Je, UKAWA tutakwepa mtego wa kuwa wasindikizaji wa harusi?

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
Nianze kwa salamu: UKAWA, TUMAINI LETU.
Ninaunga mkono juhudi za UKAWA za kuleta mageuzi ya kweli (ukombozi wa pili) katika taifa hili tajiri sana lakini asilimia 90 ya wananchi wake mafukara wa kutupa!. UKAWA tuliweza na kufanikiwa kugundua katika wakati muafaka na kukwepa mtego wa kuwa wasindikizaji katika kujadili na kupitisha katiba inayopendekezwa katika BMK. Mhe Dr. Profesa JK alikwishaandaa rasimu ya katiba yake. Tume ya Warioba ilikuwa ni geresha tu. BMK kwake ilikuwa lipigie mhuri tu katiba anayoijua yeye. Tulifanikiwa kuukimbia huu mtego wa kuwa sehemu ya uchakajuaji. Sasa je tutaweza kukwepa huu mtego wa kuwa wasindikizaji wa harusi ya profesa Kikwete?

Kwa kuanzia hotuba yake ya uzinduzi wa BMK hadi leo hii katika kauli zake, mipasho yake, majigambo yake ni dhahiri alikwishaamua upande, na kwa hakika inadhihirisha kuwa alikwishaandaa rasimu yake ya katiba. Kwa maneno mengine, hii ni katiba yake. Na imeishapita, inasubiri tu sherehe.
Kwa mfumo tulio nao wa utawala (ambapo Rais ni kama mungu-mtu) ikiwa ni pamoja na Tume yetu ya uchaguzi (inayotumikia huyo Mungu-mtu) HAKUNA namna yo yote ile unaweza kumshinda Mungu-mtu kwa njia ya kura, hasa kura ya maoni. Neno ‘kura' linatumika tu kama tambala la demokrasia lililofunika udikteta wa hatari kuliko udikteta wa Idd Amin, Museveni au Mugabe. Sasa, je UKAWA kwa kuhamasisha wananchi waende kwenye kasha la kura ya maoni kupiga kura ya HAPANA, si sawa na kuingia kwenye mtego wa kusindikiza harusi ya profesa. Wananchi wapige kura au wasipige – itatangazwa kuwa kura ya NDIYO imepata ushindi wa kishindo na kama kawaida waTZ tutacheza kigodoro kusherehekea.

Ni hoja ya kutafakari. Sina jibu.
 
Back
Top Bottom