Je, unaweza kuajiri CEO na Wakurugenzi toka mashirika haya?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,186
20,659
DODOMA: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amefanya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2022-23 na kuorodhesha mashirika 99 ambayo yanadaiwa zaidi ya Sh trilioni 3.49.

Je, kama Mtu ni mkurugenzi kwenye hili shirika, amekaa hapo miaka 10 na halijawahi kupata faida, anapewa ruzuku na pia anapata hela na mabilioni kila siku ziara za ulaya kwenda kujifunza, unaweza kumuajiri huyu FAILURE?​

Mashirika kumi yenye madeni na hasara kubwa ni haya yafuatayo;
1. Shirika la Reli Tanzania Sh trilioni 1.07
2. Shirika la Umeme Tanzania Sh bilioni 677.8
3. Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya Sh bilioni 335.8
4. Shirika la Mawasiliano Tanzania Sh bilioni 319.8
5. Bohari Kuu ya Dawa Sh bilioni 197.4
6. Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania Sh bilioni 152.7
7. Mfuko wa Maendeleo ya Zao la Pamba Sh bilioni 78.3
8. Hospitali ya Taifa Muhimbili Sh bilioni 69.9
9. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam Sh bilioni 66.2.
10. Kampuni ya STAMIGOLD Sh bilioni 40.8
 
Back
Top Bottom