Ipende Nchi Yako, Mpende Rais wa JMT, Ipende Serikali na Mungu wa mbinguni atakubariki!

Hilo ni ombi langu kwa Watanzania wote na Mungu wa mbinguni atawabariki sana

Nawatakia Dominica Njema 😄
Ombi lina mawili.
Kukataliwa ama kukubaliwa....

Binafsi Naipenda Tanzania lakini huyu mtawala wa sasa ana walakini mkubwa sana
 
Viongozi wakuu wa nchi huwekwa na Yeye mwenyewe Mungu wa mbinguni
Kama ni hivyo, Yale mabegi meusi ya kura ni ya nini?
Kama wanawekwa na Mungu, huu ulinzi wote wa nini,
Hiyo Mungu aliwaweka hawezi kuwalinda?
Jo, usimhusishe Mungu na siasa zenu, mnazoziita sissa ni sayansi, ikihusisha zaidi wizi wa kura na mizengwe,
 
Naipenda sana Nchi yangu Tanzania 🇹🇿

Nachukia sana RUSHWA , ubadhirifu wa Mali ya umma na Wizi wa kura.

Napenda kuona HAKI ikitawala juu ya nchi.

Amen
Dumisha Amani kipimo Cha HAKI anacho Mungu wa mbinguni
 
Penda Nchi Yako. Tetea wanyonge dhidi ya walaji kwa urefu wa kamba. Wanastahili upendo zaidi kuliko watawala mafisadi. Mungu atakubariki
images - 2024-05-05T103251.534.jpeg
 
Kama ni hivyo, Yale mabegi meusi ya kura ni ya nini?
Kama wanawekwa na Mungu, huu ulinzi wote wa nini,
Hiyo Mungu aliwaweka hawezi kuwalinda?
Jo, usimhusishe Mungu na siasa zenu, mnazoziita sissa ni sayansi, ikihusisha zaidi wizi wa kura na mizengwe,
Shetani ameruhusiwa kuwajaribu Wanadamu na kuwapepeta kama ngano

Uongozi wa Wanadamu huwekwa na Mungu wa mbinguni Mwenyewe
 
HILI NALO MKALITAZAME.

Nawaagiza akina Kasimu muende mkaliangalie hili tujue "tunakwenda vipi".
 
Mwl. Nyerere aliwahi kusema Ikulu ni mahali patakatifu .Lakini hakuna mtakatifu kwa hii Ccm ya sasa .Ccm inaingia Ikulu kwa wizi wa kura , wanawadanganya wananchi , wanafanya ufisadi wa kutisha . Haya mambo yanainajisi nchi na nchi inalaanika ndo maana nchi sasa inaanza kupigwa na majanga ya asili .
 
Back
Top Bottom