Hili kundi ni watu ambao ni bendera fuata upepo, hawajui chochote wanachokisoma kwa mitandao, vitabu, tafiti mbalimbali zinazopinga uwepo wa Mungu ndio wanaziamini, au kwa kuwa fulani kasema basi ndiye sahihi (Wengine wamejazana makanisani kwasababu wamezaliwa wakawakuta wazazi wao ni wa dhehebu fulani basi na wao wanasali hapo ,ukiwauliza Mungu amekutendea nini binafsi hawezi kukwambia hata 1).

Mimi nimejikita kwenye mafunuo, mwalimu walker water na Einstein 40 wataelezea vizuri roho ya mpinga Kristo na Nabii wa Uongo maana wako vizuri sana kwenye hili.

N:B Kuna sehemu umefunga sikupati mkuu.
Tupo pamoja mkuu 7seven
 
Karibu sana mkuu,upatapo muda naomba usiache kusema neno juu ya hili.

Pia mimi ninavyoona kila kiongozi anayekikalia kiti cha uongozi wa juu kuna mahali anajisahau anaamini kwamba atatawala kwa akili zake, ataamini wataalamu wake na nguvu ya kijeshi (kimwili) pasipo kiroho.

Hata kama atatumia kiroho, je anakuwa yupo upande sahihi? Kwanini imeandikwa kwamba usipomtegemea Bwana nchi yako itatoa mazao na kuliwa na nchi nyingine?
Tuna rasilimali nyingi sana lakini mbona hazitunufaishi?

Ni kweli sisi ni Lango na ndio maana tuna agano na Mungu kwa ajili ya kutimiza kusudio lake lakini hatuwezi kuwa sehemu inayotufaa kiuchumi kama hatutazilinda rasilimali zetu pasipo kumuhusisha aliyeziweka hapa nchini mwetu.

Hivi Kiongozi wetu mkuu alishawahi kutoa sadaka kwa ajili ya nchi yake aweze kutawala kwa haki ,usawa, amani na kufanikiwa zaidi? Kama huwa anatoa,Je, huwa anatoa kwa haki, anazitoa sehemu sahihi?

Viongozi wake waandamizi nao huwa wanatoa sadaka ili wapate hekima ya jinsi ya kuwaongoza Watanzania kwa haki na Usawa?

Huwa najiuliza maswali mengi sana,kwanini sisi ni masikini, kwanini mali zetu hazitunufaishi, tena anayetakiwa kuwa makini katika kuhitaji hekima ya Mungu kuongoza ni Kilimo maana hii ndio uti wa mgongo(ardhi),Madini, Nishati, Utalii na Maji.

Lakini ikiwa siku moja atatokea Kiongozi ambaye ataamini katika moyo mkunjufu na kuyatafuta maarifa ya kiroho katika upande ulio sahihi ninaamini atafanikiwa sana na ataweka historia iliyotukuka katika dunia hii. Bado kitambo kidogo tu atatokea.
Shida ipo kwa raia wa tanzania na kwa watu walioitwa kwa jina la Mungu!
 
Sawa.Sala ya toba.Omba hivi.
Baba katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai.Mimi mtoto wako (taja majina yako),ninakuja mbele zako,mimi ni mwenye dhambi ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokutenda, kwa kujua ama kutokujua, nilizozishiriki au kushirikishwa, ninaomba unisamehe, futa majina yangu kwenye kitabu cha hukumu na andika majina yangu kwenye kitabu cha uzima.

Roho Mtakatifu ingia ndani yangu ili unisaidie kuishi maisha matakatifu. Kuanzia leo ninamkataa shetani na kazi zake zote.

Ahsante Bwana Yesu kwa kunisamehe dhambi zangu zote ninaamini jina langu limeandikwa kwenye kitabu cha Uzima. Amen.

Hapa wakati unaongea hivi hakikisha dhamiri yako haikusuti, usijutie dhambi yoyote, usije ukajiona una hatia tena kwenye moyo wako. Amini umetakasika na umesamehewa na hakuna atakeyeweza kukufunga tena.

