Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma

Mkuu kalou
Mimi sijawahi hata kupanda basi achilia mbali ndege!

Niko huku kijijini Bariadi ambako usafiri wetu ni mikokoteni ya kuvutwa na ng'ombe lakini tunaishi kwa furaha kwa sababu dunia yetu inaishia hapa kijijini.

Wakati tunasubiri tamko la serikali, siyo vibaya kuendelea kujiuliza maswali ya hapa na pale.

Mh! Sasa nimekuelewa sana.
 
Ni kweli Mkuu ukitulia bila hamaki utaona report either haijakamilika au ni dhaifu,PAC wanatoa ushauri kiundwe chombo cha uchunguzi ili kujua kwa nini kina Tibaijuka na wenzie walipewa zile fedha,na wachunguze kama walitoa taarifa kama sheria ya utumishi inavyosema.Sasa najiuliza PAC walishindwa vipi kuwaita kina Tibaijuka kuwauliza kwa nini walipewa na kama walipewa je walitoa taarifa kwa uma!!!Ni maswali rahisi ambayo PAC wangepata majibu kabla ya kutupatia report yao.
 
hivi wewe muajiri waku huwa anakulipa mshahara wako wote ukalipe kodi mwenyewe???

---- vipato ambavyo kodi huwa inalipwa kutoka kwenye source na vingine huwa kodi inalipwa baada ya kupoke malipo
 
Mkuu maswali yako ni ya msingi sana na nafikiri tatizo tulilokuwa nalo sisi Watanzania ni kuwa tunakuwa always obsessed na events kuliko logic na wanasiasa wanalijua hilo. Wakati wa EPA na Richmond akili yetu ilihama tukaanza kuongelea watu badala ya issues.

Kila kitu kumekuwa politicized nchi hii. Ninachelea kusema hii escorw scandal is driven by vendetta and the panacea will never be obtained

Kaka ndivyo tulivyo watanzania wavivu wa kufikiri
 
pesa ita baki kua ya umma kwasababu kuu moja.......serikali hawana chanzo cha mapato/kupata pesa zaidi ya kodi.....ss kama ni pesa zilizo tozwa kodi kutoka kwa makampuni,ina mana kwamba hiyo pesa ina mahusiano ya moja kwa moja na umma........tunapo sema 'pesa ya serikali' ina mana ni pesa ya waTanzania haijarishi chanzo chake ni kipi"msaada wa waisani au la!" ita baki kuwa ni ya TZ.......

SWALI
Sasa hiii lugha pesa siyo ya umma ni ya serikali ina mana gani?

serikali ni nani na umma ni nani??

je?serikali ina weza kuwa na pesa pasipo kuwepo UMMA wa waTZ??

maswali hayo hapo juu yakijibiwa nazani hapata kuwa na haja ya mimi kudai tena pesa za ESCROW

"bring back our money"
 
Kila aliyekula pilipili lazima atawashwa tu kwani ndivyo wahenga walivyosema, kama haukula pilipili utawashwaje? Kuwajibika ni bora lakini kujiwajibisha ni bora zaidi. Ni vema kila mwenye dhamana akajitaabisha kwani asipojitaabisha kuna mtu atamtaabisha. Viongozi waliojichosha kutumia akili na nyadhifa zao kuzuia yaliyojiri sasa watamwona Kafulila na Zito ni wabaya. Hawa nao wanafanya wajibu wao wasijetaabishwa. Kazi ndo imeanza na lazima tufike
 
Kuna baadhi ya watu wanalijongea sakata ya IPTL huku wakiwa wametanguliza emotions badala ya fikra na mitazamo inayojenga hoja zenye maswali yaliyoko ndani ya hoja zilizoko mbele yetu.

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Kamati kufuatia matokeo ya ukaguzi maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania, Mhe. Zitto amenukuliwa akisema, maelezo yaliyotolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA na pia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yalidhihirisha kuwa sehemu ya pesa au pesa zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa ni pesa za Serikali.

