Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,638
113,868
Wanabodi,

Hii ni makala kwenye gazeti la Mwananchi la Jumatano.

20240403_181933.jpg

Kwa wasomaji wapya, naendelea kutoa darasa kuhusu kuijua katiba ya JMT ya mwaka 1977, kwa jicho la Mtunga Katiba, kwa mimi kuvaa viatu vya mtunga katiba alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani.

Wiki iliyopita nilizungumzia jinsi jinsi mihimili mitatu ya serikali, Bunge na Mahakama inavyopaswa kuheshimiana, lakini pia kusimamiana, na kudhibitiana, (The doctrine of Separation of Powers Checks and Balance) na kuleza jinsi Bunge la awamu zilizopita lilivyotunga kipengele batili, kinyume cha katiba, na kuuchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977.

Japo Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa
hukumu ya kutengua, ubatili huo, lakini katika kuheshimiana kwa mihimili hii, Mahakama ya Rufaa ikaurejesha ubatili kwenye Mhimili wa Bunge, ili Bunge liloutenda ubatili huo ndio litengue, lakini Bunge letu Tukufu, limekula kobisi, (yaani limekaa kimya na kujikausha), hiyo ubatili huo bado imo ndani ya katiba yetu mpaka sasa!.

Hiki kilichofanywa na Mahakama ya Rufaa ni kinyume cha kanuni za natural justice, kanuni ya lugha ya Kilatini iitwayo "Nemo judex in causa sua", which means that no one should be a judge in his own cause. Bunge letu Tukufu limefanya ubatili wa kuchomekea kiubatili kifungu batili ndani ya katiba yetu, Mahakama Kuu ya Tanzania ikabatilisha kwa tamko tuu, badala ya kubatilisha, kisha Mahakama ya Rufani ukuurudisha ubatili huo kwenye mhimili wa Bunge ndio liuondoe.

Yaani umeibiwa gari lako, ukamkamata mwizi wako, na ushahidi wa gari lako, ukamfikisha kwa Pilato, Pilato akatoa hukumu, kwa vile mwizi amekutwa na gari, na aliiba kwa kuliendesha mwenyewe, mwizi huyo arejeshewe gari aliloliiba na alirejeshe kwa mwenyewe pale alipoliiba!.

Japo Tanzania ina mihimili mitatu inayojitegemea (independent), ya Serikali, Bunge na Mahakama, na wakuu wa mihimili hii ni Rais wa JMT, ni mkuu wa mhimili wa serikali, Spika wa Bunge ni mkuu wa mhimili wa Bunge, na Jaji Mkuu ni mkuu wa mhimili wa mahakama, lakini kwa mfumo wa katiba yetu, Rais wa JMT ndie mkuu kificho wa mihimili yote mitatu, Rais wa JMT ndie Mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu, wa majeshi ya ulinzi na usalama, yaani mkuu wa dola.

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Mahakama, kwa rais kumteua mkuu wa mhimili wa Mahakama, yaani, Jaji Mkuu, majaji na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, na mahakama inaweza kutoa adhabu yoyote, lakini rais wa JMT amepewa mamlaka ya kusamehe wafungwa wowote, na mahakama ikitoa adhabu kubwa kuliko zote, capital punishment, yaani adhabu ya kifo, adhabu hiyo haitekelezwi mpaka kwanza rais wa JMT, asaini death warrant yaani hati ya kifo, hivyo Rais ndio kila kitu kwenye mhimili wa Mahakama!.

Tukija kwenye mhimili wa Bunge, rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa kuliunda, kulivunja, kuteua mtenjaji mkuu wa Bunge, na Katibu wa Bunge, na katika utungaji wa sheria, Bunge linatunga tuu sheria lakini sheria hizo haziwi sheria mpaka kwanza rais wa JMT, aridhie na kusaini ridhio hilo, accent, ndipo sheria inakuwa sheria, hivyo na kwenye mhimili wa Bunge, rais pia ndie kila kitu!.

