KWELI Inawezekana kuwa kwenye siku za hatari ukiwa kwenye siku za hedhi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Nina swali ndugu zangu hivi inawezekana siku za hatari zikaangukia katika mzunguko kuingiliana na siku za hedhi?

Mfano, siku za hedhi ni tano ile siku ya 4 au 5 ikiwa siku ya hatari?🤔

periodcalendar_bloglarge.jpg
 
Tunachokijua
Hedhi ni tendo la kibaiolojia linalotokea kila mwezi kwenye maisha ya mwanamke aliyevunja ungo. Tendo hili huhusisha utoaji wa damu na tishu za mwili kutoka kwenye mji wa uzazi kupitia uke.

Mfumo wa homoni za mwili ndio huongoza mzunguko wa hedhi ya mwanamke. Japokuwa mzunguko huu unaweza kuchukua siku zozote kati ya 21-35, wanawake wengi huwa na mzunguko wa wastani wa siku 28 ambao kwa lugha rahisi hufahamika kama mzunguko wa kawaida.

Katika hali ya kawaida, mzunguko wa hedhi wa kila mwezi hugawanywa kwenye vipindi vinne ambapo kimoja kati yake huitwa Ovulation, yaani kipindi cha utolewaji (uanguaji) wa yai lililopevuka, kipindi ambacho kwa lugha maarufu inayofahamika sana mitaani huitwa kipindi cha siku za hatari.
Kila mzunguko wa hedhi huwa na siku yake ya kutoa yai kwa mwezi husika, siku hii ndio yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ujauzito kuliko zingine.

Mathalani, siku ya ovulation kwa mtu mwenye mzunguko wa siku 35 ni tofauti na mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28. Hali ipo hivyo kwa mizunguko mingine pia.

Rejea jedwali hili linaloonesha siku za hatari kwa kila mzunguko.

screenshot-2023-10-20-090751-png.2787023

Jedwali la mizunguko ya hedhi (JamiiForums)
Kupata mimba wakati wa hedhi
Kama ilivyofafanuliwa awali, kila mzunguko wa hedhi huwa na siku yake ya ovulation ambayo huambatana na siku zingine kadhaa ambao kwazo pia mwanamke anaweza kupata ujauzito.

Kwa hesabu za kawaida, siku hii hutokea wastani wa siku 14 kabla ya kutokea kwa hedhi ya kila mwezi.

Swali linabaki kuwa, inawezekana kwa baadhi ya wanawake kupata mimba huku wakiwa kwenye siku zao za hedhi?

JamiiForums imefuatilia suala hili na kubaini kuwa kisayansi linawezekana. Mathalani, mwanamke mwenye mzunguko mfupi wa hedhi wa siku 21 hupata ovulation siku ya 7, na uwezekano wa kupata ujauzito upo kuanzia siku ya 3 ya hedhi hadi siku ya 8 ya hedhi.

Hii inatoa maana kuwa wakati hedhi inaendelea (siku ya 3) tayari mwanamke husika anakuwa yupo kwenye siku za hatari. Pia, wanawake wenye mizunguko mifupi ya siku 22 hadi 24 wanaweza kupata mimba wakiwa bado wapo kwenye siku zao za hedhi.

Hivyo, kwa wanawake wenye mizunguko mifupi ya hedhi wanaweza kupata ujauzito wakiwa bado wapo kwenye kipindi cha kutoa damu za hedhi ikiwa watashiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga.

"Ikiwa una mzunguko mfupi zaidi, mfano ule wa siku 21 hadi 24, hiyo inamaanisha kuwa una ovulation mapema katika mzunguko. Kwa sababu mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani yako kwa hadi siku 5, unaweza kujamiiana mwishoni mwa kipindi chako na kisha kutunga mimba siku 4 au 5 baadaye sababu ovulation yako huja mapema.

Uwezekano wa kupata mimba wakati wa kipindi cha hedhi ni mdogo, lakini upo."
inaandika taasisi ya American Pregnancy Association.

Utambuzi wa siku za Ovulation
Kipindi hiki hutawaliwa na mabadiliko makubwa ya kimwili na kihisia.
8EE234F7-3D40-4043-8783-0DDFDBEA354B-653x375.jpeg

Muonekano wa yai siku ya ovulation
Dalili za uwepo wa hali hii hutofautiana miongoni mwa wanawake, baadhi yao huwa hawawezi hata kuhisi mabadiliko haya.

