Je Lissu kapiga chini ya mkanda au kasema ukweli!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,641
8,840
Nilivyokuwa Ilboru 1990-1993 niliambiwa miaka ya nyuma kulikuwa na kijana machachari sana ambaye alikuwa anaitwa Antiphas. Umachachari huo ulitokana na debate club za pale Ilboru ambazo zilikuwa mashuhuri sana. Ilboru kulikuwa na debate club ambazo kila ijumaa ya mwisho wa mwezi kuna debate ya watu wawili kwenye hoja kubwa za wakati huo. Miaka ya 80's Marekani chini ya Raisi Regan alipiga bomu nyumbani kwa Ghadafi na kuuwa watu wa famia yake baada ya magaidi kuteka na kuuwa watu kwenye ndege. Nasikia kukawa na debate kubwa je wamarekani walikuwa na haki ya kupiga yale mabomu na hii debate ilikuwa mwaka 1986 pale Ilboru. Lissu ndiyo aliacha historia kwenye debate hii pale Ilboru ambako yeye alikuwa anasema Marekani walikosea na mwana debate mwingine mahiri alikuwa advocate Joseph mpuya. Mpaka leo ameacha historia pale Ilboru . Nasema haya yote kwasababu Lissu ni tofauti kuanzia akiwa mtoto na anakipaji cha kipekee kwenye mambo haya ya haki, debate, rushwa na maono ya nchi. Ni ngumu kushindana naye kwenye debate kwasababu alianza zamani sana kuanzia akiwa Form 2.

Kweli hili swala la Zanzibari kila mtu anaogopa kufanya debate na Lissu badala yake viongizi wengine wanadai Lissu apuuzwe. Lissu hawezi kupuuzwa kwasababu ana hoja za msingi. Muungano huu wa Tanzania unapendelea zaidi upande wa zanzibar kwenye uwakilishi. Unabagua waziwazi wananchi wa bara kule zanzibar na haya yapo kikatiba. Lakini kibaya katiba hizi mbili haziendani kitu ambacho kina leta matatizo na Lissu hata nyamaza kwasababu tu ya kuogopa kuitwa mbaguzi.

Swali ni kwamba Je Lissu kasema ukweli au kapiga chini ya mkanda kwenye hili swala la Zanzibar?
Je serikali itaogopa kuendelea kuwapa biashara waarabu kwasababu ya Lissu? kama biashara ya mabasi ya mwendo kasi?
Je serikali itaogopa kuwakodisha waarabu zaidi kwenye vitalu maalumu vya uwindaji kwasababu ya Lissu?
Je uhamishaji wa wamasai utaendelea au kuna pose kwa muda?
Je Mama ataendelea kufanya anayo amini au anasubiri maumivu yaishe kwanza?
Je Mama atabadilika na kuanza Umagufuli kama machawa wanavyotaka na kuanza kufunga wapinzani bila sababu na kuanzia na kesi fake kwa Lissu? Je watafanikiwa?
 
Niliwahi kusikia Lissu alilumbana na makachero kwenye kambi ya Jeshi JKT mgogoro ulimalizwa na Hayati Ali Hassan Mwinyi baada ya Hoja za Lissu kuungwa mkono na makruta wengi kambini.

Huyu jamaa sio Mtu wa kawaida.
 
Lisu anasema tanganyika imemezwa jusa nae anasema zanziber imemezwa sasa tumsikilize nani?
 
Kitakachoiangusha Serikali ya CCM ni ugumu wa maisha na UCHAWA. Mtu akisema ukweli nongwa.
Uko sahihi. CCM hawajui tu. Uchawa ni mbaya sana. Naweza hata kusema kilimchomuua Magufuli na kundi lake kusambaratika ni uchawa!
 
Back
Top Bottom