Baada ya kuyapitia Maelezo ya CAG, TAKUKURU NA TRA nimegundua hayathibitishi kinagaubaga kama pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kama sehemu ya fedha au fedha zote zilikuwa ni fedha za umma.

Viongozi wa taasisi hizi katika matamshi yao wanaonekana hawana uhakika bali wanaongozwa na dhana ya kudhani ambayo kisheria haitoa majibu ya uhakika katika uharisia wake.

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Zitto alinukuliwa akisema,

Mheshimiwa Spika,
wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma.

Katika mahojiano hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na umiliki wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali


Kamishna Mkuu wa TRA


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU


Kuna sentesi katika maelezo ya viongozi wa CAG, TRA na TAKUKURU ambazo zinaacha maswali mengi badala ya majibu.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anasema,
“… Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu..’’
Hoja hapa ni neno TUNGESEMA badala ya TUNASEMA/TUMESEMA. Kwa lugha nyingine, HAWAKUSEMA.

CAG anamalizia kwa kuonyesha hana uhakika kama kuna fedha ya umma au la katika Escrow akaunti.

Hoja ya msingi, Kwa nini CAG kusema, Jibu ni kwamba, CAG hakusema kwa sababu hana uhakika.

Kamishna Mkuu wa TRA katika kunukuliwa alisema,

“… TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT..’’


Hoja ya msingi hapa,

Neno ILITAKIWA KULIPWA kwa lugha nyingine HAIKULIPWA.

Swali la kujiuliza, Kwa nini TANESCO walipe pesa ya TRA kwenye Escrow akaunti badala ya kulipa TRA.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yeye anadai bado wako kwenye uchunguzi lakini uchunguzi wao umejisimika kwenye maoni ya CAG, kwa lugha nyingine, TAKUKURU haijafikia uamuzi wa mwisho katika uchunguzi wake.

Hii dhana ya PAC ya kutoa hitimisho kama Tageta Escrow akaunti ilikuwa ni fedha za umma imetoka wapi wakati hata wachunguzi hawana uhakika?

NOTA BENE:
Haya maelezo nimetoa kwenye hotuba ya Mhe. Zitto ambayo iko HAPA

Tunaomba tueleweshane na kuelimisha katika mtazamo na fikra za kujenga na siyo kashfa na matusi.

Ndugu Ng'wamapalala. Una hoja ya msingi au una maswali ya kufikirisha zaidi. Binafsi kabla ya kuzijibu hizi hoja zako naomba nitafute uhalali wa Rugemalila wa VEP kutoa pesa kwa viongozi wengi walio kwenye nfasi ya kufanya uamuzi kwenye suala hili au wenye ushawishi katika mauumuzi. Je ni AG, Waziri ect ni haki kupokea pesa za mzabuni wa serikali katika zabuni ambayo bado ina utata???
 
Last edited by a moderator:
The fact remains....hakuna mtu aliyeitolea pesa jasho anaweza kumpatia mtu binafsi bilioni 1.6 just like that bila kuwa na ajenda ya siri. Viongozi hawa tumewachagua na kuwapa dhamana ya kutuongoza. Is it right and just for them kuweka maslahi yao binafsi bila kutujali sis watanzania? I respect your views on this but kuna maswali mengi bado hayajajibiwa na wote involved. are you trying to tell me hata hao wafadhili hawajui ni kwa nini wamesimamisha hiyo misaada pamoja na kwamba they flagged this Tanesco-IPTL deal kuanzia mwanzo?I fail to understand mtu anavyosema kuwa hakuna kitu kipya kwenye ripoti,kwa hiyo hicho cha zamani ni kipi?Is it right and just kuwa less than 10% ya wananchi ndio wanatumia umeme?Is it right and just watoto,kinamama wafe mahospitalini kwa kuwa hakuna dawa wakati mtu anapewa 1.6bn?! Kama kweli hakuna money laundering, can we all explain ni kwa nini mtu aende bank na kutoa more than USD 1mn cash?Really?!Let's get serious jamani.
 
Pesa ni za umma kwa sababu ziliwekwa BOT na Tanesco ambalo ni shirika la umma na zikatolewa bila kukamilisha sababu ya kuwekwa kwake.
 
