KERO Huduma ya Airtel kwa Wateja wa 5G ina walakini, iangaliwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Airtel kuna kitu wanaendelea kuwafanyia Wateja wao kwenye hizi router zao za 5G siyo kizuri.

Wanakwambia kuwa internet ni unlimited ila ukitumia kwa siku 20 internet wanaishusha speed, mfano mimi nalipia kifurushi cha 110,000 kwa mwezi ambacho speed yake ni 30 mbps ila kila nikitumia siku 20 internet wanaishusha speed.

Speed inakuwa 1.2mbps ikipanda sana inafika 2.7 mbps na nilienda ofisini kwao Morocco wakaniambia matumizi yangu ya Internet yapo juu wakasema hivi: “Mtu anayelipia kifurushi cha 110k wanampa 1TB akiitumia akaimaliza internet inashushwa speed”.

Je, wanakuwa na maana gani kusema unlimited internet? Hili jambo siyo sawa wawe wanawaambia ukweli wataje wao wakati wanawauzia hizo router.
 
Nalipia kifurushi 110k, na matumizi yangu hayazidi 200GB per month lakini hii router hakuna kitu mzee, tumepigwa. Speed yake ukiconnect kwenye 4G na 5G ni sawa na inakata sana yaani kuitumia kwenye vitu vinavyohitaji video rendering muda wote hutoboi, inawafaa watumiaji wa social media wale wa kuscroll short videos na youtube wataenjoy.

Mbadala ni nini tunaomba mrejesho wa router za makampuni mengine.
 
Nalipia kifurushi 110k, na matumizi yangu hayazidi 200GB per month lakini hii router hakuna kitu mzee, tumepigwa. Speed yake ukiconnect kwenye 4G na 5G ni sawa na inakata sana yaani kuitumia kwenye vitu vinavyohitaji video rendering muda wote hutoboi, inawafaa watumiaji wa social media wale wa kuscroll short videos na youtube wataenjoy.

Mbadala ni nini tunaomba mrejesho wa router za makampuni mengine.
Naskia supa kasi wanakula maisha ila sina uhakika.
 
Ni bora usinunue Router za 5G za Airtel utanishukuru Baadae Halafu ukiwatafuta Wanakwambia Tupe number yako na ya kifaa lakini hakuna kitu wanachofanyia kazi; mimi mwenywe nimelipia 110000/= lakini nikiingia kabisa kwenye domain nakuta message eti kifurshi chako kimeisha what a mess!!
Inakuwaje Unlimited ikaisha! Wanakwambia 5G lakini hiyo 5G ni sio sehemu zote, basi wakupe 4G lite Hakuna kitu ni Ujinga tu..
 

Attachments

  • Screenshots_2024-04-17-08-23-54.png
    Screenshots_2024-04-17-08-23-54.png
    156 KB · Views: 6
Mi nashangaa pamoja na malalamiko ya miaka yote toka kwa watumiaji wa airtel bado kuna watu wana ujasiri wa kununua hadi router zao, airtel inajulikana toka zamani huo mtandao wanakupa vifurushi vinono ila internet utajua mwenyewe utakakoipata, mtu unafurahia kupewa GB 10 kwa 5000 kumbe ni danganya toto tu mwisho wa siku unajikuta hadi kifurushi kinaisha umewaachia GB zao hujatumia hata nusu sababu ya speed ya internet
 
Back
Top Bottom