Rais wa Tanzania, tukiisha mchagua, anaapishwa kwa kula kiapo cha kuilinda na kuiteteta katiba ya JMT, na kumuomba “Mungu nisaidie”, ili rais wetu aweze kutekeleza majukumu yake ya urais, katiba yetu imempa rais wetu kinga ya kutokushitakiwa kwa kosa lolote atakalo litenda katika kutekeleza majukumu yake ya urais, wakati akiwa madarakani, na kinga hiyo inaendelea hata baada ya kustaafu.

Hili la Kinga ya Rais kutokushitakiwa mahakamani, naomba tulipigie mstari, kinga ya rais kutokushitakiwa mahakamani, inahusu kosa lolote ambalo rais wa JMT, atalitenda katika kutekeleza majukumu yake ya kuuraisi tuu, hii maana yake, rais wa JMT, anaweza kushitakiwa mahakamani kwa kesi ya madai, au akitenda kosa jingine lolote ambalo sio la utekelezaji wa makumu yake ya urais, kwasababu rais pia ni binadamu, anaweza kutenda makosa ya kibinadamu, hivyo anaweza kushitakiwa kwa kesi ya madai, ila ni baada ya kumaliza kipindi chake cha urais.

Hivyo japo katiba yetu imempa kinga rais wa JMT, kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayo yatenda, hii maana yake ni, rais wa Tanzania anaruhusiwa kutenda makosa ndio maana amewekewa kinga ya kutokushitakiwa.

Lakini katika kuonyesha ukuu wa katiba, uitwao constitutional supremacy, katiba ndio iko juu ya kila kitu, hata rais wa JMT japo yuko juu ya serikali, Bunge na Mahakama lakini yuko chini ya katiba, hii maana yake katiba ya JMT ndio iko juu ya kila kitu, hakuna aliye juu ya katiba, hata rais wa JMT hayuko juu ya katiba, lakini kuliisha jitokeza mazingira fulani fulani huko nyuma, rais wa JMT akajiinua juu ya katiba na kuikanyaga katiba, na hakuna yeyote aliyekohoa!.

Japo nimeeleza kule juu kuwa Rais wa JMT, anaruhusiwa kufanya makosa mengine yotote lakini rais wa JMT haruhusiwi kufanya kosa lolote la kukiuka katiba, kwasababu katiba iko juu yake. Hivyo katika kuhakikisha Ukuu wa katiba, mtunga katiba ameweka Ibara ya 56A, ili rais wa JMT asikiuke katiba, na iwapo rais atakiuka katiba, anaweza kushitakiwa na Bunge na kuondolewa madarakani.

Kitendo cha serikali kupeleka Bungeni, muswada wenye kipengele batili, kinachokwenda kinyume cha katiba ya JMT, huu pia ni ukiukwaji wa katiba ya JMT. Kitendo cha Bunge kupokea muswada wenye kipengele batili kinyume cha katiba, na kukitunga kuwa sheria, pia huu ni ukiukwaji wa katiba ya JMT, na kitendo cha Rais wa JMT, ila mamlaka pekee yenye kuweza kutamka sheria fulani ni batili, au kipengele fulani cha katiba ni batili na linakwenda kinyume cha katiba, sio mimi, wala sio mtu mwingine yeyote bali ni Mahakama Kuu ya JMT pekee.

Wiki ijayo nitaendelea kwa kukuletea hiyo sheria batili ni ipi, na ubatili wake ni upi, jinsi Mahakama Kuu ya Tanzania ilivyoitengua hiyo, sheria batili na nini kilitokea.

Paskali
 
Rais ndiye mwenyekiti wa chama tawala ambaye pia husimamia mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya uspika. Spika akienda kinyume na matakwa ya mwenyekiti anaweza kupokwa uanachama na akapoteza ubunge na uspika.

Rais huyu huyu ndiye huteua jina la waziri mkuu kisha kuthibitishwa na bunge. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za serikali bungeni.

Muswada wowote lazima upite kwenye Kamati ya bunge uangaliiwe na kuridhiwa na serikali (kupitia waziri mkuu na mwanasheria wa serikali) ndipo upate kibali na utengewe muda na spika wa kujadiliwa bungeni .

Kwa mazingira hayo, rais tayari amepoka nguvu na mamlaka ya ibara ya 56A. Hakuna namna rais anaweza kuwajibishwa na bunge.
 
Back
Top Bottom