Je, nitumie dili niliyopewa ukweni hata kama wife ananitambia?

lelulelu

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
423
378
Wakuu mimi ni mume ambaye tumezaa mtoto mmoja na mke wangu ndoa yetu ina miaka zaidi ya mi4 mpaka sasa.

Ukweni kwangu yaani familia ya wife imekuwa ikinisaidia saana ila tatizo wife sasa huwa anatamba sana kwamba mimi nasaidiwa na familia yake.

Wife amekuwa akiyasema hayo hata wakija marafiki zangu na ndugu zangu nyumbani basi anawaambia hivyo.

Utasikia lile shamba kapewa na baba yangu kasaidiwa sana.

Juzi juzi walinipa connection ya eneo zuri la biashara na fremu pale Kariakoo kitu bacho bila wao nisingeweza kupata, ila wife yatari keshamwambia mdogo wangu wa kike kwamba nimesaidiwa kitu fulani.

Binafsi huwa sipendi hii tabia.

Sasa hapa karibuni kuna fursa ya kwenda kusoma Uturuki chuo fulani ambacho wanakufund na unalipwa ukienda kusoma, na hiyo fursa imetoka ukweni.

Je, niikubali hii fursa wakuu ama niikatae kutokana na wife na kujigamba kwamba wananisaidia sana?
 
Sijui wengine huwa mnaoaje na hamna akili,

Chukua karatasi, andika hasara na faida za kwenda na kutokwenda, kisha weigh down utajua,
Unataka sisi tukuamulie, utakuwa na sisi kwenye future yako ? Utakuwa na sisi wakati mke anajigamba ?

Halafu kwann unashindwa kumsimamia mke wako? Ni mwanaume wa dar au
 
hata ukitaka iwe siri mkeo huko ni kwao atajua tu na uatasambaziwa mnoo kazi unayo mahi huyo mke ni kama redio mbao haihimili mikiki mke gan hana kaba friji compressor mbovu haigandishi hata chembe? sjawah kuona mwanaume anahofia mke halaf hao wakwezo mbona wanakusaidia san ukute wanataka wakurithishe uchawi!!
 
Lelulelu,
Huyo mkeo ndiyo anafaa, kongole kwa kupata mke bora anakuaminia mtaji hutautapanya na ndiyo maana anatamba na hiyo siyo kitu kibaya.

Jamii za wahindi, waarabu, wayahudi, wangazija n.k familia zao zinaendelea kiuchumi kwa kusaidiana namna hiyo

Achana na mambo ya waswahili, wakwe wamekuamini kuwa unaweza na hivyo wameamua ku-ku'boost' kiuchumi nawe usisahau kusaidia ukiona mmoja wa wanafamilia au ukoo ana dalili za kufanya vizuri akipewa mtaji.

Usiwaangushe familia kwa kukuamini unaweza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom