Huyu ofisa wa udahili TCU, Fabian Mahundu anapotosha umma kwa maslahi ya nani?

Sasa hivi Rushwa ndio itatawala,TCU walikua hawapokei rushwa nina kuhakikishia 100%.
Sasa hivi vyuo ndio watapokea rushwa na nina mfano tayari wa mtu anaetafutiwa nafasi chuo fulani.

Kwa nini atafutiwe? Kama huyo mtu anatafutiwa chuo basi hatavuka mwaka wa kwanza. Anaonekana ni immature na mentally incapable. Unatafutiwa chuo? Rushwa zingine tunaziombea wenyewe.
 
Uko sahihi. Lakini,mfumo wa TCU ulidahili wanafunzi wenye ufaulu mdogo kwenye kozi zinazohitaji ufaulu mkubwa. Kozi husika,na hata vyuo vikuu husika,zikashuka kiheshima.

Unaweza kuelezea vizuri? Kila chuo kina mahitaji yake,udahili wa UDSM na Tumaini ni tofauti. Udsm wanachukua mwanafunzi mwenye points 5 na kuendelea na Tumaini wanachukua mwanafunzi mwenye points 4,Mzumbe wanachukua mwanafunzi mwenyw points 4.5. Kila Chuo kina hitaji lake.
Mwanafunzi mwenye points 4 hawezi kusoma UDSM na Mzumbe kwasababu hawana vigezo,hawa ndio wanalalamika kwasababu walikosa nafasi ya kusoma UDSM.
 
Kwa nini atafutiwe? Kama huyo mtu anatafutiwa chuo basi hatavuka mwaka wa kwanza. Anaonekana ni immature na mentally incapable. Unatafutiwa chuo? Rushwa zingine tunaziombea wenyewe.

Sio kila chuo mwanafunzi anaweza kupata nafasi.
 
Sasa hivi kuna zaidi ya wanafunzi 60k wataomba udahili vyuo vikuu,kipindi cha nyuma walikua wachache ndio maana mfumo haukusumbua sana hila idadi ilivyoongezeka kwa kasi ndio wakatafuta jinsi ya kuwadahili bila ya kasoro kujitokeza.
Hii ndio tofauti ya miaka ya nyuma na sasa.
 
Inabidi Mhe Rais ashauriwe vizuri maanake hii italeta mkanganyiko kwa wanafunzi, kuna watu wataa-apply hata vyuo vitano.

TCU ilifanya vizuri sana kuharmonise. Ilipunguza kwa kiasi kikubwa application fees ambayo ninaona sasa mwanafunzi atatumia mpaka laki 3 kufanya application. Hata hivyo TCU kama chombo cha usimamizi kinachofanya monitoring and Evaluation ya vyuo, haikutakiwa kufanya hii kazi. Maana kuna vyuo vingine vingine vililetewa wanafunzi wasiofaa na kwa sababu vinahitaji ada vimewapokea tu. TCU imeshindwa sasa kuvisimamia vyuo na kuangalia ubora wa wanafunzi na walimu kwa sababu yenyewe imekuwa sehemu ya tatizo la kuleta wanafunzi wasio na sifa. Kwa sasa hakuna monitoring ya vyuo maana TCU kwa kiasi kikubwa ilijiingiza kwenye uendeshaji.
 
Mkuu kila jambo huwa linachangamoto zake, nashauri TCU waachiwe hili jukumu ilikuwapunzia gharama wanafunzi.
 
TCU ilifanya vizuri sana kuharmonise. Ilipunguza kwa kiasi kikubwa application fees ambayo ninaona sasa mwanafunzi atatumia mpaka laki 3 kufanya application. Hata hivyo TCU kama chombo cha usimamizi kinachofanya monitoring and Evaluation ya vyuo, haikutakiwa kufanya hii kazi. Maana kuna vyuo vingine vingine vililetewa wanafunzi wasiofaa na kwa sababu vinahitaji ada vimewapokea tu. TCU imeshindwa sasa kuvisimamia vyuo na kuangalia ubora wa wanafunzi na walimu kwa sababu yenyewe imekuwa sehemu ya tatizo la kuleta wanafunzi wasio na sifa. Kwa sasa hakuna monitoring ya vyuo maana TCU kwa kiasi kikubwa ilijiingiza kwenye uendeshaji.

Je matatizo uliyaandika yametatuliwa? Je huu mfumo mpya utatatua hayo matatizo uliyoaandika?
 
nashukuru Mungu nilisoma enzi za vyuo vikuu vitatu tu (UDSM-MLIMANI, UCLAS, MUHIMBILI), MZUMBE na SUA....... Tena nikaapa nikimaliza BSc sitasoma tena Bongomovie....... na kweli a dream came true...
 