Usiangalie ukubwa wa dhambi ,Mungu husamehe dhambi zote ,kubwa na ndogo Mungu anasemehe, hata kama uliwahi kuua na damu ya mtu imekuwa ikikuandama, wewe tubu utajisikia umepata amani.

Uzuri wa hii sala huwa haifutiki ,yaani hapa unakuwa umejisajili rasmi kuingia mbinguni. Maana ukiwa unaisema malaika wa mbinguni huwa wanasimamisha shughuli zao zote na kushangilia kwasababu roho iliyokuwa imepotea imeokolewa.

Kwahiyo siku ukijikwaa kwenye dhambi damu ya Yesu inakutakasa na kukusafisha, na unarudi kuwa kundini, unaposema hii sala,kuna vita inaibuka, ila usiogope maana Mungu anakuwa yuko na wewe ,hata ukitenda dhambi tena bahati mbaya wewe tubu tu usijione Mungu amekuacha.

Mpaka uje kusimama lazima ujikwae mahali ,uanguke tena,ndio maana huwa unasikia watu wanasema huyu bado mchanga kiroho, huwezi kuzaliwa ukakua hapo hapo na kuanza kukimbia,lazima ubebwe, utambae na kuanza kusimama, hata kiroho ni hivyo hivyo.

Hata mimi ninayeandika haya bado sijafika mahali naweza kusema ni msafi,msije mkaona nakosea mkakata tamaa, bado najifunza na kufunza wengine tunatofautiana viwango. Lakini sote ni watoto wa Mungu.

Sala hii inasemwa na yeyote, awe Mkristo, Muislam, Mbudha,Mpagani, yeyote apendaye, haimfungi mtu. Silaha zote hizi za ulimwengu wa roho zinatumiwa na wote waliojisajili kwenye ulimwengu wa Nuru.

MBARIKIWE SANA WOTE MPENDAO KUYATAFUTA MAARIFA YA MUNGU ILI KUUSHINDA UFALME WA GIZA.

Amina. Naomba vitabu vya Biblia vya kusoma.
 
MIMI SIYO MWANDISHI MZURI KABISA TENA KABISA:,, Siku ya jana nilikua kwenye maombi ya kuombea aridhi, asubuhi hii ya saa 12,nimepatwa na ndoto hii, kwamba nilikua nimelala na nilivyoamka nikajikuta nimelala kwenye jiwe(yale mawe ya majini lakini siyo kubwa bali ni bapa),chakushangaza hapakua nyumbani bali palikua kwa bibi angu mzaa baba,, basi nilivyogundua kua nipo sehemu siyo nilichanganyikiwa huku nikimtuhum bibi kua ndo kanifanyia mchezo ule, baada ya kuona hivyo niliingia ndani mwake nkiwa na jaziba na kuanza kumkemea kwa maombi na nilifanikiwa kumdhibiti. WAKUU Walker Water, 7seven e.t.c, naombeni ushauri zaidi nifanyeje kuhusu ndoto hii maana inanikosesha amani,, hasa ilipoonekana kwamba nimeamkia pale kwa bibi kimiujiza tena kwenye jiwe... Einstein 40
Ile kwamba ulikuwa kwenye jiwe ni moja ya dalili kuwa tayari ulikuwa umeshinda, maana maji yaani dhoruba ilikuwa imekuzunguka na wewe uko juu yake tena kwenye jiwe, ukienda kuchunguza ndani ya biblia kuhusu mawe au jiwe ni kuwa Yesu ndiye mwamba na jiwe kuu la pembeni

Hii ni ushindi mkubwa kuwa umevuka kwenye kile kilichokuwa kimefunga kwa aridhi uliyopo
 
Mbinguni kuna vitabu 3 vyenye majina ya wanadamu. Vitakuja kusomwa siku ile ya hukumu ya mwisho. Mwenye mamlaka ya kusoma hivi vitabu ni Yesu Kristo Mwenyewe maana Yeye ndiye Lango la kuingia mbinguni.

