Imedhihirika: Yanga Vs Mamelodi Sundowns ndiyo mechi kubwa kuliko zote hatua ya robo fainali, Simba ni kama wamejikatia tamaa kabisa

Simba na Al Ahly ni trela picha kamili ni Yanga Vs Mamelod jumamosi. Simba amejishushia hadhi Kwa kupigwa 5-1 na Yanga thus why there is no big discussion about their match Africa nzima inaelewa🤔
 
Kuanzia mtaani hadi mitandaoni, mechi iliyowajaa midomoni wapenzi na mashabiki wa soka ni ile ya Yanga. Kuna wanaoiamini Yanga na kuona itaibuka kidedea Benjamin Mkapa na hata mwisho wa mechi mbili. Kuna wanaoibeza na kuona imefikia mwisho. Lakini, Yanga ameteka mazungumzo.

Kuanzia wachambuzi uchwara hadi wale wa maana, mechi ni ya Yanga tu. Wanaizungumza mechi ya Jumamosi kanakwamba hakuna mechi siku ya Ijumaa ambayo kimsingi ndiyo inayotangulia. Hata vikosi vinavyopambanishwa ni vile vya Yanga na Mamelodi.

Simba hawatajwi. Simba wamekosa hamasa na amshaamsha iliyozoeleka. Ni kama vile wamekata tamaa kwa Al Ahly. Wao wanaanza Ijumaa lakini wananchi walio wengi wamepania, wanajadili na kujiandaa kwa Jumamosi 'wakiipuuza' mechi ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Kwani mashabiki wa Simba wamekatishwa tamaa na kitu gani? Hakika, Yanga v Mamelodi Sundowns ndiyo mechi bora kwenye hatua hii. Mpira utapigwa, mshindi atapatikana. Tujue kabisa, Mamelodi ni timu nzuri au la? Tukutane kwa Mkapa Jumamosi!
Subirini Mamelod atumie mbele km mnavyotamka Daima mbele kisha achomoe na huo mwiko nyuma
 
Back
Top Bottom