IMF yawapongeza Rais Samia na Waziri Mwigulu Nchemba

Nimesoma article nzima sijaona mahali ambapo Mwigulu kama ulivyomuita Mr Clean katajwa kuwa ni waziri bora wa fedha Afrika.

Wala sijaona mahali ambapo Samia kapongezwa .

Sababu za ukuaji na zinazoweza kupelekea na kupata hiyo B+ zimetajwa kuwa ni hizi ambazo zipo aya ya mwisho.

Mleta Mada wapi Samia na huyu Mr Clean wametajwa ?

"On the other hand, factors that could lead to a credit rating upgrade for Tanzania include:

1.Higher domestic revenue mobilisation, greater transparency and confidence in the exchange-rate regime.

2.Greater central bank independence.
 
Kwa hakika Mheshimiwa Dr Mwigulu Lameck Nchemba Anastahili pongezi sana kama waziri wetu wa Fedha kwa namna alivyo tumia vyema taalaluma yake katika kujenga uchumi ulio imara ,shirikishi na wenye kugusa maisha ya watu. Ni kiongozi ambaye Mheshimiwa Rais ana kila sababu ya kujivunia uteuzi wake na kutokujuta kwa kumteua katika nafasi hiyo nyeti kabisa.

Mwigulu kupata kwake first Class UDSM ilikuwa siyo kwa bahati mbaya bali ni kwa uwezo mkubwa wa kiakili alionao.

Hongera sana Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba wewe kweli ni Daktari wa uchumi na mwenye tiba sahihi kwa uchumi wa Tanzania na kwa hakika Umeupatia Afya njema uchumi wetu,ambapo sasa uchumi wetu unatembea kwa kuringa ,nguvu na kujiamini kwa hali ya juu sana.

Apongezwe sana pia Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutambua na kuwa na uwezo mkubwa wa kupanga safu nzuri ya ushindi na kujuwa mchezaji gani acheze wapi na yupi acheze wapi.

Naamini Mheshimiwa Rais wetu ataendelea kumuamini Mheshimiwa waziri kuendelea kusalia katika nafasi hiyo ya Waziri wa fedha pasipo kumuhamisha. Maana ni wizara nyeti sana hiyo na moyo wa Taifa ambayo imepata mtu sahihi.

Nami pia naunga mkono kuwa Mheshimiwa ni Mr Clean maana sijawahi kusikia wala kuona akiguswa na tuhuma zozote zile za ufisadi au rushwa .
Kwenye hiyo article hakuna mahali pameandikwa Mr Clean achilia mbali Mwigulu au Samia!

Au wewe una article yako ukiwa chief editor wa IMF siku hizi?
 
Wameona jamaa analipa madeni,IMF wao suala la Wananchi kusota kiuchumi haliwahusu.
Uchumi mzuri ni lazima uongeze ajira,watu wanamaliza vyuo hawana kazi alafu unawaambia Uchumi wenu upo stable,how!
Labda wamepima kupitia zile royal family
 
Nukuu IMF " This makes Tanzania's economy BIGGER than several small European countries" hapa wameongeza chumvi..
Nukuu "The size of Tanzania's GDP in 2023 has grown to $85.42 billion from $69.94 billion in 2021, according to the IMF" Apewe maua yake. Na bado DP World bado haijatema. Bwawa la Nyerere halijatema na...., na.......na.....

Tahadhari:
  • 2021 mpaka 2023 alikuwa huru sana kutekeleza maono yake japo ya matuta madogo madogo aliyokutana naye.
  • 2024-2025 Ni mwaka wa mtikisiko. Aidha atakomaa au atadhoofishwa kabisa.
  • 2026-2030 ( ???......) Ni ngumu kutabiri. Ila sidhani kama anaweza kufanya vizuri kama 2021-2023. Kuna mawili yanaweza kutokea: (a) Apangiwe safu na timu... na aamue kuliacha basi liende bila muelekeo(Probability 70%). (b) Akomae(liwalo na liwe) na kuendelea kupanga safu zake kama 2021-2023, ili atekeleze maono yake (probability 30%).
Ni vigumu kujua atacheza vipi, ila Mama anaitaka mema Tanzania.
Ana nia njema kweli ! Ila Bam’s alisema yapo Majitu yanajaribu kumkwamisha !
 
Mwigulu tumponde kwenye siasa zake lakini Uchumi wa nchi kaumudu sana.

Majirani wanakiri hilo sana, nilikuwa kisumu juzi, wanatupongeza sana linapojuja suala la stability ya uchumi na siasa za nchi.

Mwigulu atakuwa Rais baada ya Samia kwa fact ya kukuza uchumi na collection ya tax.

Wengi huwa wanamchukia Mwigulu bila facts, hizi story za wizi wake hazina supporting vivid evidence, zote ni story za vijiwe vya kahawa.

Kwenye sekta ya fedha Mwigulu hana anachoiba, TRA wanakusanya kimfumo, BOT wanatoa kimfumo, Mikopo na misaada inaingia kimfumo, Mwigulu hakutani na hata senti, kwenye wizi tumtoe, tumzodoe kwa siasa zetu za speculation ya 2030.
 
•Yasema MR CLEAN ni Waziri Bora wa fedha afrika.
•Facts hizi za kichumi zimembeba.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limemtaja Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe Dkt Mwigulu Nchemba (ambaye watanzania wengi hupenda kumwita “ Mr Clean ”) ni daktari bingwa wa uchumi na mtaalam halisi wa uchumi na ndio Waziri bora wa fedha aliesimamia kwa ubora wa hali ya juu misingi ya kichumi kuliko mawaziri wote wa fedha kwa nchi za Africa.

Hayo yamesemwa na IMF kufuatia report yao inayoitaja Tanzania kuwa ni mwiongoni mwa Nchi chache Duniani zenye Uchumi Imara.
IMF inasema Tanzania chini ya uongozi makini wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatekeleza Miradi mingi mikubwa ya kimkakati na miradi mingi ya huduma za jamii lakini deni lake ni limeendelea kuwa dogo na himilivu, na kuweka wazi kuwa nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi zenye madeni madogo sana duniani kote, Pili IMF imesema licha ya misukosuko ya uchumi dunia, "Mr Clean" ameweza kubakiza mfumuko wa bei asilimia 3, Pia IMF imesema licha ya matatizo ya upatikanaji wa Fedha za Kigeni ulimwenguni kote "Mr Clean" ameweza kudumisha uimara wa shilingi ya kitanzania, na kwamba Tanzania ndio nchi pekee Africa Mashariki yenye uwiano mzuri wa vitabu vyake vinayoweza kuvutia mitaji ya Fedha.

IMF IMEMPONGEZA MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA UONGOZI BORA WA TANZANIA, UADILIFU NA UTEKELEZAJI BORA WA MAENDELEO. TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KULIKO NCHI ZOTE ZA EAC NDANI YA MUDA WAKE.

Source: IMF MEDIA RELEASE

View: https://x.com/TanzaniaInsight/status/1737011736908103877?t=vB--7FMxeM4MECr6x59NaA&s=08

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1686792647954886657?t=SAEhofIp8pnLcHPy6x4-Zw&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1650769226699886592?t=_DqRd53M-71uPxneNyJCHg&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1647159085425467392?t=jGM_PNEJMz7sDkxLGnT6jw&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1625049055746306049?t=ltrjqJCC_wp0jj5V2h33Ew&s=19

Umeharibu ulipoita Mr Clean. Mwigulu hawezi kuwa Mr Clean, ni fisadi tu anaye vaa scarf ya bendera ya Tanzania
 
Mwigulu tumponde kwenye siasa zake lakini Uchumi wa nchi kaumudu sana.

Majirani wanakiri hilo sana, nilikuwa kisumu juzi, wanatupongeza sana linapojuja suala la stability ya uchumi na siasa za nchi.

Mwigulu atakuwa Rais baada ya Samia kwa fact ya kukuza uchumi na collection ya tax.

Wengi huwa wanamchukia Mwigulu bila facts, hizi story za wizi wake hazina supporting vivid evidence, zote ni story za vijiwe vya kahawa.

Kwenye sekta ya fedha Mwigulu hana anachoiba, TRA wanakusanya kimfumo, BOT wanatoa kimfumo, Mikopo na misaada inaingia kimfumo, Mwigulu hakutani na hata senti, kwenye wizi tumtoe, tumzodoe kwa siasa zetu za speculation ya 2030.
Mwigulu hana mchango katika kukuza uchumi wa nchi. Pengine angekuwa Waziri mwingine labda tungekuwa tumeipita Kenya in terms of GDP. Kenya kwa takwimu za 2023 walikuwa na DGP ya USD 113 Billion wakati Tanzania tulikuwa na USD 75 Billion.

Sera zake za kodi ya miamala ya mawasiliano, udhaifu wa makusanyo ya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ni kati ya maeneo ALIYOFELI sana
 
Hizi ni Kampeni za Wafia tumbo.

Hatahivyo, ukizingatia yale yanayoendelea Duniani-Davos in particular, utona hizi ni ngonjera (rushwa tu)ili kuanza kuwalainisha wakulu.

Wakifika mezani mabichwa yamekua, wanaanguka tu misignecha.

NB: Naona kuna kupokezana vijiti wa namna fulani ya uwasilishaji taarifa. Duly noted
 
Ana nia njema kweli ! Ila Bam’s alisema yapo Majitu yanajaribu kumkwamisha !
Haya Majitu ndio ninayoyaogopa sanaaaaaa! Sijui tufanyeje!
Maana naye anapitia machungu sana kama Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi alivyopitia kwa Nyerere na washiriki wake.
Dogo tunaloweza kufanya ni kuonyesha wazi wazi kuwa tunamuunga mkono kwa juhudi zake.
 
•Yasema MR CLEAN ni Waziri Bora wa fedha afrika.
•Facts hizi za kichumi zimembeba.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limemtaja Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe Dkt Mwigulu Nchemba (ambaye watanzania wengi hupenda kumwita “ Mr Clean ”) ni daktari bingwa wa uchumi na mtaalam halisi wa uchumi na ndio Waziri bora wa fedha aliesimamia kwa ubora wa hali ya juu misingi ya kichumi kuliko mawaziri wote wa fedha kwa nchi za Africa.

Hayo yamesemwa na IMF kufuatia report yao inayoitaja Tanzania kuwa ni mwiongoni mwa Nchi chache Duniani zenye Uchumi Imara.
IMF inasema Tanzania chini ya uongozi makini wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatekeleza Miradi mingi mikubwa ya kimkakati na miradi mingi ya huduma za jamii lakini deni lake ni limeendelea kuwa dogo na himilivu, na kuweka wazi kuwa nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi zenye madeni madogo sana duniani kote, Pili IMF imesema licha ya misukosuko ya uchumi dunia, "Mr Clean" ameweza kubakiza mfumuko wa bei asilimia 3, Pia IMF imesema licha ya matatizo ya upatikanaji wa Fedha za Kigeni ulimwenguni kote "Mr Clean" ameweza kudumisha uimara wa shilingi ya kitanzania, na kwamba Tanzania ndio nchi pekee Africa Mashariki yenye uwiano mzuri wa vitabu vyake vinayoweza kuvutia mitaji ya Fedha.

IMF IMEMPONGEZA MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA UONGOZI BORA WA TANZANIA, UADILIFU NA UTEKELEZAJI BORA WA MAENDELEO. TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KULIKO NCHI ZOTE ZA EAC NDANI YA MUDA WAKE.

Source: IMF MEDIA RELEASE

View: https://x.com/TanzaniaInsight/status/1737011736908103877?t=vB--7FMxeM4MECr6x59NaA&s=08

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1686792647954886657?t=SAEhofIp8pnLcHPy6x4-Zw&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1650769226699886592?t=_DqRd53M-71uPxneNyJCHg&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1647159085425467392?t=jGM_PNEJMz7sDkxLGnT6jw&s=19

View: https://twitter.com/TanzaniaInsight/status/1625049055746306049?t=ltrjqJCC_wp0jj5V2h33Ew&s=19

Jarida la Business Insider Afrika ndo IMF?

Ripoti za wizi wapesa za mikopo ulioripotiwa na CAG mmeficha wapi?

Mnawadanganya Uchumi unajua wakati pesa zinakopwa Ili zije kuibwa?

Miradi mingi imesimama, wakandarasi hawalipwi pesa!!

Tusubiri
 
Back
Top Bottom