Mtu yeyote atakayeingia mbinguni lazima awe amesajiliwa kwenye vitabu hivi, asikudanganye mtu mwenye kutoa ruhusa ya kuingia au kutokuingia ni Yesu peke yake. Yeye ana mamlaka ya kuhukumu aliyopewa na Mungu, ukiniambia kwanini apewe Yeye sina jibu la moja kwa moja ila Mungu allisema alipendezwa naye ndio maana akamuweka juu ya mamlaka ya ukuu,ufalme na usultani wote.

Ni sawa sawa na Rais ambavyo huwa anateua mtu fulani awe mkuu, mfano Waziri mkuu, nani anaweza kumuhoji Rais kwamba kwanini umemteua fulani awe Waziri mkuu, nani anaweza kusema mimi huyu simfuati kwasababu simpendi? Rais akisema ni sheria hakuna wa kumpinga kwenye nchi.

Na kwa Mungu ni hivyo hivyo alimpa Yesu mamlaka ya kuhukumu na kutenda kazi za Mungu kwasababu anazijua, kwahiyo huwezi kumjudge wala kumquestion Mungu,Yeye humpa yule ampendaye.

Sasa turudi kwenye vitabu 3.
1.Kitabu chenye majina ya watu waliomkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Hiki ni kile ambacho tumeomba sala ya toba. Pigania vyote jina lako lisikose kwenye hiki kitabu.

Siku ya hukumu ya mwisho tutakuwa tunaitwa majina tunakwenda upande wa kulia wa Yesu Kristo baada ya parapanda kulia. Hapa ambao tutakuwa humu kwenye hiki kitabu tutashangilia sana na kuruka ruka kama ndama. Tutapewa mataji ya ushindi. Hapa tunasubiria kwenda paradiso kumuona Mungu live. Maandishi yangu haya yataonyeshwa kwa wote walioyasoma na kuamini na ambao waliyakataa kwa kusema huyu anaandika ujinga.

2.Kitabu hiki cha pili ni kile ambao walimkataa Yesu wakaacha kutubu, waliokumbatia eti dini zao, na wote wenye dhambi na waliokubali muhuri wa mpinga Kristo. Hawa ndio watakuwa wanalia na kusaga meno siku hiyo.Maana jehanamu itakuwa inaunguruma kwa sauti ikiwaita waingie waanze kuchomwa huku waking'atwa na funza,hawa funza moto hauwaunguzi. Hakuna hasara kubwa ambayo iliwahi kumpata mwandamu kama hii kuingia kwenye hiki kitabu. Kinatisha.

3.Kitabu cha tatu ,hiki ni wale ambao waliandikwa kwenye kitabu cha awali lakini matendo yao yalikuwa dhaifu, walitegea kazi za Mungu, hawakutoa sadaka,hawakuwajali mayatima, wajane, kuwatunza wazee, kuwaona wagonjwa na kuwasaidia wenye uhitaji.

Hawa wataingia mbinguni lakini wataishi maisha ya masikitiko,maana hawatakuwa na maisha sawa kama wale walioishi kwa kufuata Upendo wa Mungu wa kusikiliza maelekezo ya Roho Mtakatifu.

Ukitaka kuamini mbingu na kuzimu kupo,ebu fuatilia mtu ambaye anakaribia kukata roho kwanini mara zote huwa anaongea ukweli?

Unadhani anasema tu hivi hivi? Anakuwa anaona mahali ambapo roho yake inakwenda hivyo anapenda kusawazisha hapendi kuacha deni hapa duniani na anakuwa anahitaji msamaha ili huko aendako aweze kupokelewa.

Mwingine hawezi kuongea chochote kwasababu kinywa chake tayari kimeshafunga kuna ukweli anauona ila kuusema hawezi,anashindwa kukutahadharisha kwasbabu alitakiwa kutengeneza akiwa bado hai,ana nguvu za kufanya hivyo, kwahiyo Mungu anaamua kumfunga kinywa si alimkataa? Nilikupa nafasi ya kutubu mara nyingi ukagoma sasa hivi umekata kauli ndio unamuhitaji Mchungaji;kufa na uovu wako ili uadhibiwe vizuri.

