Mtafiti Pro
Member
- May 5, 2018
- 12
- 6
Habari wana taaluma.Mimi nilihitimu kidato cha 4 mwaka 2010 masomo ya biashara.
Masomo yote nilipata D isipokuwa Book-keeping 'A' , Mathematics 'B' na History 'C'.
Niliendelea advance masomo ya biashara pia (ECA) na kuhitimu mwaka 2013.
Matokeo hayakuwa mazuri, sababu zilikuwa nyingi lakini nisingependa kuzifanya kuwa kikwazo cha kuto-move on maana muda haurudi nyuma na naamini ilikuwa ni mitihani tu ya kimaisha ambayo imenisukuma kuelekea katika dira mpya hadi kufikia hapa nilipo.
Haikuwa pendekezo langu kuchukua masomo ya biashara ila kwa wakati huo mazingira ya shule za kata walimu wa science ilikuwa issue sana.
Hivyo ilinilazimu nisome masomo haya ya biashara kwa sababu ya woga wa kufeli maana walimu wa science ilikuwa wanaonekana kipindi cha mitihani tu ila vipindi vya darasani ni mara chache sana.
Kusudio langu hasa ni kusoma masomo ya science (PCM au PGM) na kuyafanyia mitihani kwa level zote mbili kwa muda wa miaka miwili ili niwe na msingi imara utakaoniwezesha kuendelea na elimu ya juu hasa upande wa natural sciences au Engineering kutokana na fursa ambazo nakutana nazo.
Kwa sasa naishi DAR na ni mfanya biashara ila nashukuru nina muda mwingi wa kusoma.
Je, endapo nitaamua kuanza kuelekea kwenye dira hii mpya nitawezaje kufanya mitihani ya science kwa level zote mbili kama PC CANDIDATE?
Natanguliza shukrani kwa watakaonionesha njia.