Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?

The dumb Professor

JF-Expert Member
Dec 10, 2023
667
1,420
Wasalaam,

Nilikuwa down bad, yaani nimepigika kinoma, yaani apeche alolo, yaani mbombo ngafu, yaani moja haikai mbili haikai, Yani nmechina mweupe pee. Kula ya mashaka, kulala kama ndege. Ila Kuna huyu jamaa angu tulisoma ote Olevel akaniconnect kwenye ajira inalipa fresh sio haba.

Sasa tatizo, imekuwa kama kero, Kila siku anajimwambafy kuwa bila yeye nsingetoboa anasema natakiwa niwe namshukuru kila mshahara ukitoka. Tukienda out Kila siku Mimi tu ndo anataka nimnunulie bia. Wote tuna mshahara ila yeye anataka na shida zake Mimi nimtatulie.

Mimi naona imekuwa kama manyanyaso sasa.

Nifanyaje?
 
Si haki, chukua shillingi elfu 50 mwambie kaka asantee Kwa mchango wako sina kikubwa chakukupa lakini hiki kinatosha. Kisha baada yahapo mkatae, kwani lazima utoke nae out?. Akikuambia mtoke ukamuambia hauko vizuri kifedha atakulazimisha?.

Jifunze kusema hapana.
Kuna siku nilimpa 30 akasema "kazi nmekuconnect ya mil 30 kwa mwaka Wewe unanipa afu30?"
 
Si haki, chukua shillingi elfu 50 mwambie kaka asantee Kwa mchango wako sina kikubwa chakukupa lakini hiki kinatosha. Kisha baada yahapo mkatae, kwani lazima utoke nae out?. Akikuambia mtoke ukamuambia hauko vizuri kifedha atakulazimisha?.

Jifunze kusema hapana.
Elf hamsini haitoshi ampe laki tatu 300k au 500k

Jamaa atatulia
fanya hayo vinginevyo jamaaa atakufanyia hila utolewe kazini

Mm yamenikutaaa hayo
 
Back
Top Bottom