Unadhani kwanini Hitler na ubabe wake wote alimuhitaji Mchungaji kabla hajajiua?Tayari alishajua anapokwenda alitaka kusamehewa dhambi zake, ukiniuliza alisamehewa au lah, mimi sijui mwenye kusamehe dhambi za mtu na kumhesabia haki ni Mungu peke yake.

Fidel Castro na upelelezi wake wote na alivyowakwepa CIA miaka yote na alivyokuwa haamini mambo ya Mungu kabla hajafa aliomba toba, kwanini asingekufa pasipo kuamini?

Hapa kwetu Kingunge alikuwa haamini uwepo wa Mungu lakini mwishoni aliomba padri amfanyie kitubio kitakatifu na kubatizwa, sasa kwa elimu ya mzee yule aliyokuwa nayo unadhani hakuona kitu cha kumstaajabisha?

Kama utasema waliogopa kifo, mbona hawa ambao huwa wanatuusia mambo kabla hawajafa tusipofanya kama walivyosema huwa yanaturudi? Hapo anakuwa yupo katika ubindamu kamili na uungu.

NB.Ukiona unakiwaza kifo halafu unapata hofu ujue kuna mambo hujayatengeneza na Mungu na ukifa unaenda sehemu isiyo salama.
AU
Kifo chako kinawahishwa muda wako wa kufa bado, ni watu wabaya wanakutumia roho za mauti, hivyo kemea roho ya mauti na vifo kwenye familia yako au watu wako wa karibu maana wakikukosa wewe wanaenda kwa wapendwa wako ili wakutaabishe.

Uzuri wa nuruni kama MUNGU akitaka kukuchukua anakupa taarifa hivyo kama ulikuwa hujajipanga, unajikuta unajiandaa kwa kujitakasa na kutubu na unakuwa hukiogopi kifo maana unajua unaenda kustarehe.

Ukiwa nuruni ni sawa umekata bima ya maisha yako ya milele katika ufalme wa Mbinguni ambapo hakuna usiku wala mchana, hakuna magonjwa wala uasi, mateso wala manyanyaso, kuna furaha ya ajabu sana.Ninatamani watu muanze kuuona huu ufalme katika maono na ndoto. Japo ninajua kuna watu ambao wanaujua kunishinda mimi.

Gizani bwana ni ghafla tu umekwenda Mungu hakulindi maana si wake, kwahiyo watu waache kumsingizia Mungu eti watu wake iweje wafe? Ukimfuata shetani wewe si wa Mungu huna dhamana kwake shetani akikutaka anakuchukua wakati wowote.

Hujawahi kujiuliza kwanini mtu anayekwenda kwa mganga kuaguliwa hatakiwi kumwambia mwenzake kwamba nimeaguliwa kwa fulani? Sababu ili asimjue maana hakawii kwenda kumwambia mganga amwambie ametumia uchawi gani ili amloge tena;na mganga akipewa dau anakandamiza tena hapo hapo au anamwambia nenda kwa mganga fulani ni mkali zaidi yangu ,yaani huu ufalme ni kaa chonjo hakuna kulala mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama.

Nuruni ukishaomba umeomba unalala usingizi mnono sana, una amani maana unao ulinzi wa Yesu, una furaha maana mizigo imeondishwa kwako. Una tumaini la kuishi, kwasababu Upendo wa Yesu umekuzunguka.



Je,wewe unapenda kuwa katika kitabu gani kati ya hivi 3?.
Samahani hicho kitabu ni cha makaratasi kama hivi vyetu au cha namna gani?
 
