Je, Amina atakubali kutoa penzi..?

Jambo Kubwa

Senior Member
Jan 21, 2017
150
205
Habari ndugu jamaa na marafiki.

Jambo Kubwa nawapa kisa changu alafu mnisaidie kujibu swali langu lililosimama kama kichwa cha habari hii.

Wakati nimeanza chuo, chuo flani chenye jina kubwa jijini Dar es Salaam nilibahatika kupata rafiki wa kike anaitwa Amina. (naamanisha ni rafiki wala sio mpenzi kama wewe ulivyotafsiri, hahah).

Rafiki yangu huyu nilisoma nae kozi moja, kadri siku zilivyozidi kwenda ukaribu wetu ulizidi sana hadi watu wakasema sisi ni wapenzi kumbe si kweli na hatukua na hisia hizo kabisa.

Urafiki wetu ulikomaa tukawa kama ndugu, kusema ukweli ule msemo wa "HAKUNA URAFIKI KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE" mimi niliupinga kwa herufi kubwa kwa sababu niliishi na inawezekana kabisa.

Tulikua tunasaidiana sana, urafiki wetu ulikua wa kwenye raha na shida, hadi masuala ya mapenzi..!! eeh ndio hadi masuala ya mapenzi, namaanisha Alikua ananisadia kutatua changamoto zangu za mahusiano, nikiwa na kimanzi changu tumekorofishana kazi ya kumuweka sawa ilikua yake, akigombana na mchizi wake akiwa na hasira kazi ya kwenda kuongea na jamaa ilikua yangu na wanakaa sawa, mda mwingine alikua ananisaidia kuset mitambo kwa baadhi ya vitoto ili niruke navyo, na kweli nilikua naruka navyo si mchezo.

Kwa mfano wakati tupo 3rd year kuna kitoto kimoja cha first year nikamwambia anisetie, rafiki yangu Amina hakusita akikiset kikasetika nikaruka nacho. Kwa kifupi ayo ndo yalikua maisha yetu.

Huu sasa ni mwaka wa 4 tangu tumalize chuo, urafiki wetu upo pale pale japokua sa hizi hatupo karibu sana kutokana na mihangaiko ya kimaisha kutuweka mbali, lakini haijawai maliza wiki hatujawasiliana na tukianza kuongea kwa simu ni zaidi ya masaa mawili tunaongea tu.

Sasa katika kipindi cha karibuni (ni zaidi ya wiki sasa) hali yangu kihisia imeanza kubadilika. Najikuta naanza kumpenda rafiki yangu Amina, nampenda sana inafikia hatua naangalia picha zake tuu natamani angekua mpenzi wangu yani sielewi kwa kweli.

Sijawai kumwambia, sababu sina uo ujasiri anajua mambo yangu mengi masafi na machafu namjua mchizi wake na mahusiano yake kwa ujumla wake.

Haya mabadiliko ya kihisia ndo yanayonipa shida na kunivuruga kichwa. Je, nimwambie? nikimwambia atanielewa? na akinielewa atanikubali na kunipa penzi lake? na vipi akikataa si ndo ntapoteza hata urafiki uliodumu zaidi ya miaka 7?

Nikijiuliza hayo maswali sipati jibu, lakini jibu ambalo nna uhakika nalo hadi naandika andiko hili ni kwamba NAMPENDA Amina na endapo atanikubali natangaza ndoa kabla huu mwaka haujaisha. NDIO.

Sasa ndugu zangu naombeni ushauri wenu nifanyeje, nimwambie hisia zangu au nibaki nazo moyoni mwangu
Bado najiuliza ili swali "JE, AMINA ATAKUBALI KUTOA PENZI?" au ndio ntapoteza hata urafiki.

Sielewi elewi.
NB: JINA AMINA LIMETUMIKA KUWASILISHA UJUMBE TU.
 
Kama unamaanisha kwa hisia just mwambie ukweli tu kuwa japokua mlikua mnachukuliana kama ndugu wewe siku za karibuni umekuwa na hisia za kuwa nae kimapenzi na unamuhitaji kama mke Sio mpenzi coz mmejuana kitambo mambo ya mpenzi hutaki tena ,Yale ya zaman kukusetia mibususu ilikua ujana tu coz ndo wanaume tulivyo ila kwasasa umetulia na unamuhitaji muanze maisha....ukweli utakuweka huru ukichelewa laxima Kuna siku atakupa Kadi ya harus so wewe liwalo na liwe ndo hisia zako huwezi jidanganya naamini kama ni mwanamke anajielewa atakuelewa all the best kaka
 
Umenipa nguvu kaka, ila vipi akichomoa ..?
 
Hatimaye baada ya muda mrefu unakuwa fisi mwanaume. Acha hizo habari, ni ujinga wa hali ya juu sana. Life mean't to have someone of opposite sex very special.Trust me she is the one. Huna hisia nae, bali shetani anatafuta njia KONGWE ya kukuteganisha nae.
 
Nimekuelewa ndugu, yawezekana ni majaribu tu haya
 
Kama kweli unamaanisha na unalengo la kumuoa mwambie ukweli wako usimpigie simu ila ongea nae ana kwa ana funguka kila kitu wanaume tumeumbwa kutoshindwa swala la kuchomoa hilo litategemeana na maelezo yako kwake na yeye atakuelewaje
 
Back
Top Bottom