News Alert: Huku ni kunitega au kunijaribu

luche1

Senior Member
Jan 18, 2017
144
107
Habarini wakuu, niende kwenye lengo husika, nakumbuka nikiwa shule ya msingi darasa la sita kuna madam mmoja alikuwa ananifuatilia sana kila akiniona lazima ataniita na kuanza kujisemesha Fulani Leo mbona umechafuka hivyo hujachomekea, shati hujanyoosha na mambo mengine mbalimbali.

Nilimzoea sana kwa maneno yake ikafika mahali nikienda ofisini kupeleka daftari kama hakuna walimu ananiita nikae pembeni yake na kuanza kunihoji maswali ya hapa na pale kuhusu somo lake, kisha naondoka nilichukulia kawaida sana wala sikuumiza kichwa kuwaza kingine kiumri nilikuwa mdogo.

Siku moja aliniita na kuanza kunisifia Fulani Leo umependeza sana punguza Michezo usichechafuka kama watoto wengine napenda nikuone ukiwa msafi muda wote nikamjibu sawa mwalimu, akiwa na walimu wenzake hanisemeshi anapita kimya kimya nilikuwa nikishangaa kwa nini madam Leo hujanisemesha wakati huo nimetoka kucheza mpira na kuluka salakasi vumbi mwanzo mwisho.

Nakumbuka ilikuwa siku ya mtihani wa kufunga muhula darasa la sita mwezi wa kumi na mbili somo la kiswahili madam kaja kusimamia, nilikuwa nimekaa na rafiki angu saizi ni msanii wa bongo fleva tumekaa upande wa katikati dawati la nyuma, madam akaja upande niliokaa Mimi akasimama kwa muda sana kama mtu mwenye wasiwasi mwingi akiangalia huku na huku anaenda mbele kidogo analudi nyuma tena akifika nilipo kaa nashindwa kuandika naanza kutetemeka nilikuwa sipendi kusimamiwa kalibu na mwalu wakati nikiwa kwenye mtihani.

Baada ya muda madam akasogea taratibu akaegemea ukuta kisha akaniponda chaki kichwani nikajikausha kama vile sikuona akaniponda nyingine nikainua kichwa kumtazama, hahaha nilishangaa madam ameshika karatasi kwa upande yenye majibu ya kiswahili moja mpaka hamsini, akaniambia kwa ishara andika haraka, mwanaume sikuchelewa nikajipinda kuandika majibu yote, baada ya kumaliza madam akaondoka kaenda kukaa mbele kwenye kiti, baadhi ya wanafunzi wenzangu walishitukia na jamaa angu aliona ule mchezo, nae nikampatia majibu ya maswali 44 tu mengine nikamdanganya tusije fanana hakuwa na uwezo sana darasani mwalimu wa somo asije shitukia.

Kwa kuogopa kupata 50 ya 50 nikajikoshesha maswali mawili kitu ambacho nilifanya kosa kubwa sana, mwanafunzi mmja wa mkondo A alipata 49, na Mimi 48 sikuongoza katika somo hilo, iliniuma sana madam akaniita akaniuliza Fulani imekuwaje nikamwambia nilichanganya wakati naandika, akasema sawa siyo mbaya lakini tokea hapo madam akaenda masomoni tukamaliza shule sijawahi kumuona tena mpaka leo, swali nalojiuliza alikuwa ananitega au alikuwa ananipenda kama mwanafunzi wake lakini kwanini alinipa majibu peke angu na kunifuatilia kila mala, sijawahi pata majibu kwa kweli, ebu ndugu zangu mniambie hii ilikuwa kunitega ama, nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu hakuwa anakupenda,ila alikuwa anataka kukuharibia maisha kwa kukupa majibu ya mtihani,ni wazi hakutaka uwe na mwelekeo mzuri kielimu,bora alivyokwenda kusoma,anyway tafuta namba yake ya simu,unaweza kula used k from tz
 
Back
Top Bottom