COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,599
- 3,647
Kwanza rekebisha.Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali na alama za kuuliza nimeziweka, maana watu tusije itwa mahali kuhojiwa kuwa tumelidhalilisha Bunge.
Swali lenyewe ni hili,
Jee Wajua Bunge Linaweza Kutoa Azimio Batili?. CAG yuko Kikatiba, Jee Bunge Lina Uwezo Kutopokea Ripoti ya CAG?.
Tuliisha zungumza sana kuhusu kuhusu kitu kinachoitwa "The Principle of Separation of Powers, Checks and Balances" tukasema kanuni hii hutumika na mihimili hii mitatu ya dola kwa lengo kila mhimili kuwa a watchdogs wa mihimili mingine isijiinue kupita mamlaka yake.
Jee Azimio hili la Bunge kuamua halitafanya kazi na CAG ni Azimio Batili?, kwa sababu Ofisi ya CAG ipo kwa mujibu wa katiba, na Ripoti ya CAG inawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa katiba, Jee Bunge lina uwezo huo wa kuamua kutofanya kazi na CAG, wakati Bunge sio Mamlaka ya nidhamu ya CAG, kama CAG amelikosea Bunge, then Bunge ama limshitaki CAG mahakamani au limshitaki CAG kwa mamlaka yake ya nidhamu, hiyo mamlaka ndio iamue kumchukulia CAG hatua za kinidhamu tena kwa mujibu wa Katiba lakini sio kwa Bunge kutoa Azimio Batili la altimatum kuilazimisha serikali kumuondoa CAG.
Bunge ni tukufu haliwezi kukosea, lakini linaongozwa na watu hivyo watu hawa wanaweza kukosea na ndio maana wakikosea, wanaweza kuondolewa.
Serikali inaongozwa na rais na pale Ikulu ni mahali patakatifu hivyo rais wetu anapaswa kuwa Mtakatifu ambaye hawezi kukosea na ndio maana rais hawezi kushitakiwa, ana kinga ya kutokushitakiwa kutokana na utakatifu huu, lakini rais pia ni binaadamu anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu na anaweza asiwe Mtakatifu, ndio maana akikosea anaweza kushitakiwa na Bunge na akikutwa na hatia anaondolewa.
Ofisi ya CAG ni vivyo hivyo, ipo pale kwa mujibu wa katiba na CAG yupo kikatiba, Bunge haliwezi kujiamulia kuwa halifanyi kazi na CAG, bali kwa vile ofisi ya CAG nayo inaongozwa na mtu anayeitwa CAG, mtu huyu anaweza kukosea, akikosea anashitakiwa na akithibitishwa amekosea, anaondolewa.
Rais anapokea ripoti ya CAG kwa mujibu wa katiba, na baada ya rais kupokea ripoti hiyo bado inakuwa ni closed document.
CAG anatakiwa kuiwasilisha ripoti hiyo Bungeni within 7 days za mwanzo za kikao cha Bunge, baada ya rais kupokea ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ikiisha wasilishwa tuu Bungeni, from that moment, Ripoti hiyo ni Public document, CAG anakuwa amemaliza kazi yake .
Sasa Bunge lijadili au lisijadili, it's up to Bunge na hapa ndipo kwenye udhaifu wenyewe wa Bunge letu.
Bunge halina mamlaka kukataa ripoti ya CAG bali lina uhuru lisiijadili.
Hivyo kama CAG, ana makosa dawa sio kwa Bunge kuamua kutofanya kazi na CAG, kwa kutoa Azimio batili, bali kumshitaki, GAG aondolewe, maisha yaendelee.
Naomba msaada kwa wabobezi wa sheria, taratibu na kanuni, watufafanulie jee Bunge letu tukufu, lina uwezo huo?.
Paskali
Bunge si takatifu.
Ikulu si patakatifu.
Mungu alipatamka mahali hapa ni patakatifu shehemu moja tu dunia enzi za nabii Mussa.
Hayo maeneo mengine tunajitengenezea utakatifu sisi wenyewe kitu ambacho siyo sahihi
Sent using Jamii Forums mobile app