iSiKuPiTe hiI iSoMe jApO nI......., itAkU.....!!!(MaMA)

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
[h=6]Hakukuwa na mwanamke
ambaye
nilikuwa simpendi kama mama
... yangu. Yeye alikuwa masikini wa
kutupwa huku uso wake ukiwa
unatisha
kwa
kuwa tu hakuwa na jicho moja.
Kila nilipokuwa nikimuona nilikuwa
nikimkasirikia sana. Alikuwa
akijaribu
kunionyesha mapenzi kama
mtoto
wake lakini kwangu sikuwa nikitaka
kumuona kabisa. Kuna siku
nilikaa
nae
chini na kumwambia kwamba
nilitamani sana kuwa na furaha,
akaniuliza kitu gani kifanyike
ili
niwe
na furaha, kiukweli
nikamwambia kwamba kama angekufa muda
huo, hakika ningefurai milele.
Nikafanikiwa kusoma chuo na
kwenda
nchini Afrika Kusini kusomea
sheria, nilifurahi sana. Sikutaka kurudi nyumbani, nikaoa huko
huko na
kupata watoto. Katika maisha
yangu
yote hayo hakika
sikumkumbuka kabisa mama yangu, nilikuwa
nikitamani sana afe ili niwe na
furaha. Nikafanikiwa kupata
watoto wawili
huku nikiwa nimejenga
nyumba ya kifaari na kuwa na utajiri
mkubwa.
Kuna siku nikasikia mlango
ukigongwa, watoto wangu
wakaenda
kuufungua mlango, ALIKUWA NI
MAMA YANGU amekuja
kunitembelea. Watoto
wangu wakaanza kulia kwani
walikuwa wakimuogopa sana
mama yangu kutokana na hali ya
kukosa
jicho aliyokuwa nayo,
nikaamua
kwenda mlangoni,
nilipomuona, alifikiri ningetabasamu,
nikamfokea kwa haira
sana "TOKA NYUMBANI
KWANGU
KINYAGO WEWEUNAWATISHA
WATOTO WANGU". Kwa sauti iliyojaa
upole,
mama yangu akaniambia
"SAMAHANI
BABA. NAFIKIRI NITAKUWA
NIMEKOSEA NJIA" hapo hapo akaondoka.
Nikafanikiwa kutembelea
nchini
Tanzania, na moja kwa moja
nikaanza
kwenda kwenye nyumba ile tuliyokuwa tunakaa. Majirani
zangu
wakaniambia kuwa mama
yangu
alikuwa amefariki kwa kuwa
tundu la jicho lake lilikuwa limeharibu
hadi
mishipa ya fahamu, WALA
SIKUHUZUNIKA KABISA ZAIDI
YA
KUTABASAMU. Hapo ndipo waliponiletea barua ambayo
aliiandika mama yangu na
kunipa.
Barua ile
ilikuwa imeandikwa hivi.
Mwanangu mpendwa. Najua kwamba katika maisha
yako
ulikuwa ukinichukia sana ila
amini
kwamba nilikuwa nikikupenda
sana. Ulipokuwa mtoto ulipata ajali,
jicho lako
likapasuka ila kwa kuwa
nilikuwa
sitaki uishi maisha ya kuwa na
jicho moja, nikaamua kutoa jicho
langu
na
kuwekewa wewe ili tu uweze
kuuona
ulimwengu kwa macho yote mawili.
Sikutaka kujali ningepata
matatizo
gani
lakini niliamini kwamba wewe
ndiye ungekuwa furaha yangu hasa kila
nitakapokuona unauangalia
ulimwengu huu huku ukitumia
jicho
langu moja.
Mimi mama yako Mpendwa
[/h]
 
Oosh! bampami,
inatufundisha,si kila ulicho nacho mwilini umezaliwa nacho,
vingine umepaka au kubandika,
cheki kope,mkorogo,lace wig,kucha,hips,makalio na vinginevyo utaongezea mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom