Je, nifanye ubatizo na ubarikio kanisani kwangu (Anglican ) au huko kanisani kwao?

johnsonmgaya

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,818
3,727
Habari za asubuhi wapendwa,

Poleni na mvua na majukumu ya leo
Natumai mpo salama kabisa,
Poleni kwa watakaosombwa na maji siku ya leo.

Naomba nilete mada mezani kama ifuatavyo:

Mimi ni muanglikana siwezi sema ni safi moja kwa moja maana siendi kanisani mara kwa mara ila naamini katika Anglican na namjua Mungu kiasi fulani, mke wangu yeye ni mlokole (nimekosa jina la dhehebu ila ni haya makanisa yenye majina majina)

Tumejikuta tupo katika ugomvi (japo si mkubwa) kuhusu dini zetu, baada tu ya kupata binti, kwa sasa huyo mtoto ana miaka 2 na miezi 4 hadi leo nisiwe muongo hatujashukuru wala kumbatiza huyo mtoto kutokana na mvutano uliopo tangu akiwa mchanga.

Mara ya kwanza alisema wao hawabatizi mtoto akiwa na umri mdogo (hajitambui)
Ila kanisani kwangu tunaruhusiwa tena ndo vizuri mtoto akimjua Mungu akiwa hivyo.
hapa kati nikapata ibilisi basi sijaenda tena kanisani kwa kipindi hicho chote labda siku za sikukuu tu. Maisha yakaendelea

Sasa juzi kati mama mtu kapata shoga mlokole (pure) mwenyewe anamuita au tuseme aliyeokoka, wamebebana wakaoneshana kanisa hilo la huyo bibie, mazoea yakaendelea wanatembeleana kila siku tatizo likaanzia hapa, yule anakuja saa moja saa mbili usiku kuondoka saa 4, mwanzo nikajua ni dharura kwa siku hiyo, lakini ile tabia ikaendelea kila siku akijisikia anakuja hadi mda huo, kiukweli kama binadamu mwingine hii hali ikawa inanikera sana maana umetoka kazini unatoka kuoga tu au upo bafuni unasikia hodi sebuleni ukizingatia muda huo kuna habari na vitu vingine.
Anyway hii si issue sana iliyonileta hapa leo, lakini ndo walokole mnavyoelekezwa jinsi ya kuwaokoa watu?

TATIZO LIPO HAPA:

Jana amekuja nyumbani (mda huo) kanikuta nipo zangu sebuleni, wakaanza kunong'onezana sijui kuhusu kubariki mtoto, (walikuwa washaambizana tangu Jumapili walivyokutana kanisani) hivyo hapo alikuwa anampa feedback ya nini kinahitajika, kwakuwa nilikuwa pale akaone anishirikishe na mimi (mambo ya kifedha) kuhusu vinavyohitajika.

Wanahitaji hela ya kadi ya ubarikio 3000/- tu, pia hela ya sadaka kulingana na thamani ya mtoto (hapa ndipo ubongo ulipocheza) anasema kama mwanao anathamani ya elfu mbili sawa toa japo Mungu anakuona kama anathamani ya mbuzi wawili toa Mungu anakuona, Hhhahahha nikajikuta namuangalia binti yangu nikacheka moyoni nikajisemea yale yale washaanzaa hawa watu, maana hakuna mtoto anayelinganishwa na fedha je hawa wanahitaji nini au shilingi ngapi?

So nilichomjibu mimi ni kitu kimoja, hili suala ni la kifamilia hivyo tunapaswa lijadiliwe majibu atakupa mwenzio kesho, kama unavyojua hii issue yenu ndo kwanza nasikia sasahivi japo nilishamwambia hili mda mrefu tu, yeye mwenyewe alisema mda bado so nahitaji niongee nae atakujibu.

Lakini yeye akawa kama analazimisha nikubaliane nalo hapo hapo, kajisomesha biblia hapo wee, mara kumpokea Yesu halihitaji majadiliano na mtu we ukiamua tu moyoni mwako fanya, au hauamini katika Yesu? Au ninavyokuja hapa nakukera maana haupo kabisa na sisi, nikacheka tena kama kawaida yangu, nikamjibu Aunt mbona kitu kidogo tu hiki unataka kulikuza? Umeleta jambo kama baba kichwa cha familia huwa sitoi majibu bila kuangalia effect zake so kuwa na amani kesho si mbali utapata majibu na pia shughuli umesema ni tarehe 29 leo ni tarehe 3 huoni kama kuna mda mrefu wa kujipanga? Then sisi pia tunafamilia mjukuu wao ndo huyo huyo lazima hili suala liwafikie wazazi wa pande zote mbili ili walibariki basi wakabeba hapo wakasindikizana.

Sasa hapa swali langu linauliza hivi:

JE KUNA MNANISHAURI NIFANYE UBATIZO NA UBARIKIO KANISANI KWANGU (ANGLICAN ) AU HUKO KANISANI KWAO?

Serious nahitaji hili lifanyike kama nilivyoelezea hapo juu ila siamini katima makanisa hayo ya ulokole huo ndo ukweli wangu.
 
Duh pole, naona hujasimama katika nafasi yako kama mwanaume na kama kichwa cha familia, umeacha nafasi ambayo itakukosti sana. Ngoja nikuitie wanaume wenzio wakusaidie Asprin BAK njooni mumsaidie mwenzenu jamani.

Jina la Mungu unayemwamini huanza kwa herufi kubwa.
 
Usiiyumbishe meli yako kwa kelele za baharia.

