Je, ni kweli Ada ya kumuona Daktari (Consultation Fees) inavutia Daktari kwenda kufanya kazi katika Hospitali fulani katika eneo fulani?

Dx and Rx

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,304
3,086
Katika Hospital za Rufaa za Mikoa na Hospital za Ngazi ya Taifa na Kanda, Madaktari wana maslahi tofauti kimishahara, Daktari wa Hospital ya Ngazi ya Taifa na Kanda anamzidi mshahara Daktari wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wakiwa na elimu sawa.

Kuwaona hawa madaktari wakati wa kuanza matibabu lazima ulipie hela (Consultation Fees) kwa cash au kama una Bima, italipwa na Bima, hii hela haingii mfukoni mwa Daktari utakayemuona, yaani sio hela ya Daktari badala yake ni Mapato ya Hospital. Mara nyingi wananchi ambao hawajui kuhusu hii Consultation fees huwa wanafikiri anaichukua Daktari, Kipindi cha nyuma iliwahi kuzuka mjadala wa hii hela kwa wale wanaolipa cash ambapo wananchi walidai kuwa wanatozwa hela kubwa kumuona Daktari na kusema Madaktari wanajineemesha, kumbe sio kweli.

Sasa jana imesomwa Hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2024/2025 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu. Katika hotuba yake kaelezea mambo mbalimbali ikiwemo Mambo makubwa yaliyofanyiwa maboresho katika Kitita cha Mafao cha NHIF cha mwaka 2023. Katika kufafanunua hayo mambo ameleza kama ifuatavyo kwenye kipengele cha V kilichopo kwenye ukurasa wa 249, “Kuweka usawa wa ada ya usajili na kumuona madaktari wenye elimu na taaluma zinazofanana kwa wanufaika wa NHIF. Mathalani, kwa kitita kipya Daktari Bingwa katika ngazi ya Rufaa Mkoa ada imeongezeka kutoka Shilingi 15,000 hadi Shilingi 25,000 ambapo ni sawa na ada ya kumuona Daktari aliyeko ngazi ya Kanda na Taifa. Hatua hii itavutia madaktari bingwa kufanya kazi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa hususan ya pembezoni
IMG.jpg

Hapo anasema kuwa kitita kimeboreshwa kwa kuweka usawa wa ada za kumuona Daktari katika ngazi ya Taifa, Kanda na Rufaa za Mikoa kwa lengo la kuwavutia Madaktari wakafanye kazi kwenye Hospital za Mikoa hususan za Pembezoni mwa Nchi, kivipi hii ada ya kumuona Daktari ambayo si mali ya Daktari bali ni mali ya Hospital itamvutia Daktari kufanya kazi kwenye hiyo Hospital? Hawa Madaktari wanaotakiwa kuvutiwa na ada za kuwaona wanamishahara tofauti na maslahi mengine ya ndani yanatofautiana pia. Madaktari njooni mnifafanulie zaidi hii hoja ili niielewe maana sijaielewa.
 
Ile consultation fee kuna % inaingia kwa daktari moja kwa moja, inategemea na ngazi ya Elimu ya daktari husika.
 
Back
Top Bottom