Wezi wanajarib kufurukuta lkn hatuwez waelewa zaid ya kuachia nafas zao.hayo mapumba yao watapeleka mahakamani
 
Ninashukuru sana kwa sababu baadhi ya hoja zangu zimepata majibu kutoka kwa wabunge huku wengine wakijenga hoja na maswali kama niliyouliza katika bandiko langu la msingi.

Mapungufu mengine ya Kamati ya PAC ni kutowahoji wahusika wa mgao wa pesa badala yake wakaanza kuwahukumu bila kufahamu sababu za wao kupewa mgao wa pesa kutoka kwa James Rugemalila. Nadhani kuwahoji wapokeaji kungewasaidia sana kufahamu kilichokuwa nyuma ya mgao wa pesa, hasa mchakato uliopelekea mpaka uwekezaji wa mitambo ya IPTL nchini.
 
Job lusinde kawauliza kama si za umma CAG alienda kufanya nn? Si angeenda kuaudit mohammed enterprises? CAG anaudit mahala penye Mali ya umma!!
 
Ni kweli Mkuu ukitulia bila hamaki utaona report either haijakamilika au ni dhaifu,PAC wanatoa ushauri kiundwe chombo cha uchunguzi ili kujua kwa nini kina Tibaijuka na wenzie walipewa zile fedha,na wachunguze kama walitoa taarifa kama sheria ya utumishi inavyosema.Sasa najiuliza PAC walishindwa vipi kuwaita kina Tibaijuka kuwauliza kwa nini walipewa na kama walipewa je walitoa taarifa kwa uma!!!Ni maswali rahisi ambayo PAC wangepata majibu kabla ya kutupatia report yao.

PAC hawakutumwa kuaudit walitumwa kupitia ushaidi wa CAG na PCCB ...hawakutumwa kuanza upya walitumwa kazi ya kibunge, tayari vyombo vya pccb na cag vilishahoji ivo PAC wasingerudi kuanza upya, pia ingehitaji muda mrefu kurudia kazi ya PCCB ns CAG...ikumbukwe kufanya ivo CAG katumia zaidi ya miezi5.
 
Mkuu Ng'wamapalala, asante kwa hoja hizi, ila nasikitika kukujulisha kuwa humu jf tulikuwa tuko supposed kuwa ni the home of Great Thinkers, ila kiukweli ma GT humu ni wachache wao kila siku wanakuja na ideas, wengi humu ni ordinary mind ambao wao wanazungumzia matukio, na kundi kubwa zaidi ni akina sisi ma simple minds kila siku kuzungumzia watu!, hawa ndio mabingwa wa kutukana humu.

Hoja yako kwenye uzi huu ni kwa ma GT, nakuomba usishangae kama uzi huu utapata michango michache na mingi ya michache hiyo ndio hii ya akina sisi, tuko empty kabisa!.

Sasa nakurudisha kwenye mada husika!, TRA hawakuwa wakweli kuwe kule kwenye zile fedha kuna malipo ya TRA, malipo ya kodi za halali ambazo zingepaswa kulipwa ni zile kodi za transfer toka Mechimal -Pieper Link then to PAP. Sijauona mkataba wa IPTL lakini kwa reference ya mkataba wa Dowans, kodi zote zinalipwa na Tanesco!. Hvyo mwenye jukumu la kulipa kodi zote za serikali ni Tanesco, hivyo fedha zote zinazolipwa IPTL zilikuwa hazina kodi!, sasa kama hawa Tanesco wanaidanganya TRA eti kule wame deposit na kodi?!, how?!.

Malipo yale ya IPTL ni malipo kwa mujibu wa mkataba!. Mkataba ni makubaliano!. Kama Tanesco na IPTL walikubaliana kiwango hiki, na Tanesco akawa analipa, then fedha hizo ni malipo halali ya mkataba na sio fedha za umma!.

Kama Tanesco walikuja kugundua baadae kuwa wanalipa zaidi, ili hiyo ziada kurudi kuwa ni mali tena ya Tanesco, ilikuwa ni lazima wakae upya na IPTL na kukubaliana kwanza kama kweli kuna ziada, kisha wakubaliane viwango vipya, na utaratibu wa kulipana hiyo ziada!, hii sio jinai ni madai tuu ya kawaida kwenye biashara!.

Mimi sijaipenda Ripoti ya PAC imejikita kwenye matokeo tuu, Escrow ni matokeo tuu na sio chanzo!, nilidhani pia wange deal na chanzo nani ametufikisha hapa ndipo tukamalizia na matokeo!.

Pasco.

Pasco una maana mtu anapo kupa invoice vat inakuwa inclusive au laa. Sasa kama vat ni inclusive wewe una maana utalipa less amount ya vat au total invoice cost?
 
Mkuu maswali yako ni ya msingi sana na nafikiri tatizo tulilokuwa nalo sisi Watanzania ni kuwa tunakuwa always obsessed na events kuliko logic na wanasiasa wanalijua hilo. Wakati wa EPA na Richmond akili yetu ilihama tukaanza kuongelea watu badala ya issues.

Kila kitu kumekuwa politicized nchi hii. Ninachelea kusema hii escorw scandal is driven by vendetta and the panacea will never be obtained

tatizo lenu mnatumia lugha ngumu tunashindwa kuwaelewa. Kwa hiyo anayeongea kwa jazba au vijembe ndo tunamwamini maana tutaambulia jambo hisia. Nakwambia Chambo na mwalimu wa msingi na lusinde wameeleweka mpaka kwa mtogole. Sasa "vendetta" na ""panacea" ndo nini kwa mfano? lol
 
PAC hawakutumwa kuaudit walitumwa kupitia ushaidi wa CAG na PCCB ...hawakutumwa kuanza upya walitumwa kazi ya kibunge, tayari vyombo vya pccb na cag vilishahoji ivo PAC wasingerudi kuanza upya, pia ingehitaji muda mrefu kurudia kazi ya PCCB ns CAG...ikumbukwe kufanya ivo CAG katumia zaidi ya miezi5.

Sawa PAC hawakutumwa kufanya Audit bali kuifanyia kazi report ya CAG na PCCB je majina ya watu waliopewa fedha nayo waliyapata kwenye report ya CAG au PCCB?
 
Job lusinde kawauliza kama si za umma CAG alienda kufanya nn? Si angeenda kuaudit mohammed enterprises? CAG anaudit mahala penye Mali ya umma!!

Lusinde huyo huyo aliuliza kwa wale wanaoshauri PM na mawaziri wengine wawajibike jewao walishawahi onyesha mfano? ni mara ngapi katika vyama vya siasa yanatokea madai ya ufujaji wa fedha za ruzuku na hamna anayewajibika ? lakini alikwenda mbali zaidi kwa kutoa tuhuma dhidi ya mwenyekiti wa PAC ndugu zito kuwa amechukua pesa na vielelezoamevitoa hapo napo tunasemaje ?
 
Pasco una maana mtu anapo kupa invoice vat inakuwa inclusive au laa. Sasa kama vat ni inclusive wewe una maana utalipa less amount ya vat au total invoice cost?
Anayelipa VAT ni end user, invoices zote zinakuwa raised na IPTL na wana raise two invoices, ya capacity charge, na ya utility. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, all local taxes zitalipwa na Tanesco!. Hapa Tanesco ndie collecting agent wa TRA. Invoice ya IPTL ikienda Tanesco, inakuwa na VAT ambapo hao Tanesco, ndio wakati wa kulipa IPTL, walitakiwa kulipa ile invoice na VAT kuipeleka TRA. Sasa kama Tanesco waliremit kila kitu kwenye escrow, kosa ni la nani?!.

Siku zote ikitokea kodi stahiki hazijalipwa, huwa zinalipwa tuu wakati wowote, TRA watakuita, watakupa mpaka tarehe fulani uwe umelipa, muda huo ukifika kuna penalty fulani unalipishwa, hizi ni kesi za madai na sio jinai!.

Pasco
 
Back
Top Bottom