Hivi nyie mnaotoa hii hoja mnaweza kutuambia ni namna gani mfumo wa manual admission utakavyoshindwa kutoa wanafunzi kwa hivyo vyuo mnavyoita vya ubabaishaji??

Truth be told, hapa JPM amechemka! Let's assume chuo cha ubabaishaji X. hivi kwa akili zenu mnadhani hakuna watakao-apply huko? Hivi mnaamini wote wata-apply kwenye hivyo vyuo mnavyoamini kwamba ni bora?!

Sasa je, wale walio-apply kwenye vyuo vya ubabaishaji, tena wakati huo ni chuo wenyewe ndio wanatoa admission... wakishawachagua hao wanafunzi ina maana hawatapata mikopo kwa sababu hawakupelekwa huko na TCU?

Huu mfumo wa manual utaleta shida sana tena sana!!! Siku hizi wanafunzi ni wengi maradufu kuliko uwezo wa kuchukua wanafunzi hao kwenye vyuo vyetu "bora!"

Matokeo yake, wanafunzi wengi watakuwa wanapigwa chini kutoka kwenye vile vyuo walivyotarajia wangepata. Unless awe ame-apply chuo zaidi ya kimoja, kinyume chake wengi wataishi wakisubiria second selection.

Na wengine wakikosa hawatakuwa na namna zaidi ya kwenda kwenye vyuo hivyo hivyo mnavyoita visivyo na ubora!! Aidha, watakuwepo pia watakaolazimika kusubiri hadi mwaka unaofuata!!!

Ingawaje binafsi sijasoma kwenye huu mfumo wenu mnaotaka kuupiga teke lakini huu mfumo ulikuwa unasaidia sana kuhakikisha kila mwanafunzi anapata nafasi!!

Hoja kwamba TCU ilikuwa inapangia wanafunzi vyuo ambavyo hawakuchagua ni hoja isiyo na msingi kwa sababu hata sasa haimaanishi ukichagua UDSM ndo lazima utapata!!!

Mtu anaweza kuamini kwamba kwamba ana sifa kwenye chuo fulani lakini kumbe kuna wengine wana sifa zaidi yake!!!

And remember, sometimes kupata admission is all about the art of applying!! Unaweza kuwa na pass safi kabisa lakini uka-appy course ambayo wanafunzi walifaulu sana na bado ukapigwa chini na hiyo pass safi zako!!!

TCU mtu kama huyo walikuwa wanampeleka kwenye chuo kingine!!!
Mbona zamani iliwezekana,hii system itawapambanua vyuo visivyo na sifa,namuunga mkono magu
 
Rushwa ilitawala TCU ndo maana sasa wanahaha hamna jinsi. Wamejitoa hata mhanga lolote liwalo na liwe maana kwenda kuongelea jambo hilo live kwenye TV vile bila woga hapo lazima kuna namna si bure. Nani hajui mfumo ule umewanyima wengi wenye matokeo mazuri vyuo bora? Ila wajue muda ndo utaongea. Enzi zao zimekwisha
Si kweli , eleza, na toa mifano. It is not just revelations!
 
Unaweza kuelezea vizuri? Kila chuo kina mahitaji yake,udahili wa UDSM na Tumaini ni tofauti. Udsm wanachukua mwanafunzi mwenye points 5 na kuendelea na Tumaini wanachukua mwanafunzi mwenye points 4,Mzumbe wanachukua mwanafunzi mwenyw points 4.5. Kila Chuo kina hitaji lake.
Mwanafunzi mwenye points 4 hawezi kusoma UDSM na Mzumbe kwasababu hawana vigezo,hawa ndio wanalalamika kwasababu walikosa nafasi ya kusoma UDSM.
Siyo kweli,,
Nina mdogo wangu, alipata div 1 point tano alitaka kusoma udaktari,wakampeleka kairuki university. Ada pale ni zaidinya milioni sita ilhali bodi ya mikopo inatoa 3.6 m hivyo mpaka leo tunalazimika kuongezea kiasi kinachopungua. Kuna watoto wengi wa masikini wanaamua kuacha masomo kwa kushindwa ku top-up.

Halafu pia, moja ya motivation ya mwanafunzi kusoma vizuri kidato cha sita, ni ili apate points nzuri aweze kusoma chuo kizuri. Si sawa, mtu anapata div 1 point saba unampeleka sijui stefano moshi, sijui sekuko, sijui st joseph. Vyuo, hata waalimu hakuna, mwanafunzi anasoma degree anafundishwa na tutorial assistant. Vidarasa havina hadhi ya chuo kikuu, wanafunzi wanaishi mitaani huku mabinti wakiishia kuishi kinyumba na wanaume. Ktk kipindi hiki kilichopita, ndipo tu eshuhudia mabinti wengi sana wakimaliza vyuo na kurudi nyumbani na watoto.
 
  • Thanks
Reactions: Qj_
Mfumo wa kupitia TCU ni bora zaidi ya ule wa zamani, hauleti usumbufu mkubwa kwa wanafunzi na ni vyepesi kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa wanapata nafasi. Kama kuna chuo ambacho kilikuwa hakifurahishwi na huu mfumo sababu kinapata wanafunzi hata chini ya "standard" zake ni wajibu wa chuo husika kujitangaza vyema kwa wanafunzi ili wakichague kama chaguo la kwanza.

Pamoja na kumkubali sana JPM ila hapa amekosea, yoyote aliyemshauri hakuwa sahihi, hata yale maamuzi ya kuzuia na kuhamisha wanafunzi wa udaktari kutoka UDSM kwenda Mlonganzila sio sahihi, muda bado upo, wafanye mazungumzo waendelee na utaratibu wa kupitia TCU, na Rais asipende sana kuingilia maamuzi ya watu wa chini yake yasiyo na athari kubwa kwa jamii.
 
Siyo kweli,,
Nina mdogo wangu, alipata div 1 point tano alitaka kusoma udaktari,wakampeleka kairuki university. Ada pale ni zaidinya milioni sita ilhali bodi ya mikopo inatoa 3.6 m hivyo mpaka leo tunalazimika kuongezea kiasi kinachopungua. Kuna watoto wengi wa masikini wanaamua kuacha masomo kwa kushindwa ku top-up.

Halafu pia, moja ya motivation ya mwanafunzi kusoma vizuri kidato cha sita, ni ili apate points nzuri aweze kusoma chuo kizuri. Si sawa, mtu anapata div 1 point saba unampeleka sijui stefano moshi, sijui sekuko, sijui st joseph. Vyuo, hata waalimu hakuna, mwanafunzi anasoma degree anafundishwa na tutorial assistant. Vidarasa havina hadhi ya chuo kikuu, wanafunzi wanaishi mitaani huku mabinti wakiishia kuishi kinyumba na wanaume. Ktk kipindi hiki kilichopita, ndipo tu eshuhudia mabinti wengi sana wakimaliza vyuo na kurudi nyumbani na watoto.

Kama alikosa nafasi MUHAS ni juu yake,labda alichelewa kuapply kwasababu jinsi unavyowai kuapply ndio jinsi chance ya kupata nafasi kwenye chuo husika inavyokua kubwa.
Mfano MUHAS wana idadi yao ya wanafunzi wanaowahitaji na kutokana na wanafunzi wengi kuhitaji kusoma hiko chuo wana wai kuapply.
Kuna dogo mwaka juzi alichelewa kuapply UDSM akakosa nafasi wakati alikua ana div 2,sasa hivi anasoma Chuo kikuu cha Iringa lakini malengo yake yalikua ni kusoma UDSM.
Kama mtu unataka chuo fulani na una vigezo wahi kuapply utapata bila shida ila ukichelewa lazima ukose.
 
Sidhani kama unasema kweli. CAS ina select automatically bila kuwa na mkono wa mtu! Muhimbili walikuwa wanachukua point ngapi mwisho? Kumbuka mfumo wa Kiwete.. merit, distinction???? ulikuwa una mitihani rahisi na hivyo wengi walikuwa wanapata div 1 ya point 3,4,5. Ushindani kwa mfumo wa zamani ulikuwa mkubwa. Kwa div huwezi pata point 5 ukakosa.
 
Kama alikosa nafasi MUHAS ni juu yake,labda alichelewa kuapply kwasababu jinsi unavyowai kuapply ndio jinsi chance ya kupata nafasi kwenye chuo husika inavyokua kubwa.
Mfano MUHAS wana idadi yao ya wanafunzi wanaowahitaji na kutokana na wanafunzi wengi kuhitaji kusoma hiko chuo wana wai kuapply.
Kuna dogo mwaka juzi alichelewa kuapply UDSM akakosa nafasi wakati alikua ana div 2,sasa hivi anasoma Chuo kikuu cha Iringa lakini malengo yake yalikua ni kusoma UDSM.
Kama mtu unataka chuo fulani na una vigezo wahi kuapply utapata bila shida ila ukichelewa lazima ukose.
kisu, hapana, CAS haina kuwahi. Kinachoangaliwa ni grades na siyo kuwahi! Div 2 huwezi kwenda UDSM, wenye div 1 wanakuwa wengi sana tena sana
 
Nimekupa mfano halisi,wenye div 2 wanaingia UDSM vizuri sana. Tena UDSM wanapokeq wanafunzi wengi kuliko vyuo vyote Tz.
 
Back
Top Bottom