Je, nchi zinaanza kukimbilia dhahabu kama pesa? Tanzania tuna akiba kiasi gani cha dhahabu?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,890
Habarini.

Habari za nchi kukimbilia matumizi ya dhahabu zimekuwa nyingi sana siku za karibuni. Ghana baada ya kuzidiwa na madeni na kuishiwa akiba ya fedha za kigeni, imeamua kutumia dhahabu kununua mafuta. Kuanzia mwezi huu makampuni ya kuchimba dhahabu yatatakiwa kuiuzia benki kuu ya Ghana asilimia ishirini hivi ya dhahabu zao. Zimbabwe baada ya kuhangaika na inflation kwa miaka mingi, hatimaye wameprint sarafu ya dhahabu ya thamani ya 900usd.

Kihistoria, na hata sasa dhahabu ndiyo pesa pekee ya kueleweka. katika vitu vyote, walichagua dhdhabu sababu ni adimu na haiharibiki miaka na miaka. ikaonekna ni kitunza thamani bora kuliko vyote. Dhahabu imetumika kuanzia miaka mia tano kabla ya Yesu hadi mwaka 1971 pale USA walipoacha kuihusianisha na dola. karibu miaka 2500 imetumika. Na bado inatumika nyuma ya pazia. US wenyewe wana akiba ya tani elfu nane. Sababu ni kuwa haya makaratasi yanayoitwa pesa yakikosa thamani mbele ya watu, kimbilio pekee ni dhahabu. Ndicho walichofanya Zimbabwe. Ujerumani wana tani kama elfu tatu. IMF wanatani elfu kadhaa, na China pia wanazo na wanaendelea kununua. Na dhahabu ni tishio kubwa sana kwa hizi pesa za kihuni za makaratasi, Gaddafi alitaka kuanzisha Dinari ya dhahabu, inasemekana ndiyo chanzo cha kumkuta yaliyomkuta.

Mwaka 2019 JPM aliiamuru benki kuu kuanzisha hazina ya dhahabu. Alisema:

""We should start buying gold, the central bank must invest in this. We must have our reserves in dollars but also our reserves in gold, because gold is money,"

Tutegemee nchi zaidi zaidi kukimbilia matumizi ya dhahabu? Ni akiba kiasi gani ya dhahabu nchi yetu inayo?
 
Back
Top Bottom