Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Aidama

Member
Apr 10, 2023
50
304
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.

Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.

Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.

Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.

Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.

Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.

Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.

Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.

Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.

Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.

Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.

Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.

Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?

Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.

Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.

Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
 
Nakushauri angaliaangalia ratiba za saili mbalimbali UTUMISHI, yale matangazo wanayoandika kua 'Hakikisha unakuja umevaa barakao',kariri tarehe za saili za aina hizo, jumua barakoa hata za dili au kopa kwa bei ndogo, nenda kawauzie wasailiwa.Uza kwa 1000 kila piece moja, kwenye boksi moja zinakua pieces 50 au 25, unaweza ukabahatika ukauza boksi 5 au sita,ukapata mtaji. Nilimshauri mtu hivyo, akabeba boksi 8,na kila boksi alinunua kwa 3000, zilikua za dili,siku hizi zipo tu kwenye mataasisi zimekaa tu, corona hamna,alipata laki nne ya harakaharaka ,akapata mtaji,kwasababu siku ya usaili wa TAKUKURU, Dodoma, walikua wawili tu waliokua wanauza, hadi zilimuishia, angepata hata milioni na hakukaa hata zaidi ya masaa mawili.

Fanya hivyo. Siku hizi saili zinafanyika kikanda, chunguliachungulia sana kwenye tovuti ya UTUMISHI.

Pole Sana, ngoja waje wadau wengine wakupe mawazo mengine.
 
Hello,

They say "If you are brave enough to let go, life will bless you with new hello".

When they close one door for you believe many will be opened for you

I know it's hard for you but believe that things will get better for believing is itself a miracle.

all gonna be okay, at the end all gonna be okay.
 
Back
Top Bottom