Nilipokuwa mtoto kuna wakati nilikuwa naona wazazi hasa baba kama wamezidisha unoko ila kwa sasa ndo nimekuja kuelewa nilikuwa najengwa kuwa mtu bora. Haya hapa makatazo ambayo nilidhani ni ya kinoko kumbe yalikuwa mema sana.
1. Giza likiingia halafu usiwepo nyumbani balaa lake lilikuwa zito mno. Baba alikuwa ana utaratibu wa kula chakula jioni nyumbani hivyo mida ya saa moja moja huwa tuko nyumbani. Ikawa rahisi kwake kujua nani hayupo home.
2. Kanisa letu lina kambi za vijana na picnic za hapa na pale. Mzazi wangu alikuwa ni mgumu mno kuruhusu kuhudhuria hizo kambi. Nakumbuka kuna kambi ya vijana kanda ya kaskazini ilikuwa inafanyikia Mlima Shengena, Same ila ilikuwa ngumu sana mzee kukubali mimi na dada yangu kwenda. Ukubwani ndo nimekuja kwenye zile kambi watu hupigana miti kinyama bila kujali kama ni kambi ya kidini.
3. Kabla ya ujio wa simu zamani tulikuwa tunajiburudisha na magazeti ya Sani, Bongo na mengine. Ila kuna majarida yalikuwa yamejaa stori za ngono. Mzee akapiga marufuku majarida yote nyumbani kwake. Tuliishia kumaind kimoyomoyo.
4. Urafiki wa wazazi wangu na wale waalimu wanoko shuleni ulikuwa unanikera sana. Kuna siku nilifanya kosa shule nikamchenga mwalimu. Ile jioni tunatoka kuchunga namkuta yule ticha mnoko yuko na baba nje wanasikiliza DIRA YA DUNIA huku wakipata chai. Wote wawili walinipa kibano. Ila ndo miaka kadhaa baadae niligundua yule mwalimu alinipenda sana na aliona nitafika mbali.
5. Kwenda kanisani ilikuwa ni lazima na kutokwenda ni kosa lisilosameheka. Yaani yule mzee hata kama hajaenda lazima apate ripoti ya walioenda na ambao hawakwenda. Hadi leo hii nikiendaga home ikifika siku ya ibada najikuta tu naenda. Ile sheria ingawa kwa sasa sio lazima sana ila ndo hivyo ukiwa home unajikuta unaifuata.
6. Kipindi cha likizo huwa ni kazi tu hakuna mambo za kwenda tuition. Likizo zangu zote za O - level nilikuwa nakutana na programs mbalimbali zilizoandaliwa kitaalam na kuniweka bize likizo nzima. Nakumbuka likizo ya mwezi wa 6 nikiwa form four nilipelekwa Karatu kwenye shamba la ngano kupambana na ndege waitwao kwelea kwelea. Na baada ya form four ule muda wote wa kusubiria matokeo hadi kwenda form five nilifanya kazi kwenye mashamba ya vitunguu. Yaani mzee alihakikisha kuanzia kupanda hadi kupeleka kitunguu sokoni Kilombero nashiriki. Ndo kipindi nilijua kilimo cha Tanzania ni kama kamari tu.