Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,716
- 29,947
Ndugu zangu. Hata sasa tumeshuhudia anguko la mwanadamu katika nyakati hizi za Neema ya Mungu ya Wokovu kupitia damu ya Thamani ya Yesu Kristo...
Manabii wa uongo walikuwepo tangu nyakati za Torati
Yeremia 14
4. Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
14. Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao.
15. Basi, kwa hiyo BWANA asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, lakini husema, Upanga na njaa havitaingia katika nchi hii; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa.
Swali ninaweka hapa, je yampasa mwanaume anaposimama kuhubiri ama kusali hali amefunika kichwa chake? Mtume Paulo ametuasa katika
1 Wakorintho 11

.
Hapo awali makuhani wa Wayahudi walikuwa wanafunika vichwa vyao, lakini tangu Bwana Yesu aliposema IMEKWISHA na pazia la Hekalu kupasuka katikati (linalotenganisha Patakatifu pa Patakatifu), ameleta kwetu Agano Jipya ambalo ndiyo kanuni za kuishi kwa Imani na Kumtumainia Mungu. Hivyo Maandiko ya Agano Jipya yamebeba hatima ya Imani yetu kwa Mungu na si vinginevyo.
Tunashuhudia makaasisi wa makanisa mengi wakisimama madhabahuni wakideliver Neno na kuongoza Ibada wakiwa wamefunika vichwa vyao. Je hayo ni makufuru dhidi ya Mungu au ni taratibu halali?
Tuelimishane bila kudhalilisha imani na dini za watu.