Shida ipo kwa raia wa tanzania na kwa watu walioitwa kwa jina la Mungu!
Tena hawa waitwao kwa jina la Mungu wao ndio wanaosababisha wengine kuyumba na kupoteza imani kwasababu ya kujifanya wajuaji. Unakuta Mtumishi huyu anamtuhumu yule eti si wa kweli kisa kafundisha mafunuo ambayo yeye hayajui au hayapendi, au anaona anasikilizwa sana ,sasa wivu unampata anaamua kumsagia sumu.

Sasa wengine walioko nje wanabaki wanajiuliza tumuamini nani ikiwa wao watuitao hawaaminiani?

Wengine wanashindwa kutambua kwamba viwango vya utumishi vinatofautiana, sasa mdogo hataki kumpa heshima yule aliyemzidi, naye anavimba kuwaonyeshea washirika wake kwamba hata yeye yuko juu ,yule anafundisha uongo. Ni upuuzi tu na kutoyajua maandiko.

Mara eti chumvi ,mafuta, udongo ni mafunuo ya uongo wakati vyote viko ndani ya Biblia, sasa hawa watumishi huwa wanasoma maandiko gani. Elisha alitumia chumvi kuponya maji machungu yakawa safi kutumika, Yesu alipakwa mafuta tena na yule mwanamke kahaba aliyeomba kusamehewa dhambi zake, Yesu alitumia ardhi kuchora chini ikamwambia siri zote za watu waliokuwa wanataka kumpiga mawe mwanamke aliyekamatwa kwa dhambi ya uzinzi. (Akasema anayejiona hana dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe, hakuna hata mmoja aliyethubutu maana kila mtu alivyojitazama nafsini mwake alisutwa na walijua amejua dhambi zao).

Alitumia pia udongo kumponya kipofu. Sasa njoo kwa hawa watu walioitwa kwa jina lake uone wanavyoshinda wanakimbizana kusemana vibaya. Watu hawana muda wa kukaa katika kusudi la Mungu ili wamjue na kufunuliwa siri za Mungu wanabaki kukariri mistari tu bila kupata neno ndani ya maandiko.
 
Amina. Naomba vitabu vya Biblia vya kusoma.
Ili uwe vizuri zaidi somo Biblia yote kuanzia Mwanzo mpaka Mwisho (Ufunuo wa Yohana).Soma kwa mtiririko usiruke hata kurasa moja,na usiwe na haraka kuimaliza, pata muda wako mzuri uende nayo taratibu.

Ukipewa vitabu tu, kuna mistari mingine hutaisoma na ni rahisi kudnaganywa na watu kwamba imeandikwa hivi na vile kumbe sivyo.

Huwa ninashangaa sana kuna watu wanajiita watumishi lakini hawajawahi kuisoma Biblia yote, watu kama hawa lazima wayumbe maana vitu vingi wanakuwa hawavijui.
 
Ile kwamba ulikuwa kwenye jiwe ni moja ya dalili kuwa tayari ulikuwa umeshinda, maana maji yaani dhoruba ilikuwa imekuzunguka na wewe uko juu yake tena kwenye jiwe, ukienda kuchunguza ndani ya biblia kuhusu mawe au jiwe ni kuwa Yesu ndiye mwamba na jiwe kuu la pembeni

Hii ni ushindi mkubwa kuwa umevuka kwenye kile kilichokuwa kimefunga kwa aridhi uliyopo
Nilimjibu hivyo hivyo kama vile tulikuwa wote
 
Samahani hicho kitabu ni cha makaratasi kama hivi vyetu au cha namna gani?
Maono haya aliyaona Yohana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana mmojawapo wa Mitume wa Yesu akiwa katika kisiwa cha Patmo.

Kwanza hivi vitabu 3 nilisahau kuvipatia majina yake kama vinavyoitwa ili vieleweke kwa urahisi.

Kitabu cha kwanza kinaitwa kitabu cha UZIMA.

Kitabu cha pili kinaitwa kitabu cha HUKUMU.

Kitabu cha tatu kinaitwa kitabu cha MATENDO YA UZIMA.