Mpe ruhusa afanye apendavyo bali wewe usijihusishe shughuli nzima kwa lolote.

Mpige marufuku huyo shoga yake kuja kwako maana si mwalimu mzuri.

Wapende familia yako kwa mali zako kisiwapungukie kitu.

Rudi kanisani kila jumapili kama enzi zilizopita.

Epuka tena kataa kata kata mijadala ya kiimani.

Muombe MUNGU akutendee muujiza maana mkeo hajui kuwa wewe ndio kichwa cha nyumba.

NIISHIE HAPA KWA SASA.
 
Sisi waafrica hatujitambui tu. dini za watu, utamaduni wa watu tumevifanya kuwa vyakwetu kiasi cha kuathiri maisha yetu ya kawaida. kwani kubatizwa au kutobatizwa kuna athari gani? mimi hapa sikuwahi kubatizwa wala sibatizi mtu. mimi naamini katika imani za wazee wetu wa hapo nyuma. si mkristo wala muislamu na sipati athari zozote. na nina matumaini kuwa nitakuwa salama daima. naamini mungu yupo na nimeyagawa matendo ya wanadamu katika kundi la haki na la dhambi.
najitahidi nisitende matendo yanayowaudhi wengine na najitahidi kuwahurumia na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wangu. waafrica waliamini hivyo tangu zamani. maadili katika jamii yalikuwa makubwa sana na walisaidiana kwa kila hali.
Mungu aiamshe Africa kwakweli
 
Hata sisi, Wasabato tunaamini(kulingana na kielelezo cha Yesu Kubariki watoto wadogo) kuwa watoto wadogo hawabatizwi(maana ubatizo ni kwao waaminio) bali huwekewa mikono. Tofauti na walokole sisi hatuamini hiyo habari ya 'kumthaminisha mtoto' wala gharama zozote,bali ni mzazi mwenyewe kutoa sadaka ya shukrani akiona ni vema.

Ushauri; Usiamue wewe kama wewe,wala wewe na mkeo bali AMUENI KWA MUJIBU WA MAANDIKO FULL STOP
 
Duh pole sana ila bado tatizo lipo kwako ndugu.. We mwanajme mwenzangu labda unaweza ona upo sahihi na mwanamke nae anaona yupo sahihi halafu wote kumbe hampo sahihi,(nielewe sana)

Mlioana kwa dhehebu gan au mnakaa kinyumba tu??

Unaposema mke,mke haswa mara nying hua anamfuata mwanaume,japo sio lazma,ndio maana wengine wanabadilishaga mpka ukoo wa kwao anaufuata wa kwako wewe mwanaume japo sio lazma vile vile,, mtoto aende kwa nan kama nyie wenyewe hampo sawa? We utataka aende kwako nae atataka aje kwake so mtoto anakuaje??

Hakuna biblia popote iliyosema au inaposema mtoto anabatizwa sababu ili ubatizwe lazma upitie mambo haya
UFUNDISHWE
UKIRI
UMKUBALI YESU AWE
MWOKOZ WA MAISHA YAKO
THEN UBATIZWE


je mtoto mdogo anaweza yte hayo jibu ni hapana so hapo kakushinda tayari..
Swali la msingi mtoto anakua ktk iman ipi? Madhara yake hutayaona sasa hivi ila baadae baada ya mtoto kukua na yy akaamua kufuta anayoiamin icyo yako wale ya mkeo.

Ushauri wngu kaeni chini,muongee vizur,mshauriane na mungu awe kati yenu mnapoliongelea suala hili maana shetana ndio anape da sehem km hizo kudhoofisha kila idara.
 
Duh pole, naona hujasimama katika nafasi yako kama mwanaume na kama kichwa cha familia, umeacha nafasi ambayo itakukosti sana. Ngoja nikuitie wanaume wenzio wakusaidie Asprin BAK njooni mumsaidie mwenzenu jamani.

Jina la Mungu unayemwamini huanza kwa herufi kubwa.
Asante mkuu lakini hata ww unanafasi ya kunisaidia kama mistake nimekiri nilifanya tangu mwanzo so now sipo tayari nifanye tena
 
Usiiyumbishe meli yako kwa kelele za baharia.

Mpe ruhusa afanye apendavyo bali wewe usijihusishe shughuli nzima kwa lolote.

Mpige marufuku huyo shoga yake kuja kwako maana si mwalimu mzuri.

Wapende familia yako kwa mali zako kisiwapungukie kitu.

Rudi kanisani kila jumapili kama enzi zilizopita.

Epuka tena kataa kata kata mijadala ya kiimani.

Muombe MUNGU akutendee muujiza maana mkeo hajui kuwa wewe ndio kichwa cha nyumba.

NIISHIE HAPA KWA SASA.
asante mkuu hata mimi nililipanga hili, sitojihusisha kwa lolote ila sitoruhusu abatizwe huko, nina mpango pasaka hii nifanye kwangu
 
Hata sisi, Wasabato tunaamini(kulingana na kielelezo cha Yesu Kubariki watoto wadogo) kuwa watoto wadogo hawabatizwi(maana ubatizo ni kwao waaminio) bali huwekewa mikono. Tofauti na walokole sisi hatuamini hiyo habari ya 'kumthaminisha mtoto' wala gharama zozote,bali ni mzazi mwenyewe kutoa sadaka ya shukrani akiona ni vema.

Ushauri; Usiamue wewe kama wewe,wala wewe na mkeo bali AMUENI KWA MUJIBU WA MAANDIKO FULL STOP
Asante
 
Back
Top Bottom