Ifike mahala mji mpya wa Dar ujengwe nje ya Dar na sio kulazimisha kila kitu kufanyia kwenye hii Dar ya sasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,285
22,815
Wakuu leo nikiwa natafakari upuuzi unaofanywa na TEC nikajikuta nakumbuka ujinga mwingine unaofanywa na wanaoitwa wataalamu wetu. Hii ni kulazimisha kila jambo la maendeleo kufanyia ndani ya jiji la dar hali inayopelekea kuwa na bomoa bomoa nyingi zinazoleta uharibifu mkubwa wa mazingira. Kuna picha niliona mtandaoni jinsi Dar city centre ilivyokuwa miaka ya 70 nikagundua uharibifu mkubwa sana wa Mazingira. Na pia ule utambulisho wa Dar unazidi kutoweka.

Kwa tulipofikia tuseme inatosha na lazima Dar mpya ijengwe nje ya Dar ya sasa. Kurundika maendeleo yote kwenye kieneo kidogo ni ujinga na uharibifu. Hata Dubai hawakubomoa majengo yao ya zamani ili kujenga mji wao unaotikisa dunia nzima. Walienda nje ya mji jangwani na kushusha mji mzuri. Dar bado ina maeneo makubwa kwahiyo kuna uwezekano wa kujenga mji mpya.

Kwa mfano pendekezo la Profesa Janabi kuvunja majengo ya Muhimbili na kujenga upya ni pendekezo la kipumbavu zaidi kwa nyakati hizi.
FB_IMG_1692525085378.jpg
 
Uko sahihi kabisa
Wamembiwa kila siku hawasikii..
Mfano proposal za kujenga muhimbili
Wakati hiyo hela inajenga hata muhimbili 3 mikoa mitatu tofauti...

Sio kujenga tu. Wanaibomoa kwanza ndio wanaanza kuijenga upya.

Najiuliza why wabomoe majengo ? Wakati kuna maeneo kibao yapo wazi nje ya mji na mikoani
 
Back
Top Bottom