passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,618
- 3,313
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.
Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.
Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo👇
Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka
Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.
Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,
Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.
Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.
(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake
Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?
Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.
Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.
( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)
Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.
HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.
Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.
Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?
Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.