Kwa jinsi Yohana alivyokiona aliona ni kitabu cha kawaida kama hivi vyetu vya makaratasi ndio maana akaita naliona kitabu kikifunguliwa.

Hata Yesu alivyofuatwa na wanafunzi wake kumwambia kwamba wametoa pepo na wamewatii, akawaambia msifurahi kwa kuwa mmetoa pepo bali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa katika kitabu cha UZIMA.
 
Maono haya aliyaona Yohana katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana mmojawapo wa Mitume wa Yesu akiwa katika kisiwa cha Patmo.

Kwanza hivi vitabu 3 nilisahau kuvipatia majina yake kama vinavyoitwa ili vieleweke kwa urahisi.

Kitabu cha kwanza kinaitwa kitabu cha UZIMA.

Kitabu cha pili kinaitwa kitabu cha HUKUMU.

Kitabu cha tatu kinaitwa kitabu cha MATENDO YA UZIMA.

Kwa jinsi Yohana alivyokiona aliona ni kitabu cha kawaida kama hivi vyetu vya makaratasi ndio maana akaita naliona kitabu kikifunguliwa.

Hata Yesu alivyofuatwa na wanafunzi wake kumwambia kwamba wametoa pepo na wamewatii, akawaambia msifurahi kwa kuwa mmetoa pepo bali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa katika kitabu cha UZIMA.
Sawa nimeuliza hivyo kwasababu vya mwilini havifanani na vya rohoni kwa mujibu wa walimu humu, sasa kama vitakuwa vya makaratasi si vitakuwa vya mwilini tena ?pia nimejenga picha kitakuwa na ukubwa wa namna gani mpaka kiweze kuingiza majina ya binaadamu wote waliowahi kuishi duniani ?
 
Sawa nimeuliza hivyo kwasababu vya mwilini havifanani na vya rohoni kwa mujibu wa walimu humu, sasa kama vitakuwa vya makaratasi si vitakuwa vya mwilini tena ?pia nimejenga picha kitakuwa na ukubwa wa namna gani mpaka kiweze kuingiza majina ya binaadamu wote waliowahi kuishi duniani ?
Ni kweli kwa Mungu hakuna kinachoshindikana, kinaweza kiwe cha makaratasi kumbe kina mfumo wa Kompyuta, sasa miaka ile ya nyuma sana kipindi cha Yesu hakukuwa na Sayansi na Teknolojia kama sasa hivi,angeonyeshwa kwa nyakati za leo asingeelewa.

Zamani walikuwa wanasema nikaona magari ya farasi yatoayo moto, na wapanda farasi wameshika mikuki na ngao ya kuzuia mishale.

Au anasema niliona moto ukitoka mbinguni na kuanguka duniani na kuwachoma wanadamu.

Sasa ukija kwenye tafsiri ya sasa hivi,magari ya farasi yatoayo moto ni kama hizi tanks na magari ya kivita ya sasa hivi, mikuki ni bunduki, mishale ni risasi, ngao ni vest za kujikinga na risasi, au kizuio cha risasi na silaha nyingine. Wapanda farasi ni Wanajeshi/Askari.

Moto kutoka mbinguni haya ni mabomu ya kemikali, biolojia ambayo yakipigwa yanaleta maasi kwenye dunia.

Mara nyingi Mungu anaongea na mtu kwa kutumia Lugha ambayo inaeleweka kwa mtu huyo, anatumia mazingira na vitu ambavyo vimekuzunguka ili uwe na ufahamu kwa kile anachokizungumza.

Kwahiyo kama angesema majina yapo kwenye Kompyuta asingeweza kujua jinsi ya kuandika maana hajawahi kuiona. Vyovyote iwavyo majina yameandikwa /yanaandikwa mbinguni.Chukulia mfano nchi za wenzetu zilizoendelea wanajua watu wote katika nchi zao,je kama wao wameweza kwa Mungu kitashindikana nini wakati ujuzi na maarifa vyote vinatoka kwakwe?