Kwa mujibu wa Tovuti ya Afyainfo, baadhi ya dalili zinazoweza kutumika kutambua siku hizi ni
  1. Ute wa mlango wa kizazi huzalishwa kwa wingi wakati huu, hufanana na ute wa yai la kuku lililopasuliwa.
  2. Mlango wa kizazi huongezeka ulaini wake, hupanda juu kidogo, hupanuka kiasi na huwa mbichi sana.
  3. Kuongezeka kwa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
  4. Maumivu ya nyonga.
  5. Kuwasha na kuvimba kwa matiti.
  6. Kuongezeka kwa uwezo wa kunusa na kutofautisha harufu mbalimbali za vitu.
  7. Sehemu ya nje ya uke (mashavu) au uke wenyewe kuonekana umevimba.
Kwa wanawake wasiofahamu siku zao za ovulation wanaweza kutumia dalili hizi ili ziweze kuwasaidia katika kujikinga na ujauzito usiotarajiwa.
Maybe siku ya 6 kuendelea hasa kwa wale wanawake ambao wametumia dawa za kurutubisha mayai
 
Nina swali ndugu zangu hivi inawezekana siku za hatari zikaangukia katika mzunguko kuingiliana na siku za hedhi?

Mfano, siku za hedhi ni tano ile siku ya 4 au 5 ikiwa siku ya hatari?🤔
Inawezekana ka wele ambayo Wana mizunguko miwili kwa mwezi mmoja
 
Inawezekana kama Sara alipata ujauzito akiwa bibi na Mariam akapata mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu!.. wewe nengay ni nani mpk ukose hatari kwenye hatari...? Kama hayo yaliwezekana Israel hilo lako haliwezi shindikana hapo kwa mpalange! Amini tu.

Kama mdada mwenye mtoto mmoja anawezakuwa na baba watoto watatu na wote wanahudumia na kadi za clinic kwa wababa wote watatu zipo!,hilo lako mbona ni dogo! This world is full of surprise..

Kuna vishetani vitakuja kupinga!😅
 
Kama kuna qatu wana vichwa viwili mwili mmoja, unashangaa mtu kuwa na mayai mawili kwa wakati tofauti?

Sio common lakini ipo.
 
Maybe siku ya 6 kuendelea hasa kwa wale wanawake ambao wametumia dawa za kurutubisha mayai
Kurutubishaje mayai nielekeze
Inawezekana kama Sara alipata ujauzito akiwa bibi na Mariam akapata mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu!.. wewe nengay ni nani mpk ukose hatari kwenye hatari...? Kama hayo yaliwezekana Israel hilo lako haliwezi shindikana hapo kwa mpalange! Amini tu.
Kama mdada mwenye mtoto mmoja anawezakuwa na baba watoto watatu na wote wanahudumia na kadi za clinic kwa wababa wote watatu zipo!,hilo lako mbona ni dogo! This world is full of surprise..

Kuna vishetani vitakuja kupinga!😅
😂😂😂 mambo ya Israel yamefikaje apa
 
Nengay, kumradhi wewe ni Mmasai?
Jina lako lina maana 'Wa Mungu', kwa kilugha chetu.

Turudi kwenye uzi.
Unachopaswa kujua ni kuwa baada ya siku za hedhi kutamatika, zinazofata ni siku salama.

Maana yake ni kuwa ukishamaliza siku zako za hedhi, kuna siku takribani 5 ama 6 kutegemeana na mzunguko wako, zinakuwa siku salama. Na mhusika hatoweza kupata mimba.

Kwa muktadha huo, HAPANA.
Ndio mm mmasai mpendwa
 
Nachoweza sema sio vizuri kuduu hizo siku, so huna haja ya kuwaza hatari au sio hatari labda baada ya hapo ndio sawa
 
A woman’s ovulation cycles can vary, so it’s statistically possible you could become pregnant while on your period. While pregnancy is less likely in the earlier days of your period, the chances increase in the later days.
GOOGLE wameshasema
Inawezekana kuwa na siku za hatari wakati WA period
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom