IMF wametoa orodha ya nchi zenye madeni makubwa zaidi katika bara la Afrika, Tanzania haipo!

Mkopo ambao unahusisha Kukupangia sera huo ni Ujinga.

Tulilipa deni lote IMF, saiv wameenda kuchukua tena.

Si ajabu wanakupa mkopo na kukupangia matumizi yake. Mfano kajengee matundu ya Choo.
Bila hivyo hawa jamaa watazila zote, tuipe IMF maua yao.
 
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa January,2024 na IMF inaonesha Tanzania ni Kati ya Nchi 10 Za Afrika Zenye deni dogo zaidi ikilinganishwa na Ukubwa wa Uchumi wake.

Kwa Afrika Mashariki ni Tanzania pekee ambayo ni least indebted Country,zingine zote Zina Hali mbaya.

View: https://www.instagram.com/p/C2Fg1zpI1U_/?igsh=MXV5eG56ZTV4YXA0aw==

My Take
Kwa Nchi kama Tanzania ambayo Ina umaskini mkubwa ambao unasababishwa na miundombinu mibovu au kutofikika kabisa kujisifia eti tuna deni dogo ni ujinga.

Serikali Kopeni Pesa Jengeni miundombinu mfungue Uchumi Nchi istawi walau tufikie Debt to GDP Ratio ya 60%.
 
RankCountryDebt amount
1.Egypt$11,968,321,674
2.Angola$3,153,816,667
3.South Africa$2,669,800,000
4.Côte d'Ivoire$2,117,559,620
5.Kenya$2,058,982,100
6.Nigeria$1,840,875,000
7.Ghana$1,644,377,000
8.Morocco$1,499,800,000
9Democratic Republic of Congo$1,294,500,000
.10.Tunisia$1,259,139,338

======

Hii ndio orodha ya nchi 10 za Africa zenye deni kubwa zaidi huko Shirika la Fedha Duniani ( IMF )

Kwa msiofahamu, Nchi Tisa kati ya kumi ndio nchi zinazoshikilia uchumi wote wa Africa,

Hawa ndio magwiji wa kuchota Fedha za IMF kutoka bara la Africa tena kwa riba kiduchu ambayo ni chini ya asilimia moja tena kwa muda wa miaka 15.

Ukiangalia katika orodha ya nchi tajiri kabisa barani Africa utakuta ni hawahawa magwiji wa uchotaji wa maokoto huko IMF.

Hoja yangu Leo, Nikwanini Tanzania yenye kauchumi kiduchu inaogopa kukopa wakati ,hawa makabaila na Matajiri wa kupindukia kama Misri, Nigeria, Morocco, Ghana, South Africa mababa wa uchumi Africa wanakopa kwa kasi kiasi hiki, Why Tanzania tunakwama wapi?

Nchi yetu ya Tanzania kwa kiasi kikubwa inamazezeta ambayo yanawatisha Watanzania wenzao kwamba kukopa dhambi tena ishara ya kufilisika kwa nchi kumbe wanataka kuwafanya Watanzania waendelee kuutamia umasikini wao.

Ombi langu kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba ongezeni kasi ya kukopa ila tu mkope IMF sio maeneo mangeni ili kuepuka riba kubwa.

Nasisitiza Leo, Tanzania tukopeni zaidi ili kujenga miradi yenye output ili na sisi GDP ya nchi yetu na yenyewe ipande kama ile ya EGYPT pamoja na kuwa kinara wa madeni IMF bado ndio nchi tajiri barani Africa.

Kazi iendelee.
Kazi iendelee 👇
Screenshot_20240113-081158.jpg
Screenshot_20240114-202212.jpg
 
Back
Top Bottom