Siku hiyo ya mwisho ukisema mimi sikutenda dhambi fulani ,inaletwa skrini inawashwa unaonyeshwa yale yote uliyokuwa ukiyafanya ndipo aibu ya kila mtu ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha UZIMA itaonekana kwa watu wote. (Hii nimeandika kwa Ufunuo wa sasa hivi, kwahiyo baadaye itatumiwa kama Kumbukumbu kwa kizazi hiki na kijacho kwasababu nyakati hizi sote tunazijua tv).

Maandiko yanasema hivi,"Kwa maneno ya vinywa vyenu mtahesabiwa haki na kwa maneno ya vinywa vyenu mtahukumiwa"
 
Ni kweli kwa Mungu hakuna kinachoshindikana, kinaweza kiwe cha makaratasi kumbe kina mfumo wa Kompyuta, sasa miaka ile ya nyuma sana kipindi cha Yesu hakukuwa na Sayansi na Teknolojia kama sasa hivi,angeonyeshwa kwa nyakati za leo asingeelewa.

Zamani walikuwa wanasema nikaona magari ya farasi yatoayo moto, na wapanda farasi wameshika mikuki na ngao ya kuzuia mishale.

Au anasema niliona moto ukitoka mbinguni na kuanguka duniani na kuwachoma wanadamu.

Sasa ukija kwenye tafsiri ya sasa hivi,magari ya farasi yatoayo moto ni kama hizi tanks na magari ya kivita ya sasa hivi, mikuki ni bunduki, mishale ni risasi, ngao ni vest za kujikinga na risasi, au kizuio cha risasi na silaha nyingine. Wapanda farasi ni Wanajeshi/Askari.

Moto kutoka mbinguni haya ni mabomu ya kemikali, biolojia ambayo yakipigwa yanaleta maasi kwenye dunia.

Mara nyingi Mungu anaongea na mtu kwa kutumia Lugha ambayo inaeleweka kwa mtu huyo, anatumia mazingira na vitu ambavyo vimekuzunguka ili uwe na ufahamu kwa kile anachokizungumza.

Kwahiyo kama angesema majina yapo kwenye Kompyuta asingeweza kujua jinsi ya kuandika maana hajawahi kuiona. Vyovyote iwavyo majina yameandikwa /yanaandikwa mbinguni.Chukulia mfano nchi za wenzetu zilizoendelea wanajua watu wote katika nchi zao,je kama wao wameweza kwa Mungu kitashindikana nini wakati ujuzi na maarifa vyote vinatoka kwakwe?

Siku hiyo ya mwisho ukisema mimi sikutenda dhambi fulani ,inaletwa skrini inawashwa unaonyeshwa yale yote uliyokuwa ukiyafanya ndipo aibu ya kila mtu ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha UZIMA itaonekana kwa watu wote. (Hii nimeandika kwa Ufunuo wa sasa hivi, kwahiyo baadaye itatumiwa kama Kumbukumbu kwa kizazi hiki na kijacho kwasababu nyakati hizi sote tunazijua tv).

Maandiko yanasema hivi,"Kwa maneno ya vinywa vyenu mtahesabiwa haki na kwa maneno ya vinywa vyenu mtahukumiwa"
Mfano mwingine miaka ijayo kuna kipindi watu watakuwa wakiendesha baiskeli angani kama ilivyo kwa magari yanayopaa. Sasa utakuta kutokana na kukua kwa teknolojia utakuta haitaitwa baiskeli inayopaa bali itaitwa kwa jina lingine, na wao watasema watu wa zamani waliona katika maono kwamba ni baiskeli inayopaa.

Kwahiyo vitu kama hivi katika ulimwengu wa roho vipo vya baadaye ambavyo kwa nyakati kama hizi vinakuwa na majina ya kipindi cha sasa hivi lakini mbeleni hubadilika kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Vitu kama hivi katika ulimwengu wa roho vipo vingi sana vitakuja kuonekana baadaye kwa majina mapya watu wasio na mafunuo watasema ni vipya kabisa.
 
